Rushwa Wodi za Uzazi katika baadhi ya Hospitali za Serikali zinahatarisha usalama wa mama na mtoto

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Wanawake wengi wanaoenda kujifungulia katika Hospitali za serikali wamekuwa wakilalamika juu ya kuombwa rushwa na manesi wakati wa kujifungua ili wapate huduma nzuri.

Wamama wengi ambao walikwisha kupata huduma ya kujifungua katika Hospitali za serikali au vituo vya afya wamesema kuwa ili upate huduma nzuri wakati wa kujifungua kutoka kwa manesi inatakiwa umpe nesi angalau elfu kumi, hata elfu tano pia hupokea.

Wengi wamehatarisha maisha na hata kupoteza maisha ya ya watoto wao wakiwa chumba cha kujifungulia kutokana na kushindwa kutoa rushwa,.

Baadhi ya hospitali ambazo zimekuwa zikilalamikiwa sana kwa kuomba rushwa kwa wamama wanaoenda kujifungua ni Hospital ya Ngarenaro,na levolosi zilizopo jijini Arusha. Na wamama wengi waliokwisha pata huduma ya kujifungulia hapo wamelalamika kuombwa rushwa na manesi wakati wa kujifungua.
 
Wanawake wengi wanaoenda kujifungulia katika Hospitali za serikali wamekuwa wakilalamika juu ya kuombwa rushwa na manesi wakati wa kujifungua ili wapate huduma nzuri.

Wamama wengi ambao walikwisha kupata huduma ya kujifungua katika Hospitali za serikali au vituo vya afya wamesema kuwa ili upate huduma nzuri wakati wa kujifungua kutoka kwa manesi inatakiwa umpe nesi angalau elfu kumi, hata elfu tano pia hupokea.

Wengi wamehatarisha maisha na hata kupoteza maisha ya ya watoto wao wakiwa chumba cha kujifungulia kutokana na kushindwa kutoa rushwa,.

Baadhi ya hospitali ambazo zimekuwa zikilalamikiwa sana kwa kuomba rushwa kwa wamama wanaoenda kujifungua ni Hospital ya Ngarenaro, na levolosi zilizopo jijini Arusha. Na wamama wengi waliokwisha pata huduma ya kujifungulia hapo wamelalamika kuombwa rushwa na manesi wakati wa kujifungua.
Mkuu matatizo ya wanawake kuanzia wanapokuwa na mimba mpaka kujifungua ni makubwa sana. Kinachonishangaza nchi hii tuna kitu kinachoitwa viti maalum kwenye bunge. Hivi ni viti maalum kwa ajili ya wanawake lakini wakishafika huko husahau kabisa masaibu yanayowakuta wanawake wenzao. Husikii hata siku moja wakipigia kelele mambo kama haya. BTW miaka ya nyuma hospital ya Mawenzi pale mjini Moshi chumba cha labour kulikuwa na manesi wenye pliers ya kufinya wanawake wanaoleta ''udekakaji'' wakati wa kujifungua. Mwanamke ambaye hajawashikisha chochote halafu akiambiwa panua sukuma akileta za kuleta walikuwa wanamfinya na pliers. Ni zamani miaka ya 2005 hivi....
Radon_Kombizange_20062266_1_800x800.jpg
 
Back
Top Bottom