Sababu 5 kwamba nyumba yako ipo katika hatari ya kuungua kwa moto wa short ya umeme

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461

SABABU YA NYUMBA KUUNGUA KWA TATIZO LA UMEME NA SOLUTION ZAKE



Habari wanajamvi,

Napenda kuwakaribisha katika majadiliano ya tatizo hili ambalo limekuwa likisababisha majanga makubwa sana hapa kwetu Tanzania kutokana na hasa kuongezeka kwa matumizi ya umeme..

Uchambuzi nitakao utoa hapa ni kwa majibu wa elimu yangu ya umeme pamoja ufahamu wangu juu sheria ya umeme ya kimataifa IEE regulation.

Pia uchambuzi huu utazingatia British Standard of the IET Wiring Regulations.Kwani mfumo yetu mingi ya umemeya Kiafrika hata ule wa Tanzania ume-copy kutoka katika regulation hizi kubwa mbili duniani.

Nasababu ya kutumia IET wiring regulation ambayo ni ya British standard 7671 ni kwa sababu inazungumzia sheria na kanuni za umeme wa kiwango cha 230V kwa single phase.Ambao ndiyo shirika la umeme Tanzania Tanesco linausambaza kwenye makazi ya watu.

1.MAKOSA YANAYO SABABISHWA NA MAFUNDI WIRERING

(a). Overload of power supply wire:Hii husababishwa na line moja ya power supply kutoka katika main switch kutumika kusambaza umeme katika vyumba vingi.

Mfano nyumba nyingi mafundi hutumia 2.5 mm[SUP]2[/SUP]wire kama supply ya kwenye vyumba,supply hii hutumika kama junction supply ya vyumba vingine.

Wire ya 2.5 mm[SUP]2[/SUP] kitaalamu mwisho wake wa kupitisha current kiusalama ni 20Ampere ikitokea current zaidi ya ishirini ikalazimishwa kupita katika waya ya namna hii husababisha waya kupata moto,kama hali hii itakua kubwa sana waya huu huungua.na huenda ukasababisha moto.

Mfano katika layout hii katika picha.

a.jpg a.jpg


(b). Current ya Miniature Circuit Breaker(MCB) kuwa kubwa kuliko current ya wire.
Mfano wire wa 2.5 mm[SUP]2[/SUP] tumeona kuwa una uwezo wa kupitisha 20Ampere kiusalama
Hivyo MCB yake inatakiwa iwe ya 20Ampere.

Lakini mafundi wengine kwa kujua au kuto kujua hujikuta wanafunga MCB zenye current kubwa zaidi ya wire husika hali hii huweza kusababisha wire husika kuungua kwani MCB itashindwa kujizima hata pale wire itakapo kuwa imefikia kiwango chake cha mwisho cha kupitisha current.



Matokeo yake wire husika unaweza kuungua na kusababisha moto.

Mfano wa MCBs;-
aa.jpg


Viwango sahihi vya MCB na size ya waya zake zinazo shauliwa kimataifa ni hizi hapa.

1.5 mm[SUP]2[/SUP] cable - 15 amp maximum circuit breaker.
2.5 mm
[SUP]2[/SUP] cable - 20 amp maximum circuit breaker.
4 mm
[SUP]2[/SUP] cable - 25 amp maximum circuit breaker.
6 mm
[SUP]2[/SUP] cable - 32 amp maximum circuit breaker.
10 mm
[SUP]2[/SUP] cable - 40 amp maximum circuit breaker.


(c). Loose Connection katika maungio ya waya na kwenye vifaa vinavyo funga waya kwa screw.

Kama fundi hato kaza waya vizuri wakati wa kuziunga pamoja katika viungo vya screw au waya kwa yaya ni chanzo kikubwa cha kutokea kwa cheche ambazo hatimaye huweza kuanzisha moto.

8fce76e3e7aa201ab950bb0a3fa6d8805ed0a165.jpeg 555.jpeg 2007_0629_outlet.jpg ar137882651155578.jpg


(d). Tabia ya mafundi umeme kukubali kuunga mfumo wa wiriring wa nyumba nyingine dhidi ya nyumba nyingine.

Kwa kawaida Tanesco huingiza umeme katika nyumba kutokana na plan pamoja na mahitaji ya kiwango cha umeme cha nyumba husika(Kilowatt Hour).Hili hujumuisha ukubwa wa size ya waya wa kuingiza umeme katika nyumba yako n.k

Pia waya unao ingiza umeme kutoka katika meter kwenda ndani ya nyumba (tell wire)mara nyingi size yake hutegemea mahitaji ya nyumba husika.

Hivyo nyumba inapo pewa umeme hua imejitosheleza kwa mahitaji yake binafsi kitaalamu.
Inapotokea nyumba nyingine ikaungwa katika mfumo huo wakati plan yake haikuhusishwa wakati wa kufunga umeme katika nyumba ya awali hali hii hupelekea OVERLOAD katika tell wire hali ambayo inaweza kupelekea wire hiyo kuungua na kusababisha moto.

aaa.jpeg



2. MAKOSA YA SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME

(a). Kuto funga Vilinda circuit wakati wa kufunga meter za umeme.
Shirika la usambazaji umeme ni lazima lihakikishe linaweka vifaa vya kulinda nyumba husika dhidi ya matatizo ya umeme.

Shirika la umeme ni lazima liweke vifaa kama vile CUT-OUT au CRCUIT BREAKER kabla ya umeme haujaingia katika METER ya umeme au ndani ya nyumba.

kama inavyo onekana katika picha.

IMG_0352-SCALED.jpg ElectricBox_small-6.jpg iii.jpeg


Ufungaji wa vifaa hivi ulikua unazingatiwa sana zamani(sababu licha ya kuwa kama fuse CUT-OUT zilitumika kukata umeme katika nyumba pale mteja akishindwa kulipa bill ya umeme).

Sasa baada ya kuingia kwa meter za LUKU imeonekana kama CUT-OUT hazina maana tena hivyo suala lake la kutumika kama kifaa cha kulinda mfumo wa umeme kama fuse limepuuziwa.

Kuna baadhi ya nyumba zimefungwa CUT-OUT hadi sasa licha ya kuwa zinatumia LUKU,pia kuna wenye bahati ambao mita zao zina Circuit brekers.
Tazama picha;-

00221327 f607e6fff98ecf4b0e1585ff7e4c1f5d arc614x376 w614 us1.jpg


Ufungaji wa umeme usio zingatia vifaa hivi,unaongeza uwezekano mkubwa wa kuto kea short ya umeme yenye madhara.

Kama umeingiziwa umeme katika nyumba yako halafu vifaa nilivyo vitaja hapo juu hujafungiwa hata kimoja(yaani umeme umetoka katika bracket na kuingia katika meter moja kwa moja bila kupitia katika CUT-OUT au CIRCUIT BREAKER )mfumo wako wa umeme si salaama ni haki yako kufungiwa vitu hivyo una haki ya kudai kwa usalama wa nyumba yako.

(b). Miundo mbinu mibovu ya shirika la ugavi wa umeme.

Hali hii hupelekea kutatika katika hovyo kwa umeme,hali hii huweza kuzalisha Electrical Surges ambazo huweza kuleta madhara kwa watumiaji wa umeme.

3. KUCHAKAA KWA WIRERING ,VIFAA BANDIA NA VIFAA VIBOVU .

(a) Circuit breaker mbovu au feki .kuna circuit breaker nyingine mbovu au bandia ambazo zinashindwa kujizima pale short ikitokea,hakikisha unaijaribu circuit breaker yako mara kwa mara kwa kubonyeza "trip test" kuona kama inafanya kazi au la.

(b) Switch za umeme na extension cables ambazo ni mbovu au hazijakidhi vigezo(bandia)ni chanzo kikubwa cha moto katika makazi yetu.

Vifaa kama vile switch ambazo zimesha haribika vibadilishwe ili kuepuka kutokea kwa moto.
Pia epuka kutumia Extension cables ambazo ni bandia.
2007_0629_outlet.jpg wire-broken.jpg 6157076.jpg



(c) Wirering iliyo chakaa huweza kusababisha kutokea kawa moto kutokana na kulegea kwa viungo vyake ambavyo husababisha chehe,pia wire zake huwa zimeshambuliwa sana na wanyama na wadudu hivyo zinaweza zikagusana na kusababisha short yenye kupelekea moto kutokea.

4. KUFANYA MATENGENEZO YA VIFAA VYA UMEME NA KUVITUMIA BILA KUWA NA UTAALAMU.

Watu wengi wamekuwa wakifanya matengenezo ya vifaa vya umeme angali hawana utaalamu wa umeme.Vifaa vyote vya umeme ni lazima vikatengenezwa na mtu ambaye amesomea kazi hiyo.

Mfano watu wengi hubadilisha fuse katika mifumo mbalimbali ya vifaa vya umeme pale zinapo ungua.Ubadilishaji wa fuse hizi mara nyingi hufanyika kiholela bila kuzingatia kiwango cha current cha fuse husika.

Hali hii husababisha fuse husika kuto kukatika wakati short ikitokea hivyo huweza kupelekea waya kuuungua napengine kusababisha short ya umeme.
electrical-outlet-plug-catching-on-fire_61d607c1ea9286a6d760681fded81b44__3x2_jpg_300x200_q85.jpg


5. KUJAZA VIFAA VINAVYO TUMIA UMEME KATIKA EXTENSION CABLE KUZIDI UWEZO WAKE .

Extension cable zimetengenezwa kwa uwezo tofauti tofauti.Hakikisha hauzidishi vifaa vya umeme vinavyo chukua umeme kupitia extension cable yako ili kuepuka uwezekano wa extension cable hiyo kuungua.

rrrrrrrrr.jpg





SOLUTION

1. 1. Makosa haya makubwa matano yanaweza yakaepukika kwa kila mmoja kufata utaratibu na kanuni za ndani ya nchi na za kimataifa zinazo simamia matumizi bora ya umeme.

2. 2. Walaji wa umeme wawe na utaratibu wa kukagua mifumo yao ya umeme mara kwa mara Kupitia wataalamu wa umeme ili kuthibitisha usalama wa mfumo wake wa umeme katika nyumba yake.

Utaratibu huu wa ukaguzi ni muhimu ambapo mtaalamu atakagua kama wirering system yako imekidhi vigezo;ambapo mtaalamu wa umeme hutakiwa kuchukua vipimo maalumu na kuangalia kama mfumo wako wa umeme umekidhi kanuni na taratibu zinazo simamia mifumo ya umeme..

Baada ya vipimo mtaalamu huyo hutakiwa kuandaa ripoti yenye taarifa ya ukaguzi na kutoa matokeo ya ukaguzi huo wa mfumo wa umeme katika nyumba yako.

Mkaguzi atatoa majibu makuu matatu kulingana na sheria na kanuni za mifumo ya umeme majumbani kuwa mfumo wako wa umeme ni (Salama,Salama kidogo unahitaji marekebisho au si salama).Report hiyo ataisaini na kukukabidhi.

3. Ufungaji wa vifaa vinavyo tambua ishara ya kutokea kwa moto(fire sensor)

1. 4. Kuepuka kufanya matendo ambayo yatapelekea kutokea kwa tatizo la umeme ambalo linaweza kusababisha moto.

5.Kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika majumba yetu.

Not always electrical fault will give you a chance to correct your mistake.BE CAREFULLY!

Mawazo haya ni mawazo yangu binafsi kutokana na utaalamu na uzoefu wangu tafadhari yasihaririwe kwa machapisho mengineyo.

Imeandaliwa na Transistor 0685-060755
 
Ona jambo la kitaalam kama hili halina wachangiaji. Ngoja Bavicha wazushe jambo hapa, wachangiaji wangefikia zaidi ya 800. Nchi iliyojaa wajinga hutumiwa kwa ujinga wao. Ahsante sana nimepata maarifa mengi humu
 
Ona jambo la kitaalam kama hili halina wachangiaji. Ngoja Bavicha wazushe jambo hapa, wachangiaji wangefikia zaidi ya 800. Nchi iliyojaa wajinga hutumiwa kwa ujinga wao. Ahsante sana nimepata maarifa mengi humu

Wewe ndo unataka kubadili upepo
 
Pamoja na haya pia tuzingatie kuwa na vifaa vya kuzimia moto na familia nzima ijue jinsi ya kuvitumia na viwe vizima wakati wote tukumbuke kuna moto wa gesi mishumaa pasi nk nk unaweza ibuka
 
Back
Top Bottom