RPC wa Kilimanjaro - Ng'hoboko hatunaye tena

Nadhani ni presha,, alipata uhamisho kwenda Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake pale inachukuliwa na SACP Absalom Mwakyomaa aliyekuwa rpc Pwani. Mapolisi wengi hawapendi kufanyia kazi makao yao makuu pale, wanapaona kama kijiweni infact ni kijiweni kwa mapolisi hawa corrupt maana pale hupati muda wa kukutana na raia ni mafile tu, sasa na marupurupu wanayopata mikoani huko basi taabu wakiambiwa wanakwenda makao makuu. R.I.P kamanda Lucas Lifan Ng'hoboko

huyu alikuwa RPC wa Mkoa wa Kilimanjaro...kabla ya kufariki leo asubuhi tayari alikuwa amekwisha staafu Utumishi wa Umma.Pole Ndugu jamaa na Marafiki

Nimeona mara nyingi sana hawa wazee hawataki kustaafu kazi sijui kwanini, wapo wengi sana ambao umri ukifika wanapata pressure huku wengine wakilazimisha kuongezewa muda kungangania ofisini; karibia kila Mkoa kuna Polisi na watumishi wa Umma waliostafuu wakaongezewa muda kana kwamba hakuna wengine wakuchukuwa nafasi hizo!

Kama ulivyo comment hakuwa waadilifu na walizoea rushwa na wizi wa ujanja ujanja hivyo wanajuwa wakiwa nje ya ofisi hakuna tena nafasi kama hiyo! Wengine wakistafu wanaenda kugombea Ubunge na wanarudi mrango wa nyuma kama mawaziri wa Kikwete na CCM huu wote ni mpango mchafu ambao lazima tuondokane nao! ni mfumo mbovu ambao CCM wameulea kwa miaka sasa bila hata kuchua hatua stahili.

Nilazima Ofisi kuu ya Utumishi iwe na mipango ya kuwatowa katika ofisi za Umma watu wanaokaribia kustaafu angalao mwaka mmoja kabla na kuwaweka katika kitengo maalum cha kuwaanda kisaikolojia kwa ajili ya kuishi maisha bora baada ya kustaafu.
 
It's now proved kafariki dunia akiwa kwenye likizo ya kustaafu, malaria ndo kilichoripotiwa kuwa chanzo.
 
Kwa mujibu wa TBC1 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Lucas Nghoboko amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa Malaria....

TBC wamemnukuu IGP Said Mwema kwamba Hayati Nghoboko alikuwa anajiandaa kuanza likizo ya kustaafu kazi...

Pole kwa familia ya Nghoboko....

Bwana alitoa,bwana ametwaa,jina la bwana lihimidiwe....

Upumzike kwa amani mzee wetu Lucas Nghoboko,daima tutakukumbuka......Amina.
 
Marehemu nakumbuka alikuwa mmoja ya watu waliokuwa wanajitahidi kuchakachua matokeo ya uchaguzi kilimanjaro.
Mungu amrehemu na amsamehe makosa yake aliyotenda huku duniani.
 
Marehemu nakumbuka alikuwa mmoja ya watu waliokuwa wanajitahidi kuchakachua matokeo ya uchaguzi kilimanjaro.Mungu amrehemu na amsamehe makosa yake aliyotenda huku duniani.
Mwenyezi mungu atuepushe na hili janga la washabiki wa chama hiki amina.
 
eeeh,majungu ukwel au kamba,kwan alikua anasumbuliwa na nin au aliugua ugonjwa gan?
 
Back
Top Bottom