Rufiji: Watuhumiwa wawili wa mauaji ya Pwani Wauawa

Polisi waua watuhumiwa wawili Leo huko Kibiti walikuwa maporini.

=====

UPDATE


Katika eneo la utende kata ya Ikwiriri, Tarafa ya ya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji kanda Maalum ya Polisi Mkoa wa Rufiji, Askari Polisi walifanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea Wilaya tatu za kanda Maalumu ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

DCP Liberatus Sabaas amesema, Polisi imemuuwa kiongozi wa mauaji ya kibiti Abdallah Ally Ngande Makeo aliyekuwa akitafutwa kipindi kirefu. Nafikiri hapa DCP Liberatus Sabaas amechanganya Majina kwani aliyekuwa anatafutwa Kipindi kirefu na Majina yapo kwenye magazeti anaitwa Abdurshakur Ngande Makeo. Aidha atakuwa ni Mpya au majina amejichanganya.

Majambazi walikuwa watano, askari wajibu mapigo na kuwajeruhi watu wawili kati ya wale watano ambao wamefariki wakati wakikimbizwa Hospitali ya Muhimbili. Katika tukio hilo, Polisi walikamata Silaha moja aina ya Rifle 375 ambayo imekatwa kitako na mtutu ikiwa na Risasi Mbili.

Sent using Jamii Forums mobile app


Du watafanikiwa lini kuwafikisha hospitalini maana kila siku wamefariki wakati wanakimbizwa hospitalini
 
Kwenye video kamanda Liberatus anasema walikuwa watu wanne au watano!!! Hivi mchana kweupe askari anashindwa kusema kwa uhakika kuwa ni watu wanne au watano. Yani sielewi, kamanda , washukiwa walikuwa wanne au watano?

This tells you something. Alafu watuhumiwa wa mauaji ya kibiti wanatembea kundi mchana kweupe na rifle yenye risasi mbili? Does this story resonate in anyones head?

Ok, Mara ya mwisho walipouawa washukiwa wawili na wengine kukimbia, ile manhunt iliishiaje? Au waliokimbia walitoweka kabisa?
Yani mtu ameshaonekana mchana kweupe na akakimbia huku askari wanamuona na anashindwa kupatikana ndani ya wiki mbili?

Mimi hamjaniokota kwa taarifa kama hizi.
Inaelekea wewe siyo mTanzania. Unauliza maswali magumu siyo kawaida yetu.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Jamani mtawaua watu wasio na hatia kisa washukiwa. Nadhani sasa polisi wakikukuta tu porini unakula risasi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeamini kweli wanasheria ni wasomi, wao huwa hawamtendei mtuhumiwa kama nwenye hatia hadi pale inapojulikana waziwazi bila uwepo wa shaka yoyote kuwa anayohatia.
Sasa hawa polisi wanauwa watu ambao "huenda" hawana hatia.
Tanzania sio nchi ya amani tena! Mungu ingilia kati usimame mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unaweza kututhibitishia kwamba walouwawa ni watunza mashamba?
Unaweza ukawa na taarifa nzuri sana ww.
Where is justice? Where is presumption of innocence?
Hebu tuthibitishie kuwa walouwawa ni kweli wanayohatia.
Tuziheshimuni kanuni za kisheria, Amani itakuja. Kama walouwawa sio wahusika basi ndugu zao lazima wawe maadui wa serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sijamsikia vibaya huyo Mkuu wa hiyo Operation huko amesema kuwa walipowafukuza hao Jamaa walikimbia msituni huku wakirusha risasi angani sasa nauliza kama hao Maadui kumbe walikuwa wakirusha risasi angani na si Kwao hao Mapolisi ilikuwaje wao Mapolisi ambao naamini wana Mafunzo ya kutosha waliamua kuwauwa moja kwa moja pasipo hata kutumia Mbinu zao ili wawakamate wakiwa hai kusudi waweze kuwahoji na wapate taarifa zaidi ambazo zingeweza kuujua Mtandao wao wote?
 
Back
Top Bottom