Rushwa ya Ngono kikwazo Wanawake kushiriki Ununuzi wa Umma (Public Procurement)

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Hayo yamo katika ripoti ya utafiti wa ushiriki wa wanawake katika ununuzi wa umma uliofanywa na Kituo cha Africa Freedom of Information Centre (AFIC) katika nchi tano za Kenya, Uganda, Ethiopia, Rwanda na Tanzania.

Akiwakilisha matokeo ya utafiti huo kwa waandishi wa habari jana jijini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa AFIC, Gilbert Sendugwa alisema hali hiyo pia inachangiwa na uelewa mdogo, lugha ngumu na ya kitaalamu inayotumika katika mikataba ya ununuzi wa umma, sera ngumu na mfumo dume unawanyima fursa wanawake kushiriki katika sekta hiyo muhimu.

Alisema utafiti huo umebaini wanawake wengi hawana taarifa, wala hawajui namna ya kuomba zabuni mbalimbali za ununuzi wa umma.

“Takribani asilimia 60 ya ununuzi wa nchi unatumika katika sekta ya ununuzi wa umma, hivyo ni jambo la kizalendo kuhakikisha nchi inaweka mazingira na sera nzuri ya kuhakikisha wanawake wananufaika na matunda ya ukuaji wa uchumi wa nchi yao,” alisema.

Aliongeza kuwa utafiti unaonyesha asilimia 48 ya biashara zote nchini zinamilikiwa na wanawake, lakini jambo la kusikitisha ni namna ambavyo wanawake hao wametengwa katika fursa za kunufaika na kandarasi mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya ununuzi wa umma.

“Kwa mfano, Sheria ya Ununuzi wa Umma inaelekeza kwamba ili kupata nafasi ya kuhudumia mkataba wa ununuzi wa umma, walengwa lazima wawe katika kikundi na siyo mtu binafsi, hatua hii inawanyima haki ya msingi wanawake wenye kampuni yao binafsi kunufaika,” alisema.

Mratibu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa AFIC, Charity Komujjurizi, alisema kuna umuhimu wa wizara husika kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya ununuzi wa umma katika kuwaelimisha wanawake namna bora ya kuomba na kunufaika na fursa mbalimbali zinazojitokeza katika ununuzi wa umma nchini.

“Kwa mfano, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) huwa wanatoa tenda za ununuzi wa umma katika huduma muhimu, hivyo ni muhimu wawe wanatoa kipaumbele kwa wanawake wajasiriamali katika maeneo husika,” alishauri.

Akipokea matokeo ya utafiti huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Maendeleo ya Jamii, Fatma Toufiq, alipongeza AFIC kwa kufanya utafiti huo muhimu. Kamati itaishauri serikali kuyafanyia kazi mapendekezo mbalimbali yaliyoainishwa katika ripoti hiyo.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom