Rungwe ‘Mzee wa Ubwabwa’ alazwa KCMC

Rungwe ‘Mzee wa Ubwabwa’ alazwa KCMC

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
rungwe_1.jpg


DAR. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe maarufu Mzee wa Ubwabwa amelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (KCMC) kutokana na uchovu wa kazi nyingi.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Gabriel Chisseo, Rungwe alifikishwa hospitalini hapo tangu juzi Juni 14 baada ya kuzidiwa na uchovu.

“Ni kweli tuko naye hapa tangu juzi tumempumzisha. Ni kwa sababu ya uchovu wa shughuli zake, hivyo tumempumzisha kwenye wodi za watu maarufu,” amesema leo Juni 16.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Taarifa kwa Umma wa CHAUMMA, John Mrema alipoulizwa hali ya afya ya Rungwe alikiri kweli anaumwa, ila akasema hilo ni suala la kifamilia.

“Alikuwa anaumwa akampumzishwa tu, lakini ameshatolewa. Taarifa kamili itatolewa na familia,” alisema awali.

Hata hivyo, baadaye, Mrema alisema Mzee wa Ubwabwa amerejeshwa hospitalini hapo, baada ya hali yake kubadilika.

“Amerudishwa ‘hospitali, ila KCMC ndio watatoa taarifa rasmi.”

Takribani wiki mbili sasa, CHAUMMA wamekuwa kwenye mikutano ya Operesheni C4C wakizunguka mikoani wakiongozwa na Mzee wa Ubwabwa.
 
Back
Top Bottom