Uchaguzi 2020 Sababu 11 kwanini Tundu Lissu atapata ushindi wa asilimia ndogo kuliko Lowassa na Dkt. Slaa

JOYOPAPASI

Senior Member
Jan 10, 2016
172
500
*SABABU 11 KWA NINI TUNDU LISSU ATAPATA USHINDI WA ASILIMIA NDOGO KULIKO LOWASSA NA DR SLAA* Fuatana na *Joseph Yona*

yonapavea@gmail.com
0713802226

1: JPM anamengi yakuonekana aliyofanya kwa wananchi, Lissu hata jimbo lake tu hakuna chochote cha kuonyesha tokea amekua mbunge, mbaya zaidi kwa Sasa Hotuba zake zimejaa Uongo na utapeli Eti Ana Risasi kwenye UTI wa mgongo, Anacheza na UTI wa mgongo, Mara Risasi iko kisogoni.

2: Kila vita anayoingia #JPM anapata ushindi (MAKINIKIA, KORONA, KUJENGA UCHUMI NA MIUNDOMBINU).
Lissu ni ushindi wa maneno.

3: Lissu amejipanga kutumia tuhuma za uongo na Risasi za kimkakati kujinadi, wakati #JPM atakuwa na muda wa kutangaza na kuwaonyesha watanzania aliyowafanyia na Yajayo.

4: Taifa bado linamwangwi wa utisho wa kazi za #JPM na maamuzi magumu kama KORONA, Lissu kaanza udalali wa kutaka kutuaminisha watu wanakufa korona kipindi ambacho kila kanisa linatoa ibada za shukrani kwa Mungu kutupa rais Jasiri Kama *JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI*

5: Wakati wananchi wameaminishwa MABEBERU ni watu wabaya (NB Ubeberu si Rangi Bali vitendo, LISSU yeye anaonekana kutegemea watu hao ambao wapiga kura wanaamini ni wabaya kama watu wake wa karibu na Akiwa Tunduma amesema atafukuza Machinga woote wanachafua miji.

6: Tangu amepata Janga la kumiminiwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni Risasi Kila akisimama kuongea anaongea yaleyale hadi anaboa. Wakati Tunategemea #JPM atoe mambo mapya licha ya kuwa na mengi ya kusema.

7: Kanda ya ziwa huwa inaamua nani ashide uchaguzi kwa idadi kubwa ya wapiga kura, huko tumeshuhudia vitendo vingi vya maendeleo kuliko maneno ya kipinzani na malalamiko.
Wanatarajia Lissu utawafanyia nini zaidi ya Meli, Busisi, Barabara, Viwanda, zahanati etc ila naona umejipanga kuwapelekea tuhuma na maneno ya kujirudiarudia ya Risasi umekwama kiunoni.

8: Lissu maarufu mitandaoni ila katika uhalisia kwa wapiga kura Dkt Magufuli ni maarufu kuliko Lissu.

9: Lissu amekaa kama mtu anayetakiwa kusumbua mfumo sio kuwa kiongozi wa mfumo wa kuwasaidia watu.
Maneno yake, Body language yake haimfanyi mpiga kura aone kuwa hapo kuna jamaa mwenye utisho wa kuwa kiongozi wa nchi.

10: Hakuna mtu wa kuvujisha taarifa za siri za kiserikali na kiCCM ili ziwape wapinzani kiki kama enzi za Dr Slaa. Karibu watu wote wanahofu hata tu kulitaja jina la #JPM kimizaha. Kwa kipindi ambacho hakuwepo LISSU nchi imebadilishwa saikolojia kabisa jambo ambalo halihitaji miezi miwili kulirudisha.

11: Kwa sasa #JPM haonekani kama Kiongozi wa nchi tu, bali pia kama Kiongozi wa Kiroho.
Kuna watu leo wanamuamini #JPM kuliko hata viongozi wao wa kidini maana Alionyesha utegemezi mkubwa kwa Mungu ktk Corona kuliko hofu za viongozi wao.

Sio suala la miezi miwili kumtolea mtu imani.

Screenshot_20200821-120435_1.jpg
 

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,351
2,000
Jiwe ana mwisho mbaya mno, iwe ni kupitia sanduku la kura, udikteta ama karma.

Nauona mwisho wake wa taabu nyingi, fedheha, na majuto

Dhambi zake ni nyingi mno.

Huwezi kukosa akili kiasi unaamrisha binadamu mwenzako auawe mchana kweupe, huo ni Uhayawani na Ujinga wa kuvuka mipaka, hata Idi Amini hakutangaza kwenye TV live Wapinzani wake wauawe
 

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,314
2,000
CM ina mgombea dhaifu mno, nguvu yake huwa ni kukanyaga wengine wasiongee aongee yeye tu.

2015 alikutana na mgombea bubu

Mwaka huu anakutana na mgombea bora kabisa, msomi kamilifu wa Sheria na mjuzi kamilifu wa historia ya nchi yetu na dunia

Sasa mgombea wa CCM anajua Madaraja tu na matofali - ndo maana ukimsema tu anakurushia tofali miguuni likuumize, Hana kingine anachojua

So Huyu mgombea Urais wa CCM atakuwa anaongelea Matofalndo maana ukimsema tu anakurushia tofali miguuni likuumize, Hana kingine anachojua

So Huyu mgombea Urais wa CCM atakuwa anaongelea Matofali na madaraja tu? Na Uwanja wa Ndege wa kijijini kwao? Na Ndege za kumpeleka kijijini kula Krismas?

Kwake Uhuru na Ustawi wa raia si agenda?

CCM mna kazi sema mmebeba vipande vya tofali mikononi!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,715
2,000
Nilidhani una hoja kumbe ni utopolo! Unadhani watanzania wajinga! Hawaoni muuaji, mwizi, mkabila, mpiga risasi, mfunga watu etc
Joseph Yona huyu ni yule aliyekuwa Temeke akatekwa na wanaccm wakamlawiti na kumpiga picha kisha kumwambia aunge mkono juhudi la sivyo watatoa picha zake?
Duh, ccm ni watu hatari na wakatili sana
 
Jun 8, 2018
63
150
So what? OK na wewe umetowa maoni yako. The most important thing is fair grounds for all candidates regardless their political parties.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,952
2,000
Joseph Yona huyu ni yule aliyekuwa Temeke akatekwa na wanaccm wakamlawiti na kumpiga picha kisha kumwambia aunge mkono juhudi la sivyo watatoa picha zake?
Duh, ccm ni watu hatari na wakatili sana
Unaona kabisa ameandika utoto! Nilidhani kuna issue za ku discuss, kumbe ni takataka!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,554
2,000
Baada ya kuona umeandika namba yako ya simu na anuani yako ya barua pepe, nimefikia hitimisho la hoja yako kukosa mashiko. Zaidi utakua umeandika tu mipasho, porojo na kujikomba komba kwa huyo magufuli wako ili upate uteuzi.
 

Baikije

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
533
998
Picha ulizoweka zinatanabaisha upo upande upi wa shilingi, kifupi wewe ni jiwe hutosikia maumivu
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,782
2,000
Siku aliyetaka kumuua Lissu akikutana naye ana kwa ana ataanguka na kufa papo hapo. Kazi kubwa anayoifanya sasa ni kuhakikisha hakutani naye popote
 

jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
3,483
2,000
Still yote ayaonekani sababu yameshindwa kuondoa njaa kwa wananchi so work done ziko to zero
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom