Rwanda yakataa uchunguzi huru wa kifo cha Msanii Kizito Mihigo anayedaiwa kujinyonga kituo cha Polisi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rwanda imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu ya kutaka uchunguzi huru kufanywa kuhusu kifo cha msanii maarufu wa muziki wa kiinjili Kizito Mihigo, ambaye alipatikana akiwa amefariki katika kituo cha polisi Jumatatu asubuhi.

Alifariki siku tatu baaada ya kukamatwa karibu na mpaka wa Burundi, polisi wakimtuhumu kwa jaribio la kutaka kutoroka nchi na kujiunga na la waasi linalopigana dhidi ya serikali ya Rwanda.

Bw. Mihigo alipigwa marufuku kuondoka nchini Rwanda kutokana na mashitaka yaliyopita dhidi yake.

Msemaji wa shirika la upelelezi la Rwanda, Marie Michelle Umuhoza, ameiambia BBC kwamba "Rwanda ni nchi huru inayojitawala na ambayo ina uwezo wa kuchunguza wa kitu chochote".

Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights Watch, Amnesty International na Commonwealth Human Rights Initiative yamekuwa yakishinikiza kufanyika kwa uchunguzi huru wa kubaini mazingira yaliyosababisha kifo cha mwanamuziki huyo aliyekuwa na miaka 38- amabaye alizoa umaarufu kutokana na ujumbe wake wa amani na maridhiano.

Siku ya Jumatatu, polisi ya Rwanda ilitangaza kuwa alijitoa uhai akiwa kizuizini.

Afisa wa Human Rights Watch ameiambia BBC kwamba uchunguzi huru utaangalia kamera za siri katika eneo ambalo msanii huyo alikuwa anazuiliwa.

Lakini Umuhoza amesema Rwanda tayari inafanya uchunguzi kuhusu kifo chake.

"Sioni haja ya kufanyika kwa uchunguzi huru, katika nchi huru", alisema, bili kuangazia uchunguzi wao utakamilika lini.

Pia amesema kwamba familia ya msanii huyo iko huru kumzika.

Baadhi ya marafiki zake na wanaharakati wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi wametilia shaka mazingira ya kifo chake.

Wamesema kwamba mwanamuziki huyo hakutaka kujiunga na kundi la waasi nchini Burundi na kwamba alitaka kwenda Ubelgiji ambapo alikuwa akiishi.

Pia wanaamini kwamba hakujiua katika kituo cha polisi alipokuwa anazuiliwa na kwamba huenda aliuawa.

Muziki wa Kizito ndio chanzo cha matatizo yaliomkumba. Katika wimbo mmoja alipendekeza kwamba kila mtu aliyeuawa katika mauaji ya kimbari ya 1994 anapaswa kukumbukwa awe Mtutsi ama Mhutu.

Wanasema kwamba mamlaka imeliona hilo kama changamoto ya wazi dhidi yake na kwamba mauaji hayo yalitekelezwa na Watutsi.

Wakosoaji wa serikali wanaamini kwamba kutokana na hilo Kizito alilengwa.

Mwanamuziki huyo alikuwa ameanza kuchunguzwa kuhusiana na madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkamata.

Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.
 
Ikiwa utumishi wake kwa Mungu haukuwa na mashaka, basi damu yake na iwapatilize walioimwaga.
 
Lakini ingekuwa ni Burundi imefanya ukatiri huo, saa hizi Rwanda ingehitisha kikao Umoja wa Mataifa kumlahumu Nkuruzinza na kupendekeza aburuzwe the Hague to face music.

Tangu lini mtuhumiwa akajinyonga kituo cha Polisi, hii inaingia akili kweli?
 
Back
Top Bottom