Royal Tour na Vita vya Kiuchumi

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,391
9,665
Kwanza naomba nitoe declaration. Mimi ni mtanzania haswa ninaependa kuona maendeleo ya hii nchi.

Nirudi kwenye mada, hii royal tour ni deal sana hasa kwa namna inavyotarajiwa na watanzania wengi.

Sote tunaamini Tanzania itafunguka na tutapata pesa kwa ajili ya mradi.

Lakini pia Mimi niliamini kwamba kama huu uzinduzi ungefanyikia bongo na ikawa live kwenda kwao; nazani watu wangeelewa zaidi ni nchi gani hasa inazinduliwa kuliko kufanyika US.
Lakini si haba; wakimaliza huko waje na huku Tanzania, ili iwe live kutokea hapa kwenda huko.

Nasema hivyo kwa sababu; Siku zote wakenya wamekuwa wakitumia mlima Kilimanjaro kama mlima wao kwa sababu wanautangaza sana hasa wakiwa kwenye ndege zao na hiyo huwafanya watalii kuelewa mlima huo uko Kenya. Je hatuoni kwamba watu wengi watajua hiyo movie ni ya US.?

Vita vya Kiuchumi:
Miaka mingi tumekuwa wahanga kwenye utalii hasa kupitia jilani zetu.
Naomba niamini kwamba hata sasa bado wanatuandamana, lakini pia hawataifurahia hii Royal tour. Hivyo watakuja na mbinu mbalimbali kutudhoofisha.

Moja ya mbinu ndogo sana nii hii ya Binti wa Ki Nigeria, ametutikisa.

Pili hii hii ya game ya Simba na Orlando. Kocha katuchafua kwamba hatuna hospitality nzuri.

Tatu ni hili la Ngorongoro Crater. Tunaonekana kuwanyanyasa wanadamu, huku tunaenda kuwatangaza kama semehemu ya utalii. Hili nano linatubagaza.

Wale majilani zetu ni wa kuwaweka mguu sawa mapema saana ili wasiharibu. Lakini pia tujiandae kufanya vetting Kali sana ya wageni wanao ingia nchini. Kwa Sasa nchi imekuwa free sana lakini tunavyoanza kuwa serious na utalii kiasi hiki basi tujiandae kimiundombinu.

Mwisho, ni wapinzani wa mama ki siasa. Sijui ni kwa Nini Mama mwenyewe ameamua acheze hii movie wakati yeye ndio mtu wa mwisho kwenye mamuzi ya hii nchi.

Ikitokea shida kwenye hii movie nani ataaangushiwa hili zigo? .

Mfano. Ikifika hadi mwaka kesho mwezi kama huu watalii wakawa hoi hawajaja. Nani wa kulaumiwa? . Mama atajiteteaje?. Wapinzani wake wa kisiasa watamuacha wasimchafue? Hawatafanya kampeni ya kumuharibia hii movie.
Je, utulivu wa nchi utakuwa wapi? .

Mungu ibariki Tanzania!

NB: Nitakuwa Live kufuatiliwa uzinduzi hapo saa nane na nusu usiku wa Leo.

Karibuni nyote.
 
Hii vita ni kiuchumi tu au zaidi? Yule Mkenya na maandamano ya Paris anaitwa Omari, Kenya ni jirani na alshabab. Huyu binti Mnaigeria Zainabu, Nigeria wana bokoharum.

Hapo AYOtV online nimesikiliza hili sakata limemuingiza na Mrusi mtalii ambaye yeye na mke wake walimuhifadhi huyu binti hapo hotelini usiku ule aliotaka kubakwa. Mrusi kaoneshwa akitoa ushahidi wa hili tukio kwenye video clip. Hapa kazi iliyobaki ni kuunganisha dots tu.
 
Mchawi ni mama mwenyewe, haiwezekani hii filamu ya utalii uiite “ROYAL TOUR” ili hali nyuma ya pazia unawafukuza wamasai ambao ni wakazi halisi wa bonde la Ngorongoro.

Kumbuka wamasai haohao ndio waliofanya Ngorongoro kuwa kivutio kwa sababu ya maisha yao na wanyama mwitu, washauri wa mama naona huwa wanamtoa nje ya reli awe nao chonjo sana.

Kwa ufupi kulikuwa hakuna haja ya kuizindua hiyo filamu ilihali wahusika wakuu (Wamasai) wananyanyaswa kwenye ardhi yao ya nyumbani, hivyo hiyo filamu ni batili na imejaa uongo mtupu.
 
Kwanza naomba nitoe declaration. Mimi ni mtanzania haswa ninaependa kuona maendeleo ya hii nchi.

Nirudi kwenye mada, hii royal tour ni deal sana hasa kwa namna inavyotarajiwa na watanzania wengi...
Mkifundishwa Ujasusi wa kiuchumi na kidola nyie mko bize kutengeneza Kesi za kumbambikia Mbowe na Lissu. Mko bize jinsi ya kuiba uchaguzi wa 2025.

Mmeshapigwa za uso.
 
Back
Top Bottom