Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

''Very poor thoughts! Kujitoa kwao kuna athari KUBWA. Sahau wafanyabiashara wa Rwanda na Uganda, kuna mfanyabiashara wa TZ mwenye magari yapatao 500 yote yanasafirisha mafuta huko, na wengine na biashara zingine. Madereva, kampuni za upakuaji, bandari za nchi kavu, na mengineyo vita athirika sana, ajira za watu katika maeneo haya na familia zao zipo njia panda. biashara za mipakani na hata mabasi ya abiria vitaathirika kwa sababu wafanyabiashara wanasafiri humo, mbaya zaidi Kagame anaweza kufunga mpaka wake.
 
chenge.jpg

Na Raymond Kaminyoge,

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

"Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam," alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... "Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo."

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.

Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

"Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi," alisema.

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

"Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo," alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.

Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.

Hapa jipya hata silioni!
1) UGANDA NI MTUMIAJI WA BANDARI YA MOMBASA, KWA ASILIMIA KUBWA, SIKU NYIMGI TU!
2) KUHUSU RWANDA, WELL, HILI TULILITEGEMEA NA HALITUSUMBUI SANA
(Haiwezekani uchumi wa nchi ukategemea mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa kwenda kijiji fulani cha watu wenye uchu wa damu za binaadam wenzao! Hawa watu wanastahili 'SANCTIONS')
TUZITUMIE BARAKA ALIZOTUPA MUNGU ZA KUWA NA BANDARI KWA MANUFAA YA NCHI YETU WENYEWE, NA MAPATO YA USHURU YAWE ZIADA TU! WATANZANIA BADO KABISA HATUJATUMIA FURSA ZETU ZOTE NA TUKIAMUA TUNAWEZA TUKAWASHANGAZA, SIO TU HAWA MAJIRANI, BALI ULIMWENGU MZIMA! TUJITUME KIKWELIKWELI (KAMA MWAKYEMBE) NA TUACHE BLAH BLAH!

LAKINI TUSITISHIWE 'NYAU' NA YEYOTE, PENYE UKWELI TUSEME!

KAGAME AONGEE NA WAASI ILI AMANI IPATIKANE MAZIWA MAKUU NA HATUUACHI MSIMAMO HUU KWA GHARAMA YEYOTE!
 
siyo hujuma wala kurogwa. Kama ni kurogwa basi tunajiroga wenyewe. Tanzania hatuna customer care kwa wateja wetu. Ndio maana katupiga chini na soon atatutandika na bandari atachukua kiulainiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Chezea banyamulenge wewe....

watusi wana kitu kinaitwa kigali college of commandoos.chunga sana.kuna tetesi kuwa profesa juan mwakyusa aliuawa kwa amri kutoka huko.na laurent kabila???pk alivyotamka kuwa "i will jk at the right time and the right place" niliogopa sana.hasa ikizingatiwa kuwa amepenyeza mashushu wake sehemu nyeti nchini kwetu.SISI TUNAKENUA TU.

nishauri tu kwamba tujihadhari na hawa watu.tuwaflash out.warudi kwao. tumewahifadhi sana.wahenga walituasa"shukrani ya punda ni mateke".
 
let them Go nothing to worry! kuendelea kulialia na RWANDA&UGANDA kutumia bandari yetu au lah kwetu ni changamoto lakini pia tujue kua ni muda mrefu hawakupenda kufanya hivyo ila kwa sasa ndo wamejidhiirisha roho zao zikoje! Tumshukuru Mungu kwakua na bahari cha msingi apa ndo iwe chachu ya kusimamia na kuanzisha vyanzo vya mapato vingine..leo tunalaumiana lakini tujiulize je nchi ambazo hazina BAHARI chumi zao zinaendeshwaje? Tuwekeje kwenye GAS na italipa tu acha watuondolee Jams na usumbufu

Sawa kabisa. Waulize Japan na China wana bandari ngapi na mizigo ya nchi gani inapitishwa pale! Tukizalisha vya kutosha tunaweza kuzitumia bandari zetu wenyewe hata zisitutoshe!
 
''Very poor thoughts! Kujitoa kwao kuna athari KUBWA. Sahau wafanyabiashara wa Rwanda na Uganda, kuna mfanyabiashara wa TZ mwenye magari yapatao 500 yote yanasafirisha mafuta huko, na wengine na biashara zingine. Madereva, kampuni za upakuaji, bandari za nchi kavu, na mengineyo vita athirika sana, ajira za watu katika maeneo haya na familia zao zipo njia panda. biashara za mipakani na hata mabasi ya abiria vitaathirika kwa sababu wafanyabiashara wanasafiri humo, mbaya zaidi Kagame anaweza kufunga mpaka wake.

Waende tu, kwanza watu hawa wa malori ndio wanao changia leli isijengwe kwahiyo let them face the music now. Wamelobby sana leli isijengwe wanaleta malori yao yanaharibu barabara tu. Issue his mimi naiona ni positive kwetu itatusaidia kujirudi na kujenga kujenga leli hadi Burundi let say, then tuachie soko liamue, tutatape vizuri soko DRC. Watanzania tuache kulalamika let think positive this can be a gate way. Tuangalie hata hao wafanyabiashara wanolalamika hivi wanalipa kodi kiasi ganI?
 
Madini kila kona, ziwa bahari maji kila kona, ardhi kubwa yeny rutuba, gas na makaa ya mawe ya kutosha. Kweli vijimzigo hivyo ndo vitasababisha mtetemeko wa uchumi,afterall mapato ya bandari kwa 90% yanaishia mikononi mwa mafisadi. Hapo hakuna kuteteleka kokote.

Viongozi wakisema tumetosha kufisadi ngoja tupige kazi ndani ya miaka miwili maendeleo yanapaa kama drones hata kama bandari tukiifunga ikapitisha mizigo zero.

Wewe umenena big up mkuu
 
Hakuna haja ya kulalamika,cha msingi bandari ipanuliwe,vinunuliwe vifaa vya kisasa kufacilitate utendaji wa kazi,urasimu na kodi kodi ziangaliwe upya.kwa kufanya hivyo wenyewe watakuja

PERIOD!
Naunga mkono hoja mkuu! Na masuala haya ni 'long term', acha wajaribu kwingine waonje joto la jiwe kwanza!


 
Wajaluo wa Kenya waling'oaga reli kuelekea Uganga, Museveni akakimbilia Tanzania, akanza kusema mara tunataka kumfanya Nyerere saint mara ile mjaluo ------- nk. Yeye na Kagame wazushi tu, ila hapa Kagame ndo mzushi zaidi, sasa wamekutana na hawa wakabila wa Kenya, ambao wanajua pesa bila siasa haiwezekani, imeshakuwa fast trakking east africa community. Waendezao huko, ipo siku yatakuja kuwashinda.
 
uploadfromtaptalk1377346405814.jpg

Huu ni mkutano wa juni 25 uliohusu infrastructure ambao haukumuona JK
 
watusi wana kitu kinaitwa kigali college of commandoos.chunga sana.kuna tetesi kuwa profesa juan mwakyusa aliuawa kwa amri kutoka huko.na laurent kabila???pk alivyotamka kuwa "i will jk at the right time and the right place" niliogopa sana.hasa ikizingatiwa kuwa amepenyeza mashushu wake sehemu nyeti nchini kwetu.SISI TUNAKENUA TU.

nishauri tu kwamba tujihadhari na hawa watu.tuwaflash out.warudi kwao. tumewahifadhi sana.wahenga walituasa"shukrani ya punda ni mateke".

hawezi kitu huyo, ndiyo maana baada ya majibu yenye vina na matendo amenywea kama fisi aliyenyeshewa. Sasa anasubira huruma ya Tanzania kubakishwa au kuondolewa madarakani huruma ambayo kwa sasa haipo hata tone.
 
Sioni tatizo hata kama wataondoka kesho.

Nina uhakika Rwanda na Uganda si watumiaji wakubwa wa bandari yetu,kuondoka kwao hapatakuwa na tatizo kubwa kwetu.

Kikubwa tuweze kuwamudu hawa mafisadi na wote wanaohujumu uchumi wetu kwa kupitia bandari.
 
As long as tukifanikisha kuzima M23, CONGO itatulia na potential ya kunufaika na CONGO ni kubwa mno kulinganisha na EAC. Wewe utanufaika je na EAC ni kidogo sana. Uganda siku zote walikuwa wanapitishia mizigo mingi Kenya utakumbuka ile vurugu ya kenya ya mwaka 2007 baada ya kung'oa reli jinsi M7 alivyotukana.

Tuna potentials zote, na tuna kila sababu zote za kupiga maendeleo tena bila hata utegemezi wa nchi yoyote. Kinachokosekana ni commitment za viongozi wetu tu. Lakini wakiji commit hata kwa 30% tu hao jamaa wa kaskazini hawatuoni tena kwa mbali sana.
mkuu tusaidie katiba ibadilishwe, manake nahofia commitment will be a mere wish
 
Upande wa pili wakenya wanalalamika Dar port imechukua biashara za Mombasa port.....

kwa watumiaji wa bandari yetu wanaweza kukiri kwamba kuna improvement kubwa imefanyika...tukaze mwendo!!!
 
Bidhaa nyingi zinazokwenda Rwanda ni silaha na sishangai wakiamua kupitishia silaha zao nchi zingine wanazoona zinawaunga mkono kuendeleza 'GENOCIDE' Kongo! Hawa ni 'BA'GENOCIDE' wenzao!
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
Hii imetulia wafanyibiashara wanaangalia faida sio malumbano ya viongozi au Hanspope anaatarifa kuwa serikoli za Rwanda na Uganda zimepiga marufuku wafanyabiashara kupitisha mizigo Dar? I
 
Hii kitu lazima itakula kwetu.

Jamani acheni wasiwasi na hofu zisizo na msingi , jiweke katika nafasi kwamba tusingekuwa na bandari je tungeiashi au tusingeendelea? acheni hofu na kumbukeni hawa jamaa wote ni madictetor au wana misingi hiyo sansa saana wanatuonea wivu na kutufanya tuwe katika hakli ya kujidharau, tena ikibidi tuongeze kodi na cha msingi tuweke huduma sawa. wanatetemeke kuhusu banrari ya kimataifa ya bagamoyo. waende zao na ujinga wao
 
Kagame na baba yake Museveni hawana jipya ni majambazi yanayotaka kutawala milele....wavunje EAC tuone ni nani atakaenufaika...?wakipigana huku ndo wanakimbilia....wakiwa shwari Bongo mbaya....kweli shukrani ya punda....
 
Huyo Museveni na Kagama ni mijitu isiyo na hata chembe ya shukurani! Wote wamelelewa hapa Tanzania, wamesomea hapa Tanzania, tena Museveni alihifadhiwa Kambi ya Jeshi Kurasini(sasa hivi ni chuo cha polisi) na akasoma mpaka ngazi ya UDSM, na hako ka dikteta kapya (Kagema) kamesota sana kambi za wakimbizi humu humu bongo na hakana hata digrii kwa uroho wa kujiunga na jeshi la Museveni kakapata nafasi ya juu huko ndio kakapewa msaada wa kurudi rwanda na baba yake (Museveni) hivyo sishangai kwa haya wanayofanya, ni waroho wa madaraka! Tuachane nao mazima!
 
Y'all lames dint want to be members of EAC from the get go, why are y'all acting like ditched teenage girls now? move along to SADC, you have more clout there considering you fruits 'helped them in the struggle for independence'. After a few years we will know who the biggest winners and losers are.
 
Back
Top Bottom