Ruhsa Kujiua Ukitimiza Miaka 70 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ruhsa Kujiua Ukitimiza Miaka 70

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ruhsa Kujiua Ukitimiza Miaka 70
  [​IMG]
  Thursday, March 11, 2010 3:11 AM
  Serikali ya Uholanzi inategemea kupitisha sheria yenye utata itakayowaruhusu watu wenye umri kuanzia miaka 70 kujiua wenyewe kwa msaada wa madaktari iwapo watahisi kuwa wametosheka na maisha duniani. Watu wenye umri zaidi ya miaka 70 wataruhusiwa kujiua kwa kusaidiwa na madaktari iwapo wataona wameishatosheka na maisha yao hapa duniani.

  Watu ambao hawana ujuzi wa udaktari watapewa mafunzo jinsi ya kuwasaidia wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 kujiua kwa kutumia sindano za sumu hospitalini.

  Bunge la Uholanzi linatarajia kuujadili muswada wa sheria hiyo baada ya watu wanaoipigia kampeni sheria hiyo kukusanya sahihi za watu 112,500 wanaounga mkono sheria ya kuruhusu watu kujiua.

  Watetezi wa sheria hiyo wamesema kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kutawawezesha wazee kuamua kufariki kimya kimya kwa utulivu pindi watakapoona wamechoka kuishi na wanataka kuepukana na pilikapilika za dunia.

  Wasaidizi wa madaktari watakaokuwa wakichanganya dawa ya sumu itakayotumika kuwaulia wazee watakaojitokeza.

  Hata hivyo mashirika ya kidini yameelezea kupinga kwake kuruhusu watu kujiua eti kwasaabu ya kuyachoka maisha.
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,757
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Is that what we call Euthanasia?
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hiyo nchi kiboko! Lakini si ndio wenye asili ya ukatili hao?
   
 4. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii si ndo ile nchi inayoruhuru kuvuta bangi? machizi tupu
   
 5. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kiimani za dini hii haijakaa vizuri kwani kwa Wakristo, kwa mfano, kujiua ni dhambi ya mauti (mortal sin) na uki-commit suicide kamwe huwezi kuuona ufalme wa Mbingu. Lakini wazungu wengi increasingly wanakuwa machizi na wanafanya mambo ya ajabu sana!
   
Loading...