Rwanda Air to acquire EA's first Airbus A330

Rwanda Air to acquire EA's first Airbus A330

Heshima kwenu wanajamvi.

Kanchi kadogo (Rwanda) na rasilimali chache ukilinganisha na nchi kubwa (Tanzania) yenye rasilimali nyingi kamatushinda katika sekta ya usafiri wa anga kwa kununua ndee mbili mpya aina ya Airbus A300.

Tanzania chini ya utawala wa CCM wa zaidi ya miaka 50 imeshindwa kumiliki hata ndege moja mpya badala yake imekimbilia ndege za kukodisha kwa bei mbaya.

Tunahitaji mabadiliko CCM imeshindwa kuongoza inastahili kuwekwa kando.

RwandAir to acquire EA's first Airbus A330 - The New Times | Rwanda

Siyo lazima wote tununue ndege. Mbona sisi tumenunua mashingingi ya kutembelea viongozi mengi kuliko nchi yoyote ile ya Kiafrica labda hata kuliko nchi nyingi za hata Ulaya na Asia.
Rwanda hawatuwezi bana!
 
Ngongo

Wameshindwa kununua hata pikipiki sembuse ndege? CCM ni laana kuna wakati nasema kwa nini mungu asishushe radi likawaangamiza pale Dodoma wanapokutana kupanga maovu juu ya Tanzania?
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi yetu imerogwa nadhani mwaka huu tusifanye makosa
 
Kanchi kadogo katatushinda tukicheka cheka kama tumepewa bia za bure
 
Hao ni ccm bwana, miaka 50 ya uhuru tunashindwa na rwanda. Halafu unataka tuisifie serekali eti imefanya mambo mazuri. I hate ccm and serekali yake.
 
Heko Rwanda. Hawa watu na wakenya ndio wanajitambua. Siis tunabaki kuchagua akili ndogo kutawala akili kubwa.
Tutasubiri sana.
 
Kainchi madogo kama Rwanda kameweza a sleeping giant anakoloma usingizini.
Jamani enough is enough tuache siasa kwenye ili LA uchumi wa inchi
 
Heko Rwanda. Hawa watu na wakenya ndio wanajitambua. Siis tunabaki kuchagua akili ndogo kutawala akili kubwa.
Tutasubiri sana.
Hii nchi tunatabia mbaya Sana sijui nn kinatupofosha. Ni ukweli usiopingika watanzani tuna matamanio ya vitu vizuri. Mf ukiona mtanzania mwenzako kafanikiwa kwenye mambo lake labda biashara au ajira unatamani kuiga ili ufike pale. Kitu Ch ajabu akili hiyo hiyo tunashindwa kuitumia tunapokua viongozi natoka ngazi mbalimbali kuiga mafanikio ya majirani zetu katika nyanja mbalimbali. Hivi kweli Rwanda wakutuzidi kwenye hili na mengine nchi ile Ni mama mkoa wa Mwanza kwa ukubwa km sikosei Ni kilomita za mraba 24,000 hivi. Hata mtasema nchi yetu kubwa sawa hata bado km watu wakimkakati tungeweka malenga kila miaka mitano tunaweka mkoa Fulani vizuri kwenye nyanja zote hilo halipo Dodoma imetushinda. Cha ajabu tunaongeza mikoa na wilaya zenye miundo mbinu hafifu hii iliyopo Tu bado Sana. Nachoka sana
 
Natumia nguvu nyingi sana kuukubali Utanzania wangu. Naabika mbele za mataifa wengine. Ni aibu sana ukilinganisha tuliyojaaliwa na hali zetu. Tuna kila kitu Tanzania. Ardhi na maji ya kilimo, bahari, madini, aaaghhh. Naamini kuna laana fulani tunayo Tanzania. Haiwezekani hatuna tunachoweza. Si reli, si ndege hata bandari yetu buree kabisa japo tumependelewa sana kijiografia.
 
Mkuu masahihisho; Ni airbus 330 sio airbus 300
airbus 330 ni ndege kubwa ,kams Rwanda watainunua basi pongezi Sana kwa brother Kagame.

Tanzania sijui lini nchi itaambulia angalau kununua kadege kapya japo kamoja
inatia huzuni tunabaki kudhalilishwa na ka nchi kadogo kama Rwanda.
Poa tutachagua wenyewe umaskini au utajiri hapo oktoba 25.

Airbus zote mbili 330, 300 purchased
 
CCM na kukumbatia umasikini kwa wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom