Naomba kuelimishwa kuhusu UTT-AMIS na Fixed Accounts

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Kuna pesa kidogo nataka niiwekeze ili isikae tuu kwa kipindi ambacho napambana kufikisha amount flani ambayo itahitajika kufanya business flani lakini pia nikiwa nimebanwa na kazi.

Binafsi hakuna kitu tofauti nilikua najua zaidi ya fixed acc za banks, japo nazo ni kwa kusikia tuu ila sijui zinavyofanya kazi.

Nikamuuliza mshkaji wangu kuhusu fixed accounts yeye akaenda mbali kwa kunitajia kitu kigeni, nacho ni UTT ambacho pia hakunipa maelezo ya kujitosheleza.

Kwahio nikawa nimeletewa jambo jipya ikiwa bado la kwanza sijaliewa,
Nikaona nilichukue hili nililete kwenu, pengine hapa ikaja options nyingne tena zinazoendana na hizi.

Hivyo naomba mwenye kujua kuhusu hizi mambo?
Kama
Kiasi cha chini cha kuweka..
Kwa muda gani(minimum)?
Faida zake zipoje?

Nb . Naomba tusizungumzie kuhusu kufungua biashara au chochote kitakachohitaji Nikisimamie/Muda wangu kwa Sasa.
 
UTT AMIS - Unit Trust of Tanzania and Asset Management and Investors Service

Ni mfuko wa pamoja = Wawekezaji mnakusanywa kwenye huu mfuko na kwa pamoja pesa yenu yote inayopatikana inafanyiwa uzalishwaji kwenye biashara za fedha na wataalamu wabobezi kwenye mambo ya mssoko ya fedha na baada ya faida kupatikana basi wote mlioweka pesa kwa pamoja mnarudishiwa faida. Vile vile kuna uwezekano wa hasara.

Ni taasisi ya serikali iliyopo kisheria na hatari ya hsara ni ndogo sana (kama watalaamu wa haya mambo wanavyozungumzia)

Njia ya uwekezaji ni kununu vipande kwenye mifuko ya pamoja. Pamoja na riba ya 12% hadi 15% kwa mwaka, thamani ya vipande inaongezeka.

Mfano Ukinunu kipande kimoja leo kwa 100, baada ya muda unawez kukiuza kipande kwa 150 na unaambulia faida ya 50.

Kikubwa youtube.com zipo kideo nyingi za kuelimisha juu ya jambo hili.

Utakapo amua kuwekeza wekeza kwenye mfuko wa ukwasi (liquid fund).

Asante
 
Asante,kwa maelezo mazuri,kingine nilichojifunza kwenye huu mfuko ni kwamba security ya fedha yako ni kubwa ila faida ni kidogo ukilinganisha na mtu anayeizungusha hiyo fedha kwenye biashara mwenyewe.
Binafsi huwa naona fedha yako hasa kama ni ndogo inazaa 1% kwa mwezi,kwenye milioni moja unapata 10k kwa mwezi.
 
UTT interest haikatwi kodi lakini Fixed Deposit Account interest inakatwa kodi ya 10% (Withdrawing tax).
Kama una pesa ya ziada na hauna muda wa kusimamia biashara ni uwekezaji mzuri. Kuna jamaa tulianza naye uwekezaji UTT pale tu mfuko ulipo anzishwa mwenzangu akawa anaendelea kuweka kila mwezi.... sasa pesa yake inamuingizia Sh. 75,000/- kwa siku.
 
Back
Top Bottom