Ruzuku itatuathiri kichama - CHADEMA

Ruzuku itatuathiri kichama - CHADEMA

Hivi kwani kufuata utaratibu kuna shida gani? Nilivyosikia vyama vinatakiwa kwanza kupitisha report zao kwa mkaguzi mkuu wa serikali ambae atapitia akiridhika ata sign na kuweka muhuri wake,kabla ya kupeleka kwa msajiri. Vyama havikupitosha kwa CAG kwa kuogopa kubanwa kimahesabu wenyewe wakakimbilia kupeleka kwa msajiri.VYAMA VYOTE VYA SIASA Acheni ubabaishaji fuateni utaratibu kwani hizo ni KODI ZETU

Umesikia kwa nani ? Are you really a GT?
 
kama ni kweli basi huu ukali wote utakuwa umeratibiwa na ccm kwa ajili ya kuvihujumu vyama vya upinzani vinavyotegemea ruzuku katika kutekeleza shughuli zao za kichama na kimaendeleo ila kwa ccm wao wako imara kwa kuwa na vyanzo vingi vya upatikanaji wa hela..mfano leo karibia viwanja vyote vitaingizia ccm hela kibao
.....
katika sherehe ya ccm mwanza .......5/2/2012 .nanukuu maneno machache ya jk mwenekiti wa ccm alisema kwa.sasa ruzuku haitoshi kwa hio wasikae wakasubiri lazima watafute vyanzo vingine,,,sasa ni vipi zaidi ya viwanja na majengo mengi mijini wamepangisha maduka
 
Kamati ya PAC inatekeleza majukumu yake kisheria. Hii ni taarifa njema kwa wapenda nchi yao.
Nadhani sheria hii ina matatizo na inapaswa kurekebishwa haraka iwezekanavyo!
  1. Kwanza vyama vya siasa havipeleki mipango kazi (Action Plans) yao kwa msajili wa vyama na hivyo siyo rahisi kukagua! Ukaguzi hufanywa kwa kulinganisha na mipango kazi!
  2. Ruzuku inayotolewa kwa vyama vya siasa ni kwa mujibu wa sheria na kulingana na uwakilishi wao katika vyombo vya dola yaani bunge na mabaraza ya madiwani hivyo matumizi ya ruzuku ni kwa kadri vyama vyenyewe viaona inafaa!
Hivyo CAG hawezi kuhoji matumizi ya ruzuku katika vyama kwa kuwa hana pa kulinganisha!
 
Hizo fedha hazina zinatokaje tokaje??

CCM hawana haja ya Ruzuku, kwanza ilitakiwa mali zote za umma walizojimilikisha kabla ya Upinzani zilitakiwa kurudi eidha serikalini kisha kila chama kianze na chake.

Hata hivyo kwa matukio mengi tumeona huwezi kutofautisha chama tawala na serikali, wote ni wamoja. Hivyo mapato ya chama ni sawa na mapato ya serikali au Vs.
 
Hata ccm wataathirika vibaya sana,

ndugu chenyewe ni chama dola,kinaweza kudokoa mafungu serikalini kama vile,[epa] [meremeta] [kagoda] siunajua ikichama tangu nyerere atutoke,kime kaa kimagumashi,
 
Kwani mabilioni ya EPA, Kagoda, Meremeta na juzi juzi mabilioni kuhusiana na ziara ya Obama ambayo inadaiwa "uchunguzi unaendelea" yaliibwaje.

Hizo fedha hazina zinatokaje tokaje??
 
Hivi slaa ataweza kuvumilia hata mwezi mmoja bila mshahara?
 
Back
Top Bottom