Tatizo siasa imefanya hata uwezo wetu wa kufikiri umekuwa mdogo sana na kibaya ziadi hatujui tunachotaka ndio maana wanasiasa wanatuchezea wanavyotaka.
Tatizo sio ku-invest hizo hela kwenye ndege sababu hata tungeivest huko kwenye madawa ndio matatizo ya afya yangeisha ?
Tanzania ni maskini lazima tuinvest kwenye project zitakasaidia kukuza sekta mbalimbali za uchumi ili kuongeza pato la nchi ili tuweze kuhudumia hizo sekta za afya na maji
Tatizo kubwa la Tanzania ni usimamizi wa project zetu hata hizo hela zikipelekwa kwenye maji zinaweza zikatumika ovyo usione kabisa impact ya hizo fedha
Pamoja na mashirika mengi kuingiza hasara lakini serikali zao bado wanaendelea kuya-support kwa sababu wanafahamu impact yao,aviation industry inachangia karibia 35% ya GDP ya Dubai
Oh Lord! I like this observation:
Tatizo siasa imefanya hata uwezo wetu wa kufikiri umekuwa mdogo sana na kibaya ziadi hatujui tunachotaka ndio maana wanasiasa wanatuchezea wanavyotaka.
Ukweli ni kwamba, hata wewe ni muathirika wa hilo tatizo... I MEAN IT!
How come unatoa mfano wa Dubai ambayo mazingira yetu kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni hayafanani hata kidogo?!
FYI, post ambayo niliandika awali niliweka mambo mengi sana including suala la Emirates na mashirika mengine ya Dubai! Hata hivyo, yote ambayo niliandika nili-erase na kuacha ulichokuta kwa sababu nafahamu, watu aina yako mnasukumwa na siasa na kwahiyo kuwaambia uhalisia ni kupoteza muda! Mmeathiriwa na siasa na kuacha kuchezewa na wanasiasa! Wao wanachosema ni RIGHT, you don't argue!
Tena basi umesema:
Tanzania ni maskini lazima tuinvest kwenye project zitakasaidia kukuza sekta mbalimbali za uchumi ili kuongeza pato la nchi ili tuweze kuhudumia hizo sekta za afya na maji
Hiyo ni kweli kabisa lakini inawezekana pale yasipofanyika maamuzi ya kisiasa! Rational Decision Makers hawasukumwi na maamuzi ya kisiasa ambayo hayajali vipaumbele!
Huwezi kufikia hayo uliyosema endapo hufahamu au hutaki kufahamu uanze na kipi na umalizie na kipi!
Tanzania kuna sekta kibao za kiuchumi ambazo hazijawa exploited! Leo hii kama serikali inaandaa future investment portfolio, zenye impact kubwa kiuchumi na hata zenye socio-economic impacts, uwekezaji kwenye ndege KATU hauwezi kuwa hata miongoni mwa Top 5 Best Possible Investments in Tanzania!
Hayo unayosema wewe yangewezekana endapo tu serikali ingewekeza kwenye best investment alternatives ambazo probability ya return ni kubwa! Na hata kama return yake inachukua muda mrefu lakini socio-economic impact yake ingekuwa kubwa!
Ni hizo best investment ndizo zingenunua ndege kutokana na re-investments!