Hivi kesi za EPA zimeishia wapi jamani?kwa mtindo huu Watanzania tutafikaje?

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Kuna wakati nimesikia bungeni swali likiulizwa kwa mwanasheria mkuu endapo kuna kesi zozote pending kwa DPP na jibu lililotoka likawa ni kwamba kesi zipo na zitawekwa wazi karibuni.Mimi sikutilia maanani jibu hilo kwani nimetafakari mambo yafuatayo na kuona kuwa Watanzania bado tuna safari ndefu sana ya kusafisha maovu yanayotufanya tuwe hapa tulipo(namaanisha ufisadi uliokithiri).Tafakari yangu inahusisha yafuatayo katika swala zima la kupambana na ufisadi ktk nchi hii:

1.Hivi watanzania tueleweje sheria za nchi zinavyofanya kazi?,je zile kesi kadhaa za EPA zilizofunguliwa kwa kishindo zimefikia wapi jamani,mbona hatusikii kesi zikiendelea na watu kuchukuliwa hatua?,wako wapi kina Jeetu Patel,Rajabu Maranda na wengine walioshikwa EPA na kufunguliwa mashtaka?(kwa maana walirudisha hela).

2.Kama hawa wameshtakiwa mbona kesi hizi haziishi?kama watu wameshikwa ushahidi upo mbona kesi hizi haziishi jamani?hivi nchi hii inaendeshwa kwa sheria gani?mbona majaji/mahakimu wapo?

3.Mbona wale waliohusika na mauaji ya albino kesi zao ziliisha?(au kwa vile jumuiya ya kimataifa ilipiga kelele?)

4.Mbona mtaani kesi za hela ndogondogo zinaendeshwa haraka?yupi mwenye kosa kubwa,anaefilisi nchi au anaeiba kuku?,yupi wa kushughulikia haraka kwa logic ndogo?

5.Tutawezaje kupambana na rushwa/ufisadi kama wale wanaoshikwa hawachukuliwi hatua?

6.Nchi hii ya ajabu sana, watu wamepiga kelele saana ndipo baadhi ya ufisadi ukagundulika,baadae watu wamepiga kelele saana watu washikwe,wakashikwashikwa(na wale waliorudisha fedha eti wakaachiwa),baada ya hapo watu wamesahau hatima ya kesi hata za wale walioshikwa mh!hii nchi ya ajabu saana.Kinachofanyika ni tukio moja kuja na kufunika lililopita.Mfano, juzi juzi kelele zilipigwa serikali ikatingishika,then pakaja babu wa loliondo akafunika zile kelele,sasa pamekuja issue ya katiba mpya itafunika story zote zilizopita(ikichangiwa na haya mambo ya ccm kujivua gamba dodoma),baadae pataibuka tena issue itafunika haya yoote yaliyopita.

Huu ndio utaratibu wa Mtanzania kushughulikia shida zake.Tunapiga kelele kuondoa uovu lakini hatuhakikishi uivu umeondoka na serikali hii inajua jinsi ya kushughulika na raia wake kweli kweli kwa mtindo huu.Angalieni wenzetu kenya jamaa sasa wako the Hague wanapata kiti moto(bila kuangalia huyu mkubwa au nani),mbele ya sheria jamani watu wote sawa.Zimepigwa kelele za richmond watu hawachukuliwi hatua hata wale watendaji waliohusika moja kwa moja technically wako maofisini wanakula shushu kwani mambo yameshasahaulika(hizi zote zimebaki historia tu na watu watastaafu poa na kuondoka na mafao ya PSPF sijui nssf n.k),ndivyo tulivyo wabongo(sijui nani alitupa jina la wabongo maana naona halitufai maana bongo hamna)

7.Kuna jamaa waliohusika na EPA(kumbukeni EPA ililiza wabunge wote bungeni,mnakumbuka?),hawa waliorejesha fedha wakazibwaga kwenye mabenki na kutimka vipi hawakuchukuliwa hatua?hivi wewe leo unakutana na mwizi wako akiwa anaendesha gari aliyokuibia alafu unamwangalia unamwacha?hivi hii ina ingia akilini kweli?au jamaa umemfumania anatembea na mkeo hivi kweli unamwangalia tu!,nakumbuka issue ya EPA ilichangiwa kwa kilio na wabunge wote wa vyama vyote kwa msimamo mmoja mnakumbuka?(au mmesahaulishwa na matukio kama kawaida yetu?),alafu eti jamaa wengine wameshikwa alafu watu wala hawahoji hatima yao?hivi hii nchi mtu yoyote naona anaweza kuwa raisi hapa tz,maana huitaji kufikiri sana,bora ujue psycology tu ya wa tz.

8.Nahitimisha kwa kusema tu kwamba,hata tufanyeje nchi hii,kama mfumo wetu wa sheria hautashughulikia uhalifu kikamilifu,hapatakuwa na chochote cha maana kuhusu maendeleo ya nchi hii,hata tuwe na nini,mtataka mumfikishe mwizi wa kura zenu mahakamani hamshindi(rejeeni kesi za uchaguzi zilizo mahakamani),mtataka mumfikishe mahakamani mwizi wa raslimali za nchi mnazozipigania usiku kucha hamtashinda kesi, n.k n.k n.k

9.Mtabaki kuwaona mafisadi wakiendesha magari makubwa,wakijenga nyumba na kumiliki mali tele,wakishiriki siasa na kupata madaraka watakavyo na ndivyo nchi hii itakavyokuwa mpaka pale hatua za dhati za haki ya sheria zitakapofanya kazi yake.Bila hivyo itakuwa ni mtindo wa kumwaga maji kwenye gunia,yaani mnapambana kukusanya mapato ya nchi na huku upande mwingine kiasi kikubwa cha mapato hayo kinaishia kwenye matumbo ya wachache.Lazima kuwe na zero tolerance kwenye issue za matumizi mabaya ya madaraka,wizi,rushwa,ufisadi na aina yoyote ya ubadhirifu wa mali ya umma ndio nchi hii itaona mabadiliko kwenye jamii yake popote pale nchini.Igeni mifano ya nchi za wenzetu walioendelea,wao hawachezi na matapeli...........................
 
Hiyo kesi ndo imeisha juu kwa ju...that why we are called 3rd world country..rushwa, ubadhilifu..uggh! afrika sijui...
 
CCM waliishasafishana toka wakati wakampeni mwaka jana. Majalada yote ya wizi yaliishachomwa moto. Kumbuka marais wa nchi walituhumiw kwenye wizi huo na wizi mwingine. Sasa mwizi ajifunge? Unakumbuka wikileaks na Hosea!
 
Kila mara huwa nasema sisi huwa hatuna ajenda tunaendeshwa na magazeti na upepo, hatujawahi simamia ajenda mpaka mwisho tunaanzisha ajenda nyingi nakuziacha pending
 
Nashangaa watu kushabikia ccm kujitoa gamba wakati ukiangalia kwa makini zi utagundua viongozi waliochaguliwa wanatoka kwenye pull hiyo hiyo na tena wengi wao ni wale viongozi wa "YES MZEE" yaani si watu wa maamuzi,kwa kifupi they are weak leaders(hawa si watu wa mageuzi ya aina yoyote bali wakutegemea vyeo na fadhila za mkuu wao).
 
Back
Top Bottom