Jamani,
Hapa Ngeleja hawezi kusema eti alikuwa hajui lolote kuhusu hii barua aliyoandika Jairo. Kimsingi Jairo alipata malekezo toka kwa mabosi wake yaani Ngeleja na Malima. Kwanza inasema "Kama ilivyo kawaida yetu"
Haiingii akilini kusema kwamba haya yalikuwa maamuzi ya Jairo bila wakubwa wake kujua.
Wah Wabunge wanapojadili taarifa hii, ichukuliwe kuwa ni taarifa ya wizara, Jairo hajaiandika ile barua ya kukusanya mihela kama yeye D.Jairo, bali kama KM wa wizara husika. Sasa katika hili wakuu wa hii wizara watakwepaje panga atakalopigwa nalo Jairo??
Kama Jairo ataonekana ana makosa (kitu ambacho siyo rahisi kukwepa) basi Waziri na Naibu wake wamo. Kama wanataka mawaziri wapone basi lazima Jairo apone kuwaokoa hao mabosi wake.
Swala hili nalifananisha na mgombea mwenza kwenye mbio za Uraisi TZ. Kama mgombea mwenyewe akishinda then automatically mgombea mwenza naye anaukwaa u-makamu, na kinyume chake. Same applies kwenye issue ya Jairo. Atakapoonekana Jairo ana hatia tu, basi Ngeleja na mdogo wake hawawezi kupona. Huu ndo ukweli kama tunataka kuonyesha utawala bora tunaousema kila siku.