Rufaa vyeti feki/utata hadharani

mkuu mie sina shida,tatizo langu halikuwa cheti faki,cheti changu kilionekana kutumika zaidi ya halmashauri moja.Na hii ilkuwa ni uzembe tu wa utumishi kwani hiyo halmashauri nyingine nilikuwa nafanyia kazi kabla sijahamishwa.Sina wasiwasi na hilo mkuu nilikuwa najua ni swala la muda tu
Kwani mkuu waliokuwa na vyeti vya utata na incomplete nao walisimamishiwa mishahara hayo?
 
Kwani mkuu waliokuwa na vyeti vya utata na incomplete nao walisimamishiwa mishahara hayo?
incomplete hawakusimamishiwa walipewa miezi 3 kuwasilisha vilivyokosekana.vyeti vyenye utata walisimamishiwa.Kumbuka vyenye utata ni wale waliooneka vyeti vyao vinatumika zaidi ya Halmashauri/taasisi moja,walisimamishiwa ili kubaini mwenye vyeti ni nani
 
Nashindwa kuliweka hapa, lakini kwa kifupi.

RUFAA VYETI NDIO BASI
Na Nasra Abdallah

Unaweza kusema watumishi wa umma waliokutwa na vyeti feki kisha kukata rufaa, hatma yao kurudi kazini ipo shakani.

Utata huo unatokana na serikali kushindwa kutangaza matokeo ya rufaa zao huku ikitangaza ajira lukuki kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliong'olewa kwa kukutwa na vyeti feki, bila bila kujali kwamba baadhi yao waliondolewa kimakosa.

Hadi jana serikali imeshindwa kutangaza matokeo ya rufaa zao kama ilivyoahidi kufanya hivyo juni 30, mwaka huu.

Majibu yaliyotolewa jana na waziri mwenye dhamana na utumishi wa umma, Angela Kairuki, yaliongeza giza na utata juu ya hatma ya watumishi hao waliokata rufaa huku wengi wao wakiwa na imani ya kurudishwa kazini.

Waziri Kairuki alipoulizwa na gazeti hili ili kujua nini kimesababisha ukimya wa hatma ya rufaa za watumishi hao, alijibu kwa kifupi kuwa mchakato wa kupitia rufaa zao haujakamilika na utakapokuwa tayari umma utajulishwa.

Alipoulizwa kama mchakato haujakamilika kwa nini wametangaza ajira mpya:"Ndugu mwandishi nimekuambia kuwa tukishakuwa na taarifa zote kuhusu suala hilo tutawaiteni, kwa sasa sina majibu yoyote kwa hayo unayoniuliza naomba unielewe.

KWA KIFUPI NI HAYO, ZAIDI TAFUTA GAZETI USOME.

Lakini kama habari yako ni ya uhakika ni vyema sana
Kilichobaki kwa hili gazeti ni KUFUTWA KABISA
 
Itakuwaje kama nafasi zao wengine wamechuka kuteuliwa kupitia barua rasmi na kuajiriwa
 
mkuu mie sina shida,tatizo langu halikuwa cheti faki,cheti changu kilionekana kutumika zaidi ya halmashauri moja.Na hii ilkuwa ni uzembe tu wa utumishi kwani hiyo halmashauri nyingine nilikuwa nafanyia kazi kabla sijahamishwa.Sina wasiwasi na hilo mkuu nilikuwa najua ni swala la muda tu
Wewe tatizo lako ni tofauti na mtumishi hewa au aliyegushi. Kama uliwasilisha vyeti vyako OG upya wakahakiki upya ni vizuri na utarudishwa tu kazini tulizana moyo. Hii haimaanishi kwamba kila aliyeondolewa utarudishwa,bali wasafi tu
 
Ni kweli wapo waliocheza na matokeo, wengine imewakuta Bahati mbaya na watu walikuwa wanaitwa NECTA.

Nafikiri upembuzi wa maana utafanyika
 
Wizara ya utumishi imetoa maelekezo kwaa maafisa utumishi kuhakikisha waatumishi wote ambao wamekutwa hawana hatia baada ya kukata rufaa kufuatia kadhia ya vyeti vyenye utata na vyeti feki wanarudishwa kwenye payroll ya mwezi wa saba haraka kabla haijafungwa.Nimejaribu kutafuta hayo majina bila mafanikio.
Naomba mwenye List ya hao wahanga atusaidie tafadhali

Mkuu kunamtu kanipigia orodha ya majina imetoka, lakini bado haijanifikia.
 
Wizara ya utumishi imetoa maelekezo kwaa maafisa utumishi kuhakikisha waatumishi wote ambao wamekutwa hawana hatia baada ya kukata rufaa kufuatia kadhia ya vyeti vyenye utata na vyeti feki wanarudishwa kwenye payroll ya mwezi wa saba haraka kabla haijafungwa.Nimejaribu kutafuta hayo majina bila mafanikio.
Naomba mwenye List ya hao wahanga atusaidie tafadhali

Tumeshasahau na tumeanza shughuli za kilimo
 
Vp nawale waliogushi wakaenda kulalamika yametoka au yametoka yaliokuwa na utata tu?imean waliochangia vyeti tu
 
Wapewe haki zao zote toka waliposimamishwa hadi sasa.

Back
Top Bottom