Watu 18 wamefariki dunia katika Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya hii ni baada Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo kusababisha maporomoko ya udongo kutoka milimani kuvamia Makazi ya Wananchi katika kata mbalimbali.
Timu ya Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Kamati ya Ulizi na Usalama Wilaya ikiongozwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya Josephine Manase imefika katika eneo la tukio ambapo taarifa za awali zinaeleza kwamba mvua hizo zilisababisha udogo na mawe kusombwa kwa kasi kutoka milimani na kufunika nyumbankadhaa hali iliyopelekea maafa ya vifo pamoja na uharibifu wa mali.
Aidha zoezi la uokoji linaendelea ambapo watu kadhaa waliofukiwa na vifusi wameokolewa huku juhudi za kuwaokoa zikiendelea kuhakikisha watu wote wanaokolewa kutoka kwenye vifusi ambapo badhi ya miili ya Marehemu imeanza kuzikwa leo kwa kufuata taratibu za kidini na Majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabubkatika hospitali za karibu.
Hata hivyo Mamlaka zimewataka Wananchi wanaoishi maeneo ya milimani na mabondeni kuchukua tahadhari zaidi wakati huu wa mvua kubwa ili kuepuka maafa kama haya kutokea tena.