GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Riba ya Mabenki kukopesha wateja wao sio suala la kisiasa, Huwezi ukasema kuanzia Leo Mabenki ya biashara riba ya kukopesha iwe asilimia kumi 10%
Mabenki kukopesha Raia au wateja wake kinachoangaliwa ni:
1. Vihatarishi (Risk) vinavyoizunguka biashara au kazi ya mteja husika, Biashara au kazi isiyoeleweka yaani tia maji tia maji ni ngumu sana Benki kujilipua kukukopesha kwa riba ndogo kwani hawajui hatima ya pesa zao( Na hizi pesa Bank inakopesha sio zao bali baadhi ya Raia waliozidiwa na pesa na hawana matumizi nazo kwa wakati huo wameamua kuzitupa pesa zao Bank)
Siku waliozidiwa na pesa na kuamua kuziweka Bank wakizihitaji pesa zao hakuna mjadala na Bank, Bank Inatakiwa kuzitoa bila kusingizia hazijarudi kwa kukopesha makapuku kwa riba ndogo
2. Uwezo wa mkopaji kurudisha deni( Creditworthiness of the borrower). Mteja ambaye yupo vizuri na amekamilika ni rahisi kupunguza riba kuliko kapuku asiye na kitu chochote, Kapuku ni ngumu kufahamu matarajio ya biashara au kazi yake ndani ya miaka miwili au mmoja ujao, Hatari iliyopo kwa kapuku ni kubwa kuliko kwa Tajiri,
Wanaosubiri Mabenki kushusha riba kwa Matamko ya kisiasa, Hii kitu kwenye uchumi huria haipo,
Ni bora ukaweka riba kubwa ili pesa yako irudi kwa wingi haraka haraka hasa kwa wafanyabiashara na wafanyakazi tia maji tia maji kuliko ukaweka riba ndogo itakayofanya mrejesho uwe kidogo na kupata hasara kubwa kapuku akishindwa kulipa deni lake
Serikali hata wakashusha riba zao za Bank za biashara kukopa Bank kuu(BoT) yaani landing rate hii haiathiri riba za Mabenki kukopesha Raia zaidi inasaidia Mabenki Kuongeza Deposits(Pesa za kukopesha Raia)
Riba ya mkopo ni Negotiable( Inajadilika) kama tu upo vizuri na unaeleweka mbele za wakopeshaji
Mtu kama Bakhresa au Asas Ltd anaweza kopeshwa na Mabenki dollar za marekani hata kwa riba ya asilimia nne 4% lakini sio wewe Kapuku, Hatari ya kuweka riba ndogo kwa kapuku ni kubwa zaidi
Mtu mwenye Fixed Deposit Bank ni rahisi zaidi kumkopesha pesa, Akishindwa kulipa tayari Bank ina fixed deposit yake kama dhamana, Mtu wa Mtindo huu unaangalia tofauti ya riba uliyompa kwenye fixed deposit na Kuongeza kidogo kwenye mkopo
N. B
Kumbuka Bank ni neno tu, Bank zipo pale kutokana na Pesa za wateja wao walioziweka, Hizo pesa ndio Bank inapata kiburi cha kukopesha Raia, Bila watu kuweka pesa Bank, Hakuna biashara ya Bank za biashara
Ni nani aliyetayari kuweka pesa Bank yaani kuikopesha Bank Halafu baada ya mwaka unaambiwa pesa zako tulimkopesha Mwanaidi Binti CCM hajarudisha, Utawaelewa?
Je watanzania sisi tupo kundi gani la kukopesheka? Level ya kapuku, Level ya kati au Matajiri
Nchi tajiri zinakopeshwa kwa riba ndogo kuliko nchi maskini, Huo ndio uhalisia