Rushwa kwa Matrafiki yapata mbinu mpya

asaprichie

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
292
227
Habari ya saizi Wakuu,

Leo nimeshuhudia njia mpya ya upokeaji rushwa kwa Trafki maeneo ya pale Goldstar ambapo ujenzi wa SGR unaendelea.

Wakati nimefika pale kituoni asubuhi ya saa 1 nikiwa nasubiri daladala za kwenda Gongo la Mboto nilikuta kituo kina raia mmoja tu ambae nae anaonekana sio mtu ambae anasubiri gari. Upande wa pili (kama mita 3 hivi) kulikuwa na trafiki anaongoza magari.

Sasa katika muda niliokaa pale nikawa nashangaa huyu jamaa ambae nimemkuta kituoni anapokea hela kwa kila daladala inayopita, yaani daladala zote zinazotokea Mnazi Mmoja lazima zipitie kituoni hapo halafu wanampa hela huyo jamaa kwa njia fulani hivi ya kisiri siri then daladala linaondoka.

Nikasema ebu ngoja nitulie kidogo nione kwanini wanampa hela. Baada ya muda nikaona anapokea simu, katika kuchunguza nikagundua kuwa alikuwa anaongea na Trafiki yule ambae yuko upande wa pili (nahisi hapa kuna ishara alimpa) maana gari iliyofuata haikutoa hela nikagundua kuwa trafiki yule anakula rushwa lakini mpokeaji ni huyo kijana aliyekuwa kituoni

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tupatie na kapicha kudhibitisha hilo. Pia siwezi kuamini maneno yako yani kwa Jiji la Dsm kituoni mlikuwepo wawili tuu, !? Kwa maana nyingine kama huyo kijana asingelikuwepo hapo ina maana wewe ndo ulikuako kituoni peke yako kitu ambacho mimi nita tafsiri kama wewe bila shaka wewe ni mwanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_2890.JPG

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndo unajua leo

hata vijiwe vya taxi..anapewa dereva watajuana na afisa baadae

waacheni wanywe hata maji jua kali sana saivi

Hii style Ndo nimeona leo mzee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tupatie na kapicha kudhibitisha hilo. Pia siwezi kuamini maneno yako yani kwa Jiji la Dsm kituoni mlikuwepo wawili tuu, !? Kwa maana nyingine kama huyo kijana asingelikuwepo hapo ina maana wewe ndo ulikuako kituoni peke yako kitu ambacho mimi nita tafsiri kama wewe bila shaka wewe ni mwanga.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na Asante kwa Maoni yako Mkuu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
nishamatwa sana bahi, ukitembea na 49 unaambiwa 59 yaan ktk kibao cha 50 tembea na 30 wakat huo unaenda Goma sasa hiyo 30 ktk kila kibao cha 50 utafika lini? hawa jamaa nawachukia sana sasa kuna siku wamenisimamisha niko na 30 nikasema leo wananitafta shar lakini bahat wakawa wanaomba lifti. nikawabeba waliikuwa wanarudi dodoma mm kama kawaida nikaanza kutembea na 30 wamevumilia ule mwendo mwisho kile kidada kikasema hii gari mbovu? nikamwambia nzima, wakasema sasa mbona hutembei nikamwambia kuna tochi mbele akasema we tembea na mia nikamwambia njoo uendeshe wewe nikamsindikiza na tusi..alaf ndio nikamtolea vikaratasi vi nne ambavyo vyote ni yeye ndio aliniandikia fine nikamwambia kama kuna mtu nataman atangulie mapema kufariki ktk dunia hii ni yeye na kisha nikasimamisha chuma nikamshusha, yaan nilimwambia tu kirafiki naomba ushuke na usije kuizoea hii gari
 
nimecheka kwa sauti we noma na nusu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom