Rubani wa US Airways afunga break ghafla - abiria matuambo moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rubani wa US Airways afunga break ghafla - abiria matuambo moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Apr 19, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Tuliondoka April 16 jioni toka Dar kupitia Nairobi kwa Swiss Air, April 17 baadhi ya tuliotoka East Africa na kuunganisha US airways kwenda kutalii Marekani tulionja joto ya jiwe tulioingia pipa la US airways kwenda Washington DC
  Dulls International Airport, dege hilo maalum kutuvusha bahari ya Atlantic lilijivuta taratibu kuingia njia ya kurukia, na kabla haijashika kasi rubani alisimamisha ghafla kwenye njia ya kukimbilia na tukasubiri kwa dakika kadhaa. Kisha akatangaza kwamba kumetokea tatizo la kifundi, kama angeamua kuruka tusingekuwa salama wakati wa kuruka au kutua. Hivyo aliruhusiwa kurudi tena kwa ajili ya matengenezo yaliyochukua takribani masaa mawili na ndipo tuliporuhusiwa kuruka tena. Pamoja na kuchelewa kuunganisha shuttle ya ndege nyingine DC, tunamshukuru rubani kutunusuru isije historia kujirudia mara kwa mara.

  Bongo walionisindikiza Airport nimefika salama na punde tu namaliza likizo ya utalii na nitakuwa bongo soon. Thanks a lot Pilot kwa uzoefu wako.
   
 2. LuCKNOVICH

  LuCKNOVICH Senior Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii nayo ni breaking news?.......
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna dalili ndege za hawa jamaa ziko choka ile mbaya. Picha hizi dege lao moja liliposhindwa kuendelea na safari jijini New York na kuishia rubani kulitua ndani ya mkondo wa bahari unaounganishwa na mto Hudson.

  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yes it is
   
 5. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo return ticket ushabadilisha usije safiri tena na US Airways, au ndiyo kujiandaa kukaa mkao mwingine wa "matuambo moto"? Lol! :smile-big:
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana. Hii ndege haikutumbukia majini kwa sababu ya hali ya choka mbaya. Kuna ndege waliingia kwenye injini wakati ilipokuwa inaanza kupaa. The accident was unavoidable and the pilot did a commendable job.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakushukuru kunishtua, kesho naenda kubadilisha ndege ya kurudi bongo, pamoja na fees zake bora kuliko kuingia ndege na roho juu juu nini kitatokea.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Utetezi dhaifu huo. Mbona uwanja wa KIA hapa kwetu Tanzania kumelalamikiwa sana tatizo la ndege kuingiliwa na ndege wengi zinaporuka na haijatokea ndege kutua ghafla? Na katika historia hatujapata kusikia ndege nyingine iliyotua ghafla sababu ya ndege kuingia kwenye engine. Kwa vyo vyote hiyo ilikuwa ni dalili wazi ya kujenga utetezi wa kosa la udhaifu wa ndege zao kuwa choka ile mbaya.
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  msalimie mkulog mwambie huku home mambo si mambo tena. Wabunge wa ndiyooo nao wanafuata upepo, japo kinafiki.
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  US airways wapo poa, sema midege yao inayofanya local trips ndiyo ipo mibovu. Locally piga JetBlue!
  Hiyo ndege imetokea wapi?.. Zurich?
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Subiri utakaposikia ndege (birds) wameingia kwenye injini wakati ndege (airplane) inapaa ndipo uje kutuambia utetezi dhaifu. The pilot of the plane that ditched in the Hudson River is an American hero.
   
 12. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Kaka hii ilibidi uwaambie ndugu zako waliokusindikiza, au unataka kusema kuna wa JF walijipanga na kukusindikiza airport? Kama ni ndugu na watu wako wa karibu, hauoni ingkuwa rahisi kuwajulisha tu hao kwa sms or email? au ni ulimbukeni wa kupanda ndege kwenda Washington, mbona hii ni kawaida tu jamani? hemu tuacheni ushamba na ulimbukeni bwana .... najua utapiga picha nyingi sana huko ... haya piga moja na fridge and ingine na video utuwekee hapa JF picha of the century .....


   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  JF bwana kuna vituko..si ungesema tu ulitaka tujue ulikuja na sasa umerudi huko amerika!! Yote haya mara breki ya ghafla mara sisi wa east africa,mara dull airport ya nini unajijazisha maparagraph wakati issue iko simple tu...
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo utaona tofauti kati ya wabongo na wa huko majuu. Sasa ili rubani la Dash 8 ya ATC kwa nini alikuamua kutokuruka baada ya kuona matatizo ambayo abiria waliya-notice? Home
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao birds ni hatari sana

  Kuna boeing ya ATC karibia ituangushe in 2006 pale KIA, waliingia hao brids kama wawili hivi na ile injini nadhali ilitupwa palepale

  BIRDS ARE VERY DANGEROUS HATA KAMA NDEGE IMENUNULIWA JANA
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  na siku ukipanda daladala la Tandale kwa mtogole likapata pancha urudi hapahapa kutuarifu.
   
 17. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Teh, nimeipenda hii! Ningebofya LIKE ila natumia mch.ina
   
 18. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  never mind nimekusoma wangu
   
 19. w

  warumu Member

  #19
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NHii yote misifa 2napotezeana time endelea na mishe zako!
   
 20. e

  emkey JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 728
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  2Mejua kama ulipanda ndege, wasalimie huko ulipo.
   
Loading...