Licha ya kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari Rais Mhe. John Magufuli kuwa katika mstari wa mbele kupiga vita rushwa, lakini katika hali ya kusikitisha vitendo vya rushwa vimekithiri Baraza la Ardhi na Nyumba Arusha.
Wengi wa wanaohitaji huduma kutoka kwa waheshimiwa Wenyeviti na Makarani wa baraza hilo wamekumbana na matatizo ya kuwekwa katika mazingira ya kulazimishwa kutoa rushwa ili kupata huduma wanayohitaji kutoka kwa serikali yao. Watendaji wa baraza hili wameweka mbele rushwa kama vile hawalipwi mishahara.
Hali ya kutakwa kutoa rushwa iko wazi kiasi kwamba TAKUKURU ikitaka kuwakamata haitachukua uchunguzi wa kina.
Serikali ya awamu ya Tano inafanya kazi nzuri, lakini kuna baadhi ya watendaji wachache kama hawa wa Baraza la Ardhi na Nyumba Arusha wanaotia doa kazi nzuri anayofanya Mheshimiwa Rais John Magufuli na serikali yake.
Vyombo vinavyohusika vinaombwa kufuatilia na kufyekelea mbali wote (kwa sasa majina yamehifadhiwa kwa muda) wanaotia doa kazi nzuri ya Mhe Rais magufuli na Serikali ya awamu ya tano.