Sababu hamsini za Lowassa kuwa mgombea wa CCM 2015

22. Anapendwa sana lakini pia anachukiwa sana! anaweza kuwa mgombea aliyepitia tanuru kali hivyo atakuwa ameiva kukabili mgombea wa upinzani.

Anapendwa si kwa sababu ni mwema, ila ni mtoa mshiko (hongo kwa wenye njaa), chunguzi wanaompa support utakuta either wamepigwa jeki au wamepigiwa Pande na EL. Anachukiwa sana. Huu ndio ukweli kwa watu wanaoipendea mema nchi hii.
Kule Mwanza alitofautiana na mkuu wa wilaya wakati fulani alipokuwa waziri mkuu ilikuwa purukushani kwani EL alikumbushwa maneno ya mwalimu kwamba hafai kuwa kiongozi hata balozi wa nyumba kumi kumi.
Ni mwajiriwa wa serikali miaka yote, mali na mtaji biashara alizonazo alivipata wapi?
 
Nilianzisha thread hii ili tuweze kuorodhesha sababu 50 zitakazo muwezesha Lowasa kuteuliwa kuwa Mgombea wa CCM 2015, lakini naona watu wengi wamejadili kama vile mgombea wa CCM ndiye atakuwa Rais mwaka 2015!!! Nimeshangaa sana kuona hata watu ninao waheshimu sana kama Mzee mwanakijiji wakichangia kijujuu kama vile tunajadili Lowasa kuwa Rais na wala siyo Lowasa kuwa mgombea wa CCM!!
Sasa itabidi tuanzishe thread nyingine ikizungumzia sababu 50 zitakazo mzuia Lowasa kuwa mgombea wa CCM
 
Tafadhali ongezea sababu unayojua bila kupendelea wala kuonea zinazo mfanya Lowasa awe Mgombea wa Urais anayefaa zaidi kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu wa 2015
  1. Ni mwanachama wa CCM mwenye sifa za kuwa mchapakazi makini
  2. Ni mwanachama wa Chama ambacho kinatetea na kusimamia maslahi ya mafisadi hata kikapachikwa jina kuwa ni chama cha Mafisadi huku Mhe. Lowasa akiwa kinara wa watuhumiwa wa ufisadi hivyo kuwa na nafasi ya pekee kukiwakilisha vizuri katika sera hiyo.
  3. Anajua zaidi udhaifu wa Rais wa sasa kuliko wanachama wenzake wote; hivyo anaweza kurekebisha makosa yake kirahisi akifanikiwa kutinga ikulu.
  4. Anaweza kutoa uamuzi mgumu.
  5. aliisha onyesha kuwa anaweza alipokuwa Waziri Mkuu.
  6. Aliisha onyesha kuwa si King'ang'anizi wa Madaraka kwa kukubali kujiuzuru uwaziri Mkuu ili kulinda Chama chake
  7. Atakuwa rahisi kushindwa na Mgombea wa upinzani kwa sababu mapungufu yake na uwezo wake vinajulikana vizuri.
  8. Ataokoa CCM kutoka katika ombwe la uongozi lililoko hivi sasa
  9. Jasiri na haogopi mtu wala kumeza maneno
  10. Hajui kuvumilia wazembe na wababaishaji ambalo sasa ni tatizo kubwa miongoni mwa watumishi wa Umma
  11. Anawakilisha matajiri na wenye nacho ambao wana nafasi kubwa kwa sasa kwenye sera za CCM
  12. Anaamini kuwa serikali inabidi kuingia tena kwenye biashara ili wanachama wa chama chake wapate ulaji kama alivyoipa meno TBC kuwa taasisi ya kibiashara kwenye tasnia ya habari.
  13. Akifanikiwa kushinda atamlinda mtangulizi wake kwa makosa yote anayofanya kwa sababu urafiki wao haukuanzia barabarani.
  14. Ni Mkristo. Kwa kuwa chama chake kina udini uliokithiri kinachoamini katika siasa za udini, sasa mgombea wake ni lazima awe Mkristo. Angalia zamu hizi: Alianza Mkatoliki, Muislamu, Mkatoliki, Muislam.
  15. Anaungwa mkono na wajumbe wengi zaidi wa mkutano Mkuu wa CCM.

EL will only, i repeat only, become President of Tanzania over our dead bodies.
Tanzania will never reach such a low point. God forbid !
 
Wakuu, kwa tathimini yangu niliyofanya ndani na nje ya chama changu hivi karibuni nimeona ni jinsi gani viongozi waandamizi wa ccm na makada wengi wanavyomzungumzia lowasa kwamba ndiye atakayefaa kupeperusha bendera ya ccm mwakani na endapo jina lake kama halitapitishwa tujue kundi kubwa lililopo nyuma yake watafanya maamuzi magumu ya kuwapigia kampeni vyama vya upinzani vinavyotarajia kumsimamisha mgombea mmoja.kimtizamo ndani ya ccm lowasa pekee ndio anaonekana kuwa na upepo mzuri wa kisiasa tofauti na wenzake mosi pamekuwa na minongono heti kwamba lowasa ni mtu wa visasi na hata baba wa taifa alimwambia hawezi kuwa raisi wa tanzania kimsingi haya maneno hayajawahi thibitishwa kwa ushaidi wa kutosha.nawasilisha
 
CCM chama cha wahuni na washenzi wakubwa hawawezi kumpitisha lowasa kwani lowasa ana roho ya kulipiza kisasi
 
Kwa maoni yangu, naona hata akisimamishwa Lowassa bado ni 50%. Siyo kweli kuwa Lowassa anakubalika na wote ki-hivyo. Kuna wale wanaojua na kuamini kuwa Lowassa ni fisadi na hafai kuwa rais. Na kuna wale waliomponda kama kina Nape na Mwakyembe, huku ukimweka na Sitta na wengineo.

Ni wazi kuwa kama CC itamsimamisha Lowassa, basi zile kambi zilizokuwa zinampinga na kumponda ndiyo zitakuwa "zimekwisha" Na sidhani kama watakubali kirahisi hivyo kuangalia mwisho wao ukiwajongelea taratibu. Kwa vyovyote vile kumsimamaisha Lowassa kutafanya utokee mgawanyiko usio na suluhu ndani ya CCM. Nadhani kwa option hii, suluhu itakuwa ni "CCM ipoteze, wote tukose"

Hali kadhalika asipokuwa nominated, bado kundi lake ni powerful. Ni wazi bado kutakuwa na mpasuko, ingawa siyo wa hatari kama ambavyo itatokea pindi akiwa nominee.

Kwa hiyo vyovyote vile, naona hali ya CCM siyo nzuri sana. Na haijalishi ni nani anasimamishwa.
 
Wanachadema watakaompigia Lowasa kampeni na kura akipitishwa na ccm waweke like hapa.
 
Pengine ndo maana anagonga vichwa vya habari za siasa kila siku kwa miaka kadhaa sasa. Pengine ndo maana hata kina Sitta na Membe huacha kuongelea hoja majukwaani na badala yake kumwongelea Lowassa tu!
 
Ukweli lazima tuongee watanzania tumechukizwa sana na hiki chama cha ccm.kwa tabia ambazo viongozi wanawafanyia watanzania.ndio maana hata rowasa tunaona nae atatuletea machungu yaleyale.nyinyi mlioko mjini hamuwezi ona taabu na shida wanazo pata watu wa vijijini ukweli ni mateso.
Ccm hata atoke nani hakuna msafi.
 
Ukweli lazima tuongee watanzania tumechukizwa sana na hiki chama cha ccm.kwa tabia ambazo viongozi wanawafanyia watanzania.ndio maana hata rowasa tunaona nae atatuletea machungu yaleyale.nyinyi mlioko mjini hamuwezi ona taabu na shida wanazo pata watu wa vijijini ukweli ni mateso.
Ccm hata atoke nani hakuna msafi.

Hata hao uwadhaniao ndiyo siyo nakuhakikishia.

Huu ni mchezo mchafu na wa kipuuzi.

Hivyo basi huna budi nawe kuupuuza na watu wake.

Siasa haitaki kujaribiwa kwa mantiki hiyo hata kiongozi wake hatakiwi kujaribiwa bali kuaminiwa.

Na hapo sasa utakuwa ukeibua mjadala mpana sana maana utakuwa watambaa na kitu chamkuliwa "IMANI" ambalo ndo tatizo kubwa la Ulimengu wa sasa/ kifisadi/ faasiki.

Ahsanta nina mangi mno ila tosheka na kionjo hiko najielekeza uwanja mwangine tena kusahihisha fikara potovu/ zenye kasoro/ziso sahihi.

Ntarejea .....
 
1: Hana utawala wa pamoja. Utaona anawaachia wenzie (katika bunge na bunge maalum) kuweka sheria na katiba mpya bila yy kujali watakavyo viweka. Hukaa kimya. Tafsiri ni kuwa ziwe/iwe nzuri au mbaya havimusumbui. Maanake atakuwa ana maamuzi ya kimya kimya ya kwake. Hii ni hatari! 2: Hana nafasi na watu wadogo hasa wakulima. Hutasikia akiwasemea.
 
Back
Top Bottom