Rushwa za mahakimu kesi za epa yaanza !!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Wana jf kama tulivyopiga kelele wahusika wa epa wafikishwe sehemu zinaotakiwa kutokana na uhalifu wake ,kumbe tunawapa ajira nyingine kitengo kilekile ambacho tumekuwa tukikiamini na kuwaomba serikali na rais wake watufikishie uko kupata haki yao kwa walichokifanya!!!
Katika gazeti la leo la tanzania daima nimesikitika kuona makarani wakilalamika kwamba mahakimu na pp wanachukua rushwa na kuna ushahidi kwamba hata hao wanaotoka kwa dhamana wengi hawajafkisha masharti yanayotakiwa !!habari zaidi zinasema makarani walienda kwa hakimu mfawidhi mkuu mama euphenia mingi
na kutolewa nje:baada ya hapo wakapelekwa kwa msaidizi wake ambaye akusaidia kitu!!!!jamani mi sijui tena na sema sijui hii nchi
anaijua mungu tu
 
magereza vile vile dili zinaendelea. maana kukaa vip sio haki ya mtuhumiwa. ni uamuzi wa magereza nani akae vip na nani akae holela. na uamuzi wao ni wa mwisho. kwa hiyo mwenye nacho anaweza akalala nyumbani kwake asubuhi anarudishwa kuja kuelekea mahakamani kufuatilia dhamana yake. hata dhamana wanaruhusiwa kufuatlia kila siku (wengine ni siku za mention tu ambazo kwa kawaida ni baada ya wiki mbili mbili).

tuache kulalamika jamani. tumewachagua wenyewe kwa kishindo.

macinkus
 
Imetolewa mara ya mwisho: 16.11.2008 0021 EAT

• Nguvu za EPA TAKUKURU 'kupiga' kambi Kisutu

Na Said Mwishehe
Majira

SIKU moja baada ya baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutumiana kupokea rushwa kutoka kwa ndugu wa watuhumiwa wa wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) , Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ina mpango wa kuweka mtego utakaowanasa wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Habari za ndani kutoka ndani ya TAKUKURU ambazo zimelifikia gazeti hili jana jioni zimeeleza kuwa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa zimeisumbua taasisi hiyo na sasa inajipanga kuweka 'kambi' ili kuwanasa watumishi wanajipatia rushwa kutoka kwa ndugu wa watuhumiwa kwa madai kuwa watawasaidia kupunguza makali ya dhamana.

Hata hivyo chanzo chetu hicho kilisema mpango wa kuweka mtego Kisutu ni wa siri.

"Wewe umeniuliza mmejipanga vipi kudhibiti vitendo vya rushwa vilivyoripoti Kisutu, nimekujibu kuwa tumejipanga sasa unataka nikueleze mipango yetu itafanyikaje! Uliona wapi askari anaanika siri za jeshi lake hadharani?" kilihoji chanzo chetu kwa sharti la jina lake kutochapishwa hadharani.

Hata hivyo chanzo hicho hakikuwa tayari kuliongelea kwa udani suala hilo kwa madai kuwa anayeweza kuzungumzia madai hayo ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dkt. Edward Hosea. Gazeti lili lilipomtafuta Dkt. Hosea, ili atolee ufafanuzi mpango huo simu yake ilikuwa imezimwa.

Jana vyombo vya habari karibu vyote viriripoti taarifa kuwa kuna tuhuma za kuwepo kwa rushwa katika mahakama hiyo ambapo baadhi ya watumishi wa mahakama hiyo wanatuhumiana kupokea rushwa kutoka kwa ndugu wa watuhumiwa wa EPA ili kuwasaidia kupata dhamana.

Mbali ya tuhuma hizo, juzi mahakimu walikaa kikao cha dharura ambacho kiliwahusisha makarani wote kujadili mambo mbalimbali ambayo yamejitokeza tangu watuhumiwa wa EPA waanze kufikishwa mahakamani.

Habari za ndani zilieleza kuwa makarani wa mahakamani hiyo walionywa kutojihusisha na rushwa na kutahadharishwa kuwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Kikao hicho kiliitwa na uongozi wa mahakama hiyo na kuongozwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Bw.Ferdinand Wambali.

Pamoja na mambo mengine mahakimu wanaosikiliza kesi za EPA waliomba kupatiwa ulinzi kwa kuhofia usalama wa maisha yao kwa kuzingatia uzito wa kesi walizopangiwa kuzisikiliza.
 
wana jf kama tulivyopiga kelele wahusika wa epa wafikishwe sehemu zinaotakiwa kutokana na uhalifu wake ,kumbe tunawapa ajira nyingine kitengo kilekile ambacho tumekuwa tukikiamini na kuwaomba serikali na rais wake watufikishie uko kupata haki yao kwa walichokifanya!!!
Katika gazeti la leo la tanzania daima nimesikitika kuona makarani wakilalamika kwamba mahakimu na pp wanachukua rushwa na kuna ushahidi kwamba hata hao wanaotoka kwa dhamana wengi hawajafkisha masharti yanayotakiwa !!habari zaidi zinasema makarani walienda kwa hakimu mfawidhi mkuu mama euphenia mingi
na kutolewa nje:baada ya hapo wakapelekwa kwa msaidizi wake ambaye akusaidia kitu!!!!jamani mi sijui tena na sema sijui hii nchi
anaijua mungu tu

fanya utafiti wa kina na hao makarani wako pamoja huyo mama mingi, maana story unayoitoa hapa na ile magazeti imelenga kitu usichokijua. Nakushauri tu urudi na ukaifanye home work yako vizuri then utauona ukweli wa issue .
 
Sasa kwanini wewe uliyefanya home work juu ya Issue hii usituambie mambo yanakwendaje.

Hongera Mama Mia kwa kuiweka thread hii maana ni changamoto
 
thx mama mia.

Unajua uozo wa idara hiyo ya mahakama huko siku nyingi.Sasa na hao TAKUKURU sijui tutawaaminije? make sasa ushakuwa mchezo wa kuigiza ndani ya shamba la bibi. Usije ukashangaa tukiambiwa kwamba mahakama imeungua na ushaidi wote umepotea mwisho DPP anawambia wananchi " nolle prosequi"

Tunayo safari ndefu ya kusafisha jamii yetu.
 
Wezi hukamatwa wakapelekwa mbele ya sheria na kuhukumiwa kulingana na kipimo cha sheria. Sasa wanasheria wakivunja sheria watapelekwa wapi ikiwa wao ndio hukaa kutoa uamuzi wa madai nk. Hii ni sawa na fumbo moja katika Biblia takatifu ambalo Kristo aliwaambia wanafunzi wake Je, chumvi ikikosa chachu yake itatiwa nini ili ipate tumika tena? Hiyo haifai hutupiliwa mbali ikakanyagwa. Haifai kwa chakula wala chochote.

Sasa I suspect we might be having the real situation in practice in Tanzania with regards and not limited to EPA scandalers.

My mind all the times betray me that sheria mkononi is the most effective and economical means to curb uhalifu. Is my mind betraying me right?
 
Jamani mbona mnashangaa? Kwani hamkujua kuwa EPA ni mchezo wa kuigiza (series) ambao kila mara wahusika wapya wanaingia na wegine wanatoka? Hakuna jipya hapa, wala jambo ambalo halikutegemewa.

Hata hivyo, jueni kuwa Mahakimu wa mwisho ni wananchi ambao wana jukumu ya kutatua tatizo hili wakati wowote wakiamua au kusubiri hadi 2010. Baada ya hapo tunaweza kupata wapiganaji wa kumalizia hii kazi na nyingine nyingi ambazo mafaili yake yako likizo (Richmond, IPTL, Buzwagi n.k).
 
Wana jf kama tulivyopiga kelele wahusika wa epa wafikishwe sehemu zinaotakiwa kutokana na uhalifu wake ,kumbe tunawapa ajira nyingine kitengo kilekile ambacho tumekuwa tukikiamini na kuwaomba serikali na rais wake watufikishie uko kupata haki yao kwa walichokifanya!!!
Katika gazeti la leo la tanzania daima nimesikitika kuona makarani wakilalamika kwamba mahakimu na pp wanachukua rushwa na kuna ushahidi kwamba hata hao wanaotoka kwa dhamana wengi hawajafkisha masharti yanayotakiwa !!habari zaidi zinasema makarani walienda kwa hakimu mfawidhi mkuu mama euphenia mingi
na kutolewa nje:baada ya hapo wakapelekwa kwa msaidizi wake ambaye akusaidia kitu!!!!jamani mi sijui tena na sema sijui hii nchi
anaijua mungu tu
Mama pole sana. Hii ndiyo hali halisi ya nchi hhi tunayoishi. Nilisikia wanataka ulinzi maalumu. Sasa napata mwanga ni kwa nini walitaka ulinzi huo! SASA WANA HELA NA WANATAKA VIBAKA WASIWASOGELEE, MAANA KUPELEKA BENKI HAWATHUBUTU WATAJULIKANA!
 
Back
Top Bottom