Rushwa hizi za wabunge wa CCM zinaharibu alama ya Dkt. Magufuli

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, Kuna ongezeko kubwa la wabunge wa ccm kuhonga na kutoa rushwa mbalimbali ikiwemo Fedha na Magari kwa wajumbe na wana chama Katika ngazi za jimbo

Hili jambo linatia doa chama cha Mapinduzi na limeanza kutudhalilisha sana kuelekea October 2020, Hawa watu wanaturudisha miaka mitano nyumba yaani kabla ya October 2015 ambapo ccm na rushwa ilikuwa kama mkono na kiganja

Dr Magufuli amajitahidi kusafisha lakini kumbe kuna watu rushwa ipo moyoni mwao, Hawawezi kutoa sera bila hongo na rushwa kuelekea uchaguzi 2020

Kuelekea uchaguzi mkuu October 2020 ni dhahiri sasa ndani ya CCM rushwa inatembea bila aibu

Wafuatao wabunge wastaafu wanaogombea tena wanahojiwa na takukuru na kuna wengi watu Wanalalamika

Mheshimiwa Lusinde wa mtera au maarufu kibajaji

Mheshimiwa David Mathayo

Mheshimiwa Serukamba

Hawa niliowataja kama ccm itawapitisha kugombea kwenye majimbo yao ubunge tena, Tutakuwa wanafiki ndani ya chama

Yafuatayo yafanyike kunusuru chama cha Mapinduzi

Hawa watu wakatwe mapema, Hakuna haja ya kuwajadili

Hawa watu watangazwe kama adui namba moja wa chama cha Mapinduzi

Hawa watu wafutwe kabisa uanachama kuonyesha uwajibikaji

Katibu wa itikadi na uenezi umekuwa ukipiga kelele sana majukwaani kuhusu rushwa mbona huwaongelei hawa watu wanaochafua chama kwa sasa?

Wanabodi huu uzi utumike kuweka ushahidi na majina husika kwa wabunge au watia nia ya ubunge ili chama kichukue hatua bila kuwa na ndimi mbili
 
CCM bila rushwa huwezi toboa kamwe!! Kila mtia nia anatoa rushwa kwa style yake. Na mwaka huu wanauhakika akisha pitishwa tu na chama uhakika wa kushinda ni 90% kwani wanajua walichofanya kwenye Demokrasia ya kuchagua. Na watauana kweli wewe subilia tu, majina ya watakao pita yatangazwe, na huenda ikawa nafuu sasa kwa wapinzani.
 
hizo rushwa zilikuwepo enzi zote ila kwa kuwa kuna uthubutu wa kupambana na rushwa ndo maana saa hizi zimeonekana wazi wazi, kipindi kilichopita zilikuwa zaid ya hapo.
 
Yy ndo KINARA WA RUSHWA aliwapa rushwa wajumbe wamfukuze membe ambaye alionekana threat na angechukua form. Kimsingi kwa jinsi wanaccm wasivompenda sirini huku wakimsifia kinafiki hadharani kwa ajili tu ya vyeo basi ilikua bayana magufuli ccm wangempiga chini yani.....
 
Mkuu, kumbuka lakini hao wote ni sehemu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, kwa hiyo ndio wapiga kura wenywew ndani ya mkutano huu muhimu ili kupitisha jina la mpeperusha bendera wa nafasi ya uraisi. Kwa hiyo ltalazimika kuwaonya tu kwa mdomo ili mambo yaishe.
 
Takukuru wamepewa meno na Mh Rais kudili na watoa rushwa, mazoea ya chama kuhonga hela ili wapite ndo mwisho wao, Polepole juz kawaambia wanaotoa rushwa wasije kutegemea watapita! Hvo ni moja ya mkakati wa chama kuhakikisha wanasifisha tamaduni chafu.
 
Mh.Rais tunaomba majina ya watakao thibitika kutoa rushwa yakatwe, tafadhali.
 
Mulianza kutoa rushwa ya kupitishwa bila kura kwa mlioowanunua, leo mnalalamikia kitu mlichokikuza wenyewe! Hata kitendo cha kumfukuza Membe huwezi kukitenganisha na rushwa. Maccm mnanyukana tu kwa rushwa huko majimboni na bado!
 
kwa akili zenu za kishamba mnadhani kuwa Kama serikali inapenda na ibariki hiyo rushwa hao watia nia wangekamatwa? Serikali haitaki huo upuuzi ndo maana inatuma vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuwakamata hao wapumbavu wote watoa rushwa,uwezo wa kuwaachia waendelee kutoa rushwa serikali inao ila haipendi, mnadhani hao TAKUKURU wanatumwa na CHADEMA kuwakamata hao watoa rushwa?
 
Takukuru wamepewa meno na Mh Rais kudili na watoa rushwa, mazoea ya chama kuhonga hela ili wapite ndo mwisho wao, Polepole juz kawaambia wanaotoa rushwa wasije kutegemea watapita! Hvo ni moja ya mkakati wa chama kuhakikisha wanasifisha tamaduni chafu.
Mkuu, kwani biashara ya Polepole ya kutafuta ushawishi kwa waungaji juhudi mkono kutoka vyama vya upinzani ina tofauti gani na hii ya hawa wengine?
 
Wanabodi, Kuna ongezeko kubwa la wabunge wa ccm kuhonga na kutoa rushwa mbalimbali ikiwemo Fedha na Magari kwa wajumbe na wana chama Katika ngazi za jimbo

Hili jambo linatia doa chama cha Mapinduzi na limeanza kutudhalilisha sana kuelekea October 2020, Hawa watu wanaturudisha miaka mitano nyumba yaani kabla ya October 2015 ambapo ccm na rushwa ilikuwa kama mkono na kiganja

Dr Magufuli amajitahidi kusafisha lakini kumbe kuna watu rushwa ipo moyoni mwao, Hawawezi kutoa sera bila hongo na rushwa kuelekea uchaguzi 2020

Kuelekea uchaguzi mkuu October 2020 ni dhahiri sasa ndani ya CCM rushwa inatembea bila aibu

Wafuatao wabunge wastaafu wanaogombea tena wanahojiwa na takukuru na kuna wengi watu Wanalalamika

Mheshimiwa Lusinde wa mtera au maarufu kibajaji

Mheshimiwa David Mathayo

Mheshimiwa Serukamba

Hawa niliowataja kama ccm itawapitisha kugombea kwenye majimbo yao ubunge tena, Tutakuwa wanafiki ndani ya chama

Yafuatayo yafanyike kunusuru chama cha Mapinduzi

Hawa watu wakatwe mapema, Hakuna haja ya kuwajadili

Hawa watu watangazwe kama adui namba moja wa chama cha Mapinduzi

Hawa watu wafutwe kabisa uanachama kuonyesha uwajibikaji

Katibu wa itikadi na uenezi umekuwa ukipiga kelele sana majukwaani kuhusu rushwa mbona huwaongelei hawa watu wanaochafua chama kwa sasa?

Wanabodi huu uzi utumike kuweka ushahidi na majina husika kwa wabunge au watia nia ya ubunge ili chama kichukue hatua bila kuwa na ndimi mbili
Msidanganyike, hii ni danganya toto ionekane CCM "wameshughulikiwa" kumbe hamna lolote.
 
Ikiwa hao wabunge tena wengine wapo zaidi ya vipindi viwili wanaamini katika rushwa,ni ishara gani kwa CCM.
Tena hao waliobambwa ni wale wasafi kidogo,wale waliohitimu katika rushwa hawatakamatwa .
Linabakia swali la msingi kama CCM inaweza ikajitenga na rushwa?Kama haiwezekani je nani wa kuipeleka REHABILITATION CLINIC?
 
Kwa haya mambo ya wabunge kuhusishwa na rushwa ama TAKUKURU, tusisahau "only two key words" ambazo "codes" zake ni ngumu kuzifungua kwa sasa. Zipo kwenye andiko la mti wa "mkomamanga" ama kulambwa kwa "nyongo" iliyotoka mwilini.
 
ile ndio CCM halisi,wabunge CCM wanajua kama kina Sillinde walipewa rushwa. sasa kwa nini wajibane
 
Back
Top Bottom