Ruvu Shooting 1-3 Simba SC | Ligi Kuu | CCM Kirumba

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
NBC imerejea leo, Mechi kubwa Inayotazamiwa ni wenyeji RUVU SHOOTING vs Simba SC.

Baada ya Mapumziko ya wiki kadhaa sasa ngoma inarejea

Tutarajiri Nini Kutoka Kwa Simba? Au Ruvu Shooting wataendelea kuwa Bora?

=====

00' Kabumbu limeanza uwanja wa CCM Kirumba

03' Simba wanapata kona ya kwanza kwenye mchezo, Bernard Morrison anapiga na kutoka

04' Benard Morrison anapewa kadi ya njano baada ya kumfokea mwamuzi kwa madai ya kumnyima penalt

09' Almanusura Simba waandike bao la kwanza lakini mlinda mlango anasimama imara na kuupangusia nje

14' Benard Morrison anawekwa chini nje kidogo ya 18, faul kuelekea Ruvu Shooting

15' Mohammed Makaka anapangua free kick ya Mohammed Hussein Zimbwe

16' Simba wanapata kona ya nne na Morisson anaichonga

17' ⚽ Goooooal, Simba wanaweka bao la kuongoza kona ya Morisson ikizaa matunda na Meddie Kagere kuumalizia kambani

26' Dilunga anapiga off target, Ruvu Shooting 0-1 Simba

31' Cassian Ponela anapewa kadi ya njano, alizidiwa chenga akaamua kumshika Benard Morisson

33' Ruvu wanapata kona baada Manula kuupangulia nje mpira, hata hivyo inakosa matunda

36' ⚽ Simba wanaweka bao la pili, Kibu Dennis anapiga shuti na kupanguliwa na mlinda mlango mpira ukiangukia miguuni kwa Meddie Kagera na kuandika bao la pili

43' ⚽ Kibu Deniss anaiweka Simba bao la tatu, Assist ya kisigino kutoka kwa Meddie Kagere

45+2 Mpira unakwenda mapumziko, Ruvu Shooting Vs Simba uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

70' ⚽Ruvu Shooting wanaandika bao, Ruvu Shooting 1-3 Simba

72' Erasto Nyoni anapanguliwa mkwaju wake wa Penalt iliyotokana na Kibu Deniss kuangushwa ndani ya 18

90' Kibu Deniss anapoteza nafasi akiwa yeye na mlinda mlango.

Mpira umekwisha uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Ruvu Shooting wamekubali kichapo cha 1-3 dhidi ya Simba.

Ruvu Simba.jpeg
 
NBC imerejea leo, Mechi kubwa Inayotazamiwa ni wenyeji RUVU SHOOTING vs Simba SC.

Baada ya Mapumziko ya wiki kadhaa sasa ngoma inarejea

Tutarajiri Nini Kutoka Kwa Simba? Au Ruvu Shooting wataendelea kuwa Bora?
My prediction

Ruvu 0-Simb 0.
 
Maana yake ni kuwa kocha hajaridhika na usajili wa bench la Gomez.
Simba mwaka huu usajili ulikuwa ni wa kitapeli, basi tu watu wabishi.
Hiki kikosi, ingawa mimi Yanga kutakuwa na shughuli leo.
Hiki kikosi kwangu imekuwa kama surprise ,labda kama ana mbinu zake
 
Back
Top Bottom