Rushwa Fixed Account: Msajili na Gavana wanatuona watanzania hatuelewi chochote

Kuna minutes za Board zinazoeleza kwanini walifungua FD, zinasemaje? Hela ya serikali na haswa taasisi kubwa kama TRA sio rahisi kuliwa kirahisi hivyo. Siamini kama BoD ilifanya uamuzi kwa kukurupuka, na hili la ku centralize karibu kila kitu ndani ya muda mfupi sidhani kama litakuwa na matokeo chanya badala ya kuboresha mifumo ya kusimamia uwajibikaji haswa sera na taratibu zetu. Muda utanena!
 
Jambo moja sana shaka nalo hata kama sisi ni mafisadi namna gani-- na jambo lenyewe ni accounting procedures!

TRA ina vitabu vyake ambavyo no matter what; pesa inapotoka LAZIMA ionekane kwenye vitabu with detailed information kwamba inatoka!

Na kama imetoka for FD, si tu kwamba kule bank unapewa receipt bali pia printout among other things for auditing purposes for both mteja/TRA and the bank! Huyu mteja/TRA nae atachukua docs zote hizi for office filing and future auditing/authentication. FD iki-mature na TRA kuchukua pesa yao; again si tu kwamba watatoka na WDL slip bali pia Printout, again, among other things, also for auditing purposes for both bank and mteja!

Hebu nisaidie wewe... hivi pesa kama hiyo unaiba iba vp?! Remember, pesa ilipotoka kwa mara ya kwanza with supported docs kwamba imewekwa FD; tayari itafahamika interest rate ni % ngapi na TRA wanapoenda kuchukua pesa; lazima vitabu vyao vioneshe figure ya Interest Income from Fixed Deposit! Unaiba iba vp hiyo pesa?! Na mbaya zaidi; sio single hand decision.... hebu tujuze! Anyway, sio kwamba haiibiki kabisa but only if for amateur forgery ambayo inaweza kuwa detected hata na First Year student wa accounting!

Akikujibu naomba unitag.
 
Mimi nilishawahi kuuliza humu, Hivi unapoweka Fedha za wananchi kwenye fixed Deposit Account huwa unatarajia nini? yaani Lengo la TRA ni nini?

Ni kwamba, yawezekana walipopewa hizo pesa hawakuwa na shida nazo kwa wakati huo, ndo maana wakaamua waziweke huko, sasa kama hawakuwa na shida nazo kwa wakati huo kwa nini wasiseme kuwa jamani sisi kwa sasa hatuna shida ya haraka na hizi pesa hivo wapewe wengine sisi tukihitaji kwa ajili ya mradi Fulani basi mtatupatia...sasa utakuta, Kwa mwezi huu, SERIKALI imepanga kuwa, itawalipa, TRA, MKANDARASI X, MALIPO YA NDEGE, na wakati huo huo kwenye mgao huo Wizara ya AFYA ikaambiwa wewe tutakupa mwezi huo mgao wako, sasa kama huyu TRA alikuwa hazihitaji hizo pesa, kwa nini asingemwambia Rais kuwa, Mh, Kwa mwezi huu hatutazitumia pesa hizo, tutazihitaji mwezi wa kwanza, hivyo Rais angeelekeza hizo pesa apewe wizara ya Afya...!!!!!!!!!
 
Hahaha....Kinachofanyika ni kupunguza rate ya interest ya fixed deposit....mfano fixed deposit ya kawaida ni 15% lakini inafanywa 4%...na hili linafanyika kabla ya kudeposit pesa na document zote zinaonyesha fixed deposit ya account husika ni 4% baada ya hawa mabosi wa mashirika kukubaliana na mabosi wa mabenki...ili different 11% iliyobaki wanaipiga....na hii pesa inatolewa kupitia bank operational costs au mikopo hewa na inatolewa cash haipitii kwenye account.....hata waje ma auditors kutoka mbinguni hawawezi kuuona huu wizi sababu document zote zitakuwa zinaonyesha interest rate ni 4% wakati kiuhalisia ilitakiwa iwe 15%.....ndicho kinachofanyika hicho msitufanye hatuna akili hata mimi nimeshawahi kufanya kazi benki naujua mchezo wote

Kuna njia nyingi sana ya kucheza safely tena kutumia hizo hizo accounting processes . Hata hao vibosile wanajua . . . . Ila labda wanahofu ya ku reveal truth kwani kama hiyo imefanyika kwa muda mrefu kuna kuhusika kama hawaku act upon
 
Hahaha....Kinachofanyika ni kupunguza rate ya interest ya fixed deposit....mfano fixed deposit ya kawaida ni 15% lakini inafanywa 4%...na hili linafanyika kabla ya kudeposit pesa na document zote zinaonyesha fixed deposit ya account husika ni 4% baada ya hawa mabosi wa mashirika kukubaliana na mabosi wa mabenki...ili different 11% iliyobaki wanaipiga....na hii pesa inatolewa kupitia bank operational costs au mikopo hewa na inatolewa cash haipitii kwenye account.....hata waje ma auditors kutoka mbinguni hawawezi kuuona huu wizi sababu document zote zitakuwa zinaonyesha interest rate ni 4% wakati kiuhalisia ilitakiwa iwe 15%.....ndicho kinachofanyika hicho msitufanye hatuna akili hata mimi nimeshawahi kufanya kazi benki naujua mchezo wote
Watanzania wanachonifurahisha huwa mtu mmoja ana taaluma zaidi ya kumi na huwaga tunajua kila kitu! "uonekane hujui uwe falaaa"!

kwa uelewa wako uliotukuka FD interest ni 15% kwa miezi mitatu? kunahaja gani ya kufanya biashara kama ni hivyoo! Ni afadhali kama hujui ukae Kimya!
 
Sijaelewa mada yako. Hebu tuambie proceedures za kutoa fedha za serikali bank (withdrawing)

Hebu jiulize faida au interest itokanayo na kudeposit FDR inawekwa kwenye account gani au ya nani baada ya FDR kumature?

Pia jiulize bank inapata faida kubwa kivipi ndani ya miezi walau 3 inaweza kumlipa depositor na yenyewe kubakia na fedha?

Kazi ya centralbank ni zipi?

Ukijua mlolongo wote huo utaona Ndulu yupo sahihi
unamaanisha kilankitu lazima kiandikwe kwenye makaratasi,aliyekwambia 10%huwa zinaandikwa ni nani, official contract ni 8% lkn mkakubaliana kuwa nitakupa,6% per utajuaje we we???
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Jambo moja sana shaka nalo hata kama sisi ni mafisadi namna gani-- na jambo lenyewe ni accounting procedures!

TRA ina vitabu vyake ambavyo no matter what; pesa inapotoka LAZIMA ionekane kwenye vitabu with detailed information kwamba inatoka!

Na kama imetoka for FD, si tu kwamba kule bank unapewa receipt bali pia printout among other things for auditing purposes for both mteja/TRA and the bank! Huyu mteja/TRA nae atachukua docs zote hizi for office filing and future auditing/authentication. FD iki-mature na TRA kuchukua pesa yao; again si tu kwamba watatoka na WDL slip bali pia Printout, again, among other things, also for auditing purposes for both bank and mteja!

Hebu nisaidie wewe... hivi pesa kama hiyo unaiba iba vp?! Remember, pesa ilipotoka kwa mara ya kwanza with supported docs kwamba imewekwa FD; tayari itafahamika interest rate ni % ngapi na TRA wanapoenda kuchukua pesa; lazima vitabu vyao vioneshe figure ya Interest Income from Fixed Deposit! Unaiba iba vp hiyo pesa?! Na mbaya zaidi; sio single hand decision.... hebu tujuze! Anyway, sio kwamba haiibiki kabisa but only if for amateur forgery ambayo inaweza kuwa detected hata na First Year student wa accounting!
kwani mkombozi na escrow hela zilitokae ,wanaosimamia utoaji was hela ndio haohao wapiga dili sasa,dhana ya wanatoaje and procedure 2wewe itakusaidia nini, mbona hizo procurement procedure ,ndio kila siku zilalamikiwa kwa rushwa mkuu
 
Watanzania wanachonifurahisha huwa mtu mmoja ana taaluma zaidi ya kumi na huwaga tunajua kila kitu! "uonekane hujui uwe falaaa"!

kwa uelewa wako uliotukuka FD interest ni 15% kwa miezi mitatu? kunahaja gani ya kufanya biashara kama ni hivyoo! Ni afadhali kama hujui ukae Kimya!
wewe ndio hutaki kuelewa huo ni mfano angeweza kusema hata 6%and kinachoandikwa no 3% then hiyo nusu inatoka bila,bank procedure ,sasa wewe ,akili yako umebeba hiyo error ,kama kigezo ...
 
unamaanisha kilankitu lazima kiandikwe kwenye makaratasi,aliyekwambia 10%huwa zinaandikwa ni nani, official contract ni 8% lkn mkakubaliana kuwa nitakupa,6% per utajuaje we we???

Yaani kuna shida . . . . Mungu at ukumbuke Watanzania honesty ni a scarce resource
 
Kimfano hela zinazotolewa kwa ajili ya kaya maskini, ni hela za serekali, kwa sababu iliona kuna kaya haziwezi kujimudu"

Vilevile serekali ikiona wakulima hawawezi kuzalisha vzr inatakiwa itoe hela (ruzuku) ili wakulima waweze, mf: mahindi ni sh 500@kg serekali kupitia vyama vya ushirika inaweza kununua kwa 600, ili tu kuboost wakulima.

Vile vile secta binafsi\ biashara, inapokuwa taabani kama (sasa) serekali ni wajibu wake kusaidia kwa kuzipa bank mitaji bila interrest yeyote" ili kusisimua biashara na uwekezaji, baadae itakusanya kodi. Hiyo ndo faida yake"

Mi nawashangaa wanaoshabikia serkali kuondoa hela bank za biashara, tena hao hao wanalalamika maisha magum! Serekali haina biashara zaidi ya kuchukua huku na kuhamishia kule lengo kubwa ni kuweka mazingira mazuri ya watu kujiimarisha kiuchumi,
 
Sijaelewa mada yako. Hebu tuambie proceedures za kutoa fedha za serikali bank (withdrawing)

Hebu jiulize faida au interest itokanayo na kudeposit FDR inawekwa kwenye account gani au ya nani baada ya FDR kumature?

Pia jiulize bank inapata faida kubwa kivipi ndani ya miezi walau 3 inaweza kumlipa depositor na yenyewe kubakia na fedha?

Kazi ya centralbank ni zipi?

Ukijua mlolongo wote huo utaona Ndulu yupo sahihi
Maswali mengi ya nini.
Selikari imetoa pesa kwa ajili ya matumizi kwa nini uweke ktk fixed account.
Tuseme matumizi ya pesa mfano mikopo kwa wanafunzi madawa nk,yasubilie huo muda mliokubaliana na benki?
Wacha ukweli usemwe
 
Kimfano hela zinazotolewa kwa ajili ya kaya maskini, ni hela za serekali, kwa sababu iliona kuna kaya haziwezi kujimudu"

Vilevile serekali ikiona wakulima hawawezi kuzalisha vzr inatakiwa itoe hela (ruzuku) ili wakulima waweze, mf: mahindi ni sh 500@kg serekali kupitia vyama vya ushirika inaweza kununua kwa 600, ili tu kuboost wakulima.

Vile vile secta binafsi\ biashara, inapokuwa taabani kama (sasa) serekali ni wajibu wake kusaidia kwa kuzipa bank mitaji bila interrest yeyote" ili kusisimua biashara na uwekezaji, baadae itakusanya kodi. Hiyo ndo faida yake"

Mi nawashangaa wanaoshabikia serkali kuondoa hela bank za biashara, tena hao hao wanalalamika maisha magum! Serekali haina biashara zaidi ya kuchukua huku na kuhamishia kule lengo kubwa ni kuweka mazingira mazuri ya watu kujiimarisha kiuchumi,

Tatizo letu ni ufisadi . . . Watu wana abuse hizo services za serikali . Badala ya hayo kufanyika kwa public interests wahusika wamejiamulia kupata faida binafsi na kuweka sheria zenye safety nets kwa hizo mulpractices sasa ukiwa wewe ni kiongozi utafanyaje ?

Corruption imeleta abuse of power and position alafu eti wame i brand ni capitalism . . . Capitalism isn't synonymous to theft. . .
 
Kimfano hela zinazotolewa kwa ajili ya kaya maskini, ni hela za serekali, kwa sababu iliona kuna kaya haziwezi kujimudu"

Vilevile serekali ikiona wakulima hawawezi kuzalisha vzr inatakiwa itoe hela (ruzuku) ili wakulima waweze, mf: mahindi ni sh 500@kg serekali kupitia vyama vya ushirika inaweza kununua kwa 600, ili tu kuboost wakulima.

Vile vile secta binafsi\ biashara, inapokuwa taabani kama (sasa) serekali ni wajibu wake kusaidia kwa kuzipa bank mitaji bila interrest yeyote" ili kusisimua biashara na uwekezaji, baadae itakusanya kodi. Hiyo ndo faida yake"

Mi nawashangaa wanaoshabikia serkali kuondoa hela bank za biashara, tena hao hao wanalalamika maisha magum! Serekali haina biashara zaidi ya kuchukua huku na kuhamishia kule lengo kubwa ni kuweka mazingira mazuri ya watu kujiimarisha kiuchumi,

Acha kusikiliza hao waliyobanwa na walizoea kukopa kwenye mabank sasa wanakuta milolongo mirefu kweli! ukweli ni kwamba Mabenki mengi ni ya kigeni hayafanyi kazi na Wananchi masikini wanataka kutanya biashara na serikali na Matajiri tu. Na hizi bank zikipata faida zinapeleka kwngine kuwekeza. Sasa Serikali haitaki kufanya biashara na banks inataka bank zikope serikalini pesa serikali ipate faida. Na faida iongeze mapato ya serikali sasa banks walivyo na nongwa wamegoma kukopa Bank kuu. Wanavizia vihela vyoyote vya serikali wanafanya mtaji wa kufanyia biashara. Nimeandika kwa Lugha rahisi kabisa nadhani utaelewa.
 
Naona kila mtu ameshakuwa mtaalamu wa fixed deposits za mabenki sasa. Kwanza mtoa mada unasema fixed deposits accounte ni current bank assets? Deposits zote za wateja kwa upande wa benki ni liabilities maana ni mali za watu. Kuwa current au non-current ni suala la maturity yake.
Pia hayo mambo ya rushwa kwenye kuweka fixed deposits accounts suluhu yake sio kukataza FD kwa taasisi za serikali. Bali ni kuzuia mianya. Kwa mfano, kama taasisi ina pesa ambazo haitazitumia kwa mwaka mmoja ni kwa nn isitafute bank inayotoa interest nzuri ya FD ili wapate faida? Pesa zinapokaa BOT bila interest maana yake ni nini? Labda BOT wangeanzisha kitengo cha commercial banking ili pesa hizo zipate faida. Sibishi kwamba kuna uwezekano wa mianya ya rushwa ila sikubaliani na solution ya kupiga ban hizo accounts
 
Mkuu Jiongeze,
Mabenki yanafanya sana lobbying ili makampuni,mashirika na idara za serikali ziweze kuweka pesa kwenye fixed deposit, kabla ya hapo makubaliano hufanyika kwa interest ngapi FDR Italipwa, Pesa zinazoingia kwenye FDR Akaunti ni kwa mujibu wa makubaliano, lakini percent ya rushwa anayopata mleta dili haiingii kwenye FRD, Benki wana jua namna gani wana account kwa percent ya mleta dili.

Hela ya deal ina majina mengi . . . Inaweza itwa facilitation fee . . . Ndugu kuna wakati nilikopa bank moja na nilitaka kurudisha mwaka huo huo wakasema kwa time frame hiyo haiwwzekani . . . . Interests zile zina complex number ndani yake ambayo ni passwords za bank . . . . We jiulize kwanini hawa financial leaders wanang'ang'ana kuzitetea hata baada ya kiongozi mkuu kuzi kataza ? What is the motive ?
 
Back
Top Bottom