Rwanda Vs Uganda nani atashinda Vita?

Kwa hiyo afande maadui wanasainishana mikataba wasiumizane sana.
 
Rwanda anashinda mapema tu, niliona kwenye ule mgogoro wa mwanzo viwanajeshi vya Rwanda vilikuwa vinawadindia wanajeshi wa uganda na wanatepeta

Uganda hakuna kitu, labda kula Bata tu ila kwa vita hawawezi
 
Kwa hiyo afande maadui wanasainishana mikataba wasiumizane sana.
Hapana haiko hivo ila kuna makubaliano yalishafanyika huko nyuma nadhani kama mkipigana na ikatokea mambo yamefanyika kinyume na taratibu kuna uwezekano wa taifa moja kuadhibiwa nadhani moja ya vitu hivyo ni pamoja na kutowashambulia raia wasio na silaha na mengine nadhani na jambo la silaha za kivita lipo
 
Aiseee hizo taarifa nyingi sana umewapa zinatosha! Na kongine wa idadi ya wanyarwanda wanaotambuliwa na katiba ya Uganda anaijua? Hizo Million zilizoko uganda tu zinatosha kimaliza kazi huko.
Wa ku deal nao ni m7 na kabila lake sio kabila la waganda.
 
Sawa boss! Kweli Rwanda ni ndogo by size,na wao hilo wanalijua ndio maana ni wadogo kama nchi ila wa kubwa ki intelijensia na hilo liko wazi,kumbuka kumshinda adui wako ni kuwa na taarifa. Na kiingine katiba ya Rwanda inalipa jeshi ruhusa kumfata hadui aliko kabla haja attack Rwanda . In short intelijensia ndio kila kitu! Na nchi ikiwa corrupt sana kwenye mambo ya rushwa anytime inakua iko hatarini kwenye vita.
 
Battle za nn
 
Intelligence inakwambia nini kinaweza kutokea, lakini uwezo wa kukidhibiti hilo ni jambo lingine. Hakuna vita isiyo na dalili, issue ni je utaweza kupambana. Ukweli ni kwamba Rwanda is overrated. Na wanaoifananisha na Israel ni tatizo tu la uelewa. Rwanda inaionea DRC kwa sababu is a poorly managed giant, lakini sio Uganda; wana moja kati ya majeshi bora na yenye uzoefu mkubwa hapa East Africa.
 
Upo sahihi mkuu, hata USA ilitawaliwa na UK huwezi kuja kusema leo hii eti UK ataipiga USA kisa aliitawala huko ni kuongea kiushabiki..

Hata CIA wenyewe kuna muda flani huwa unafika wana declassify documents za siri walizozitunza kwa muda flani sikumbuki zaidi ni kila baada ya muda gani lakini huwa Wana huo utaratibu..

Jamaa anachozungumzia ni taarifa za kiintelejensia za Rwanda kuhusu UG lakini taarifa kwa muda wote huo ni useless, rejea Vita ya Israel na Hezbollah, Israel walichunguza ni wapi Hezbollah wanaweka roketi zao kwa miaka 6 lakini at the end walipokwenda kupiga kulikuwa hakuna kitu...

Nafikiri intelejensia za kivita zinakuwa na umuhimu wakati fulani na zinaweza kuwa useless pale hata adui tu akifahamu unajua Siri zake...

Kusema kwamba leo hii Japan ataipiga China kisa wanaijua nje ndani... Hio haipo

πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘Š
 
😁😁😁 Inaonekana hata kwny kisangani war Uganda itakua ilishinda kwa kishindo Sana πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Kwenye intelijensia kuna false feeding pia. Kama KGB miaka ya 1950s waligundua mashirika ya intelijensia ya Ulaya yametap waya wake wa Telegraph unaopita Ujerumani Mashariki, wakaanza kupitisha taarifa feki tu na za kiraia, zile muhimu wanazipitisha means nyingine. Mpaka wanaamua kusema tena Rais wa Marekani anafanya meeting na Soviet Premier walikuwa washawalisha pumba nyingi.

Hao Hezbollah wenyewe walijua Israel inavyojua wanaficha wapi silaha wakaziamisha kwa siri. Mgogoro ulipoanza Israel ilijiamini kama hata vita ikianza si tunajua maroketi yako wapi. Wakafanya mashambulizi maeneo yale ila haikusaidia, hii ilichangia Israel kuingiza wanajeshi nchini Lebanon

Kwenye WW2 Japan ndio nchi ilikuwa inaongoza kupuuza taarifa za intelijensia. Ingekuwa inazizingatia ingesumbua mno
 

Huwa hamna makubaliano ya silaha zipi zitumike unless ni vita ya kuzugia ikiwa na agenda nyuma yake (mfano kutengeneza mgogoro/vita ili kupata nafasi ya kufanya biashara au deals za magendo).
Jumuiya za kimataifa zinaweza kuhakikisha hamna matumizi ya biological weapons au nyuklia but ni ngumu sana kumpangia mtu silaha ya kutumia maana unakuta ndo advantage aliyokua nayo
 
Jeshi la Rwanda linasifika kwa Intelijensia imara na viongozi wenye elimu kubwa ya kijeshi lakini kwa kweli matokeo ya vita vya sasa hv huchangiwa na vitu vingi haswa Ubora wa zana ,nguvu na idadi ya washirika(allies) wa kila mmoja
 
kwani hao milioni 12 wote ni wanajeshi?...kwa tz hata kagame na nchi zote za eac, maziwa makuu na sadc, wanajua tz si ya kispot. imekaa kimya tu lakini muziki wake si wa kuchezea.....
 
Mkuu Uganda ina nguvu kubwa za kijeshi kuliko Rwanda,Museveni ni mjanja kuliko Kagame,Uganda kwa sasa ina vifaa Bora kabisa vya kijeshi kuliko hata Tanzania
 
Point yako mimi sijaiona kwakua rwanda alimsaidia m7 ktk hustle zake za muimomboa uganda lakini kumbuka pia m7 alimsaidia sana kagame kumuondoa havyarimana hivyo tuseme wote wanajuana battle lao mshindi atatokana na ninani mwenye washirika wengi ambaye kwa haraka haraka hata tukichukua majirani wanaozizunguka nchi hizo Uganda ana marafiki na uungwaji mkono wa nchi nyingi mf . DRC. TZ . Burund. n.k hao hawawezi msaidia kagame

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…