jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,991
- 4,361
Polisi Mkoani Rukwa linawasaka wanafunzi waliofunga ndoa miezi mitatu iliyopita.
Habari kamili ya ndoa hiyo iliyofungwa kanisani ipo hivi…..
Binti wa miaka 15 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Chipu Manispaa ya Sumbawanga amefunga ndoa na mvulana wa miaka 17 ambaye pia alikuwa mwanafunzi.
Wanandoa hao ambao wametoweka walifunga ndoa miezi mitatu iliyopita katika kanisa Katoliki la Mlangali ndani ya manispaa hii.
Wakisimulia wanakijiji walisema kuwa mara baada ya ndoa kufungwa kanisani wanandoa hao wawili walirudi kijijini hapo ambapo tafrija kubwa ilifanyika huku ikihudhuriwa na ndugu,jamaa na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Chipu ambapo wanandoa hao walikuwa wakisoma kabla ya kuamua kuoana kwa ndoa takatifu kanisani.
Mwanahabari wetu alifika kiijini hapo na kuhojiana na Katekista(mwalimu wa dini) ndugu Florence Sangu ambaye alikiri kuwa aliwapatia wanandoa hao mafundisho ya ndoa katika kanisa lililopo kijijini hapo.Alidai kuwa pia tangazo la ndoa lilitangazwa kwa muda wa wiki tatu ili kama yupo mwenyepingamizi ajitokeze lakini hakuna aliyejitokeza kupinga ndoa hiyo.
Wanandoa hao waliamua kukimbia kijijini hapo na kwenda kusipojulikana mara baada ya kupata taarifa kuwa Jeshi la Polisi linampango wa kuwakamata kwa kuwa wameacha shule na kuamua kuoana. Wanandoa hawa walishindwa kufanya fungate ili kukimbia mkono wa sheria.
Baadhi ya wanakijiji walisema kuwa ndoa iikuwa sahihi kwa kuwa wanafunzi hao walikuwa watoro wa shule. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kata ya Kasene ndugu Ludimila Ndinda alisema kuwa anafahamu ndoa hiyo lakini alikuwa hajui kuwa wanandoa hao walikuwa wanafunzi.
Afisa elimu wa manispaa ya Rukwa kwa shule za msingi ndugu Frank Sichwale aikiri kupata taarifa za ndoa lakini hakuwa na maelezo ya ziada, naye mwenyekiti wa bodi ya shule alionyeshwa kushangazwa kwake kwa wananfunzi kufanya ndoa tena tafrija ya ndoa hiyo ikihudhuriwa na walimu.
Kamanda wa polisi mkoa ndugu George Kyando alisema kuwa Jeshi la Polisi linawatafuta wanandoa hao ili kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Soma: Gazeti la DAILY NEWS LA TAREHE 10 October 2016