Amani kwenu wana JF,
Kwa takribani siku tatu mfululizo kumekuwa na mjadala mzito juu ya swala la ruzuku kwa vyama vya siasa. Mjadala huu ulianza pale Mh. Zitto kama mwenyekiti wa POAC kuhoji uhalali wa kuendelea kupewa ruzuku kwa vyama vya CCM, CDM, NCCR, TLP na CUF among others. Binafsi nilishawishika na kukubaliana na maelezo ya Zitto kwani alijinasibu kuwa anasimamia sheria na taratibu.
Well, nami sikutaka afanye vinginevyo bali kuvibana vyama vya siasa, kikiwemo CHADEMA hasa akiwa kiongozi wa ngazi ya juu kiutawala na kimamlaka, kuweza kutupeleka taarifa za mapato na matumizi kwa CAG! Hata hivyo nilikuwa nikipata tabu sana kuamini kuwa chama changu CDM hakikuandaa taarifa za mapato na matumizi, hasa nikiamini ndicho chama pekee makini kilichobaki Tanzania kinachoenda kupewa dola 2015.
Punde kidogo akaja Anthony Komu (msimamizi wa maswala ya fedha ndani ya chama) nakutoa nyaraka zenye ushahidi juu ya mwenendo na taarifa za ruzuku.
Hili aliliweka sawa na amani ikanirudi nakujua chama changu kipo macho kwani kinajua adui yake (ma-ccm) yatatafuta kila sababu yakumbana ili kuondoa ule uamnifu kwa jamii. Uaminifu unaokua kwa kasi kila uchao. Heko kwa umakini CDM
Leo nimepata nyepesi eti ile kodi ya watanzania (inayoitwa ruzuku) imesitishwa! Nataka nikiondoe hofu CHADEMA. Binafsi nitatoa SEHEMU YA MSHAHARA WANGU KILA MWEZI kuweza kufidia pengo la ruzuku.
Ndugu zangu wapenda maendeleo na mabadiliko kaeni mkitambua na iwaangie akilini kuwa hizi ni mbinu chafu za kukikwamisha CDM.
Mbinu hizi ni mwendelezo wa zile nyingi kukwama. Natambua wengi vimshahara vyetu ni vidogo mno lakini nina hakika endapo tutaamua kwa moyo mmoja basi chama kinauwezo wakupata pesa nyingi zaidi ya hizo za ruzuku.
Waswahili husema 'kamba hukatikia pembamba' na 'kondoo ni mkia'. Viongozi wetu wameshapambana na wanazidi kupambana. Kamba imefikia ukingoni/kwembamba.
Yaani ukombozi ndo unawaidia halafu wanarudishwa nyuma! Nasema hapana hapana hapana nimekataa. Naomba chama kitoe utaratibu maalumu kiweze kupata pesa yangu na wengine wengi walioguswa kila mwisho wa mwezi.
Tuamke na tuwashangaze mafisadi kuwa tumeamua kwa dhati kumkomboa mtanzania kutoka kwa wakoloni weusi ma-ccm.
Naomba kuwasilisha.