MWANALUGALI
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 601
- 34
Tafadhali ongezea sababu unayojua bila kupendelea wala kuonea zinazo mfanya Lowasa awe Mgombea wa Urais anayefaa zaidi kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu wa 2015
- Ni mwanachama wa CCM mwenye sifa za kuwa mchapakazi makini
- Ni mwanachama wa Chama ambacho kinatetea na kusimamia maslahi ya mafisadi hata kikapachikwa jina kuwa ni chama cha Mafisadi huku Mhe. Lowasa akiwa kinara wa watuhumiwa wa ufisadi hivyo kuwa na nafasi ya pekee kukiwakilisha vizuri katika sera hiyo.
- Anajua zaidi udhaifu wa Rais wa sasa kuliko wanachama wenzake wote; hivyo anaweza kurekebisha makosa yake kirahisi akifanikiwa kutinga ikulu.
- Anaweza kutoa uamuzi mgumu.
- aliisha onyesha kuwa anaweza alipokuwa Waziri Mkuu.
- Aliisha onyesha kuwa si King'ang'anizi wa Madaraka kwa kukubali kujiuzuru uwaziri Mkuu ili kulinda Chama chake
- Atakuwa rahisi kushindwa na Mgombea wa upinzani kwa sababu mapungufu yake na uwezo wake vinajulikana vizuri.
- Ataokoa CCM kutoka katika ombwe la uongozi lililoko hivi sasa
- Jasiri na haogopi mtu wala kumeza maneno
- Hajui kuvumilia wazembe na wababaishaji ambalo sasa ni tatizo kubwa miongoni mwa watumishi wa Umma
- Anawakilisha matajiri na wenye nacho ambao wana nafasi kubwa kwa sasa kwenye sera za CCM
- Anaamini kuwa serikali inabidi kuingia tena kwenye biashara ili wanachama wa chama chake wapate ulaji kama alivyoipa meno TBC kuwa taasisi ya kibiashara kwenye tasnia ya habari.
- Akifanikiwa kushinda atamlinda mtangulizi wake kwa makosa yote anayofanya kwa sababu urafiki wao haukuanzia barabarani.
- Ni Mkristo. Kwa kuwa chama chake kina udini uliokithiri kinachoamini katika siasa za udini, sasa mgombea wake ni lazima awe Mkristo. Angalia zamu hizi: Alianza Mkatoliki, Muislamu, Mkatoliki, Muislam.
- Anaungwa mkono na wajumbe wengi zaidi wa mkutano Mkuu wa CCM.