Ruzuku itatuathiri kichama - CHADEMA

Ruzuku itatuathiri kichama - CHADEMA

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Katibu wa Baraza la Wadhamini la CHADEMA Anthony Komu amesema usitishwaji wa Ruzuku kwa vyama vya siasa utakiathiri chama hicho kwa kiwango kikubwa.

Kiongozi huyo mwenye mamlaka ya kifedha ndani ya CHADEMA amesema chama hicho kinategemea asilimia 45% ya Ruzuku ya kila mwezi kulipa mishahara ya wafanyakazi na watendaji wa chama kote nchini.

Komu amesema ingawa wana vyanzo vingine vya mapato lakini havitoshi bila kutegemea Ruzuku.

Komu amesema pia usitishwaji huo wa Ruzuku utaathiri kwa kiwango kikubwa mipango ya chama hasa uimarishwaji wake katika operesheni zinazoendekea kote nchini.

Kiongozi huyo amelaani uamuzi wa Kibabe wa Kamati ya bunge kuzuia Ruzuku kwa vyama vyote huku CHADEMA wakiwa hawana kosa lolote na wakiwa wameshakabidhi mahesabu yao ofisi ya msajili wa vyama siku nyingi.

Source:Mwananchi.
 
Kwa maana hio ruzuku tiyari imezuiliwa???
Mbona hakuna taarifa hio katika huo muhtasati?!!
 
Wangeifuta kabisa ili hawa wachumia tumbo, CHADEMA wajifunze adabu!
 
Ni nani anayetakiwa kuthibitisha kauli ya CHADEMA kwamba mahesabu ya CHADEMA yameshakaguliwa na hivyo kustahili kuendelea kupata ruzuku? Hii isije kuwa ni njama ya kuidhoofisha CHADEMA baada ya propaganda chungu nzima za kukidhoofisha CHADEMA kushindwa. Ifahamike wazi kwamba CCM inaweza kutoathirika hata chembe kwa sababu wanaweza kuendelea kuchota pesa chungu nzima toka hazina na kuingizwa katika mfuko wa chama hivyo "shughuli za chama" kuendelea bila athari yoyote.
 
kama wamezuia kweli tujiandae na EPA nyingine maana ccm wataumia vibaya. Kwa chadema tunaweza kuchanga hela na viongozi kujitolea mpaka mgogoro uishe
 
natambua umuhmu wa hyo ruzuku ktk chama chochote lakin ni wakat muafaka sasa vyama hasa hivi vya upinzani kutengeneza vyanzo mbalimbali vya mapato ili upepo wowote utakapopta usiwatetereshe.
 
Ni nani anayetakiwa kuthibitisha kauli ya CHADEMA kwamba mahesabu ya CHADEMA yameshakaguliwa na hivyo kustahili kuendelea kupata ruzuku? Hii isije kuwa ni njama ya kuidhoofisha CHADEMA baada ya propaganda chungu nzima za kukidhoofisha CHADEMA kushindwa. Ifahamike wazi kwamba CCM inaweza kutoathirika hata chembe kwa sababu wanaweza kuendelea kuchota pesa chungu nzima toka hazina na kuingizwa katika mfuko wa chama hivyo "shughuli za chama" kuendelea bila athari yoyote.

Umenifumbua macho mkuu BAK CCM wana uwezo wa kupata pesa kirahisi serikalini.

CC Pasco
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata ccm wataathirika vibaya sana,
...mkuu hii ni movi yao ya kudhoofisha upinzani,so walijianda,wamevuna tembo wote,wanapiga ngada,twiga na mzigo mwingine umewekezwa kwa rostam na wazee wa epa,bila kusahau fixed deposit ya uswizi...
 
Chadema kwanini wanalialia kuhusu kufuatwa kwa utaratibu kwani wao ndo wana makosa?

Wafuate tarabu fedha zisifujwe.

mbona kila kukicha chadema wanapiga kelele kuhusu ukaguzi? Kama wako safi si watulie sheria ifuatwe!
 
Ni nani anayetakiwa kuthibitisha kauli ya CHADEMA kwamba mahesabu ya CHADEMA yameshakaguliwa na hivyo kustahili kuendelea kupata ruzuku?

Hili ndilo ilibidi liwanyime usingizi ila wao wakaitisha vyombo vya habari na kutoa tamko na vielelezo,anyways ngoja tuone umakini wa vyama katika kutatua changamoto!!!!!!

Hongera sana kamati kwa kutingisha mibuyu
 
kama wamezuia kweli tujiandae na EPA nyingine maana ccm wataumia vibaya. Kwa chadema tunaweza kuchanga hela na viongozi kujitolea mpaka mgogoro uishe

Mkuu mamseri binafsi napendekeza viongozi wa Chadema waitishe harambee ya dharura kwa wanachama kote nchini ili operesheni za chama zisisimame.
 
Last edited by a moderator:
majina mengne yanatafsir matendo MSALANI
 
Last edited by a moderator:
Ni nani anayetakiwa kuthibitisha kauli ya CHADEMA kwamba mahesabu ya CHADEMA yameshakaguliwa na hivyo kustahili kuendelea kupata ruzuku? Hii isije kuwa ni njama ya kuidhoofisha CHADEMA baada ya propaganda chungu nzima za kukidhoofisha CHADEMA kushindwa. Ifahamike wazi kwamba CCM inaweza kutoathirika hata chembe kwa sababu wanaweza kuendelea kuchota pesa chungu nzima toka hazina na kuingizwa katika mfuko wa chama hivyo "shughuli za chama" kuendelea bila athari yoyote.

Hizo fedha hazina zinatokaje tokaje??
 
Back
Top Bottom