Router (MiFi) ipi inafaa kwa matumizi binafsi?

Mtemi01

New Member
Dec 23, 2023
4
3
Habari wana jamvi. Kutokana na changamoto ya gharama za vifurushi tunaelezwa kuwa angalau tukitumia router inapunguzakwa kiasi fulani.

Sasa naomba kujua router (MiFi) ya kampuni gani ni nzuri? Kwa maana speed, gharama lakini pia na uwezo wa kupatikana maeneo mbalimbali maana mi ni mtu wa kusafiri wakati mwingine nakuwa shambani ambako kimsingi mitandao ya simu inapatikana.

Asanteni
 
Kutokana na changamoto ya gharama za vifurushi tunaelezwa kuwa angalau tukitumia router inapunguzakwa kiasi fulani.
si kweli, MiFi ni portable router yenye uwezo wa kuwekwa sim card(line)
line ile ile unayoitumia kwenye simu, na gharama ni zile zile
 
Nilichkua Airtel 5G router 110,000 tarehe 25/12/2023. Ilikua inafanya kazi fresh na speed ni nzuri sana. Ila jana tarehe 20/01/2024 imegoma kabisa kushika. sasa sijajua ni shida ya mtandao kwa hali ya mawingu au ndio mwezi ukikaribia wanakata. Mwanzo speed ilikua nzuri ila mwisho. Nmeona ni Utapeli tu.
 
Shida ulkua mtandao man fibers zao kwenye mkongo wa taifa zilipata hitilafu sabu ya mafuriko..
 
Habari wana jamvi. Kutokana na changamoto ya gharama za vifurushi tunaelezwa kuwa angalau tukitumia router inapunguzakwa kiasi fulani.

Sasa naomba kujua router (MiFi) ya kampuni gani ni nzuri? Kwa maana speed, gharama lakini pia na uwezo wa kupatikana maeneo mbalimbali maana mi ni mtu wa kusafiri wakati mwingine nakuwa shambani ambako kimsingi mitandao ya simu inapatikana.

Asanteni
Kwa mifi most of time ukinunua mara ya kwanza ndio unapata GB nyingi, mfano Airtel walikua na offer mifi ya 50,000 wanakupa gb 80 bure, ila vifurushi ni vile vile vya kawaida.

Vifurushi vyao Vya bei nafuu ni vya wafanyabiashara (Sme) vipo mitandao karibia yote Tigo wana Postpaid, Airtel wana Sme, Voda wanayo pia japo kwa sasa imesimamishwa kwa muda. So we angalia shambani kwako mtandao gani una speed unga hio line kwa SME.

Pia zipo unlimited Tigo, Voda na Airtel atleast 70,000 Kwa mwezi.
 
Naomba list ya Unlimited na bei zake
 
Naomba list ya Unlimited na bei zake
-Voda kuanzia 115,000 (bure kuunganishwa)
-Tigo kuanzia 70,000 (650,000 kuunganishwa)
-Airtel kuanzia 70,000 (200,000 kuunganishwa) na 120,000 (bure kuunganishwa)

Hio mitandao ya simu.

Kampuni za waya
-ttcl copper inaanzia 25,000 (unanunua router 55,000)
-ttcl fiber kuanzia 55,000 bure kuunganishwa
-Raha (liquid) kuanzia 50,000 ila wanaisuport majengo na sio mitaa.
-Zuku kuanzia 69,000
-Go fiber kuanzia 75,000
-Net solution fiber kuanzia 60,000 (wanataka uanze na miezi 3)

Overall Airtel wapo vizuri zaidi na hio laki 2 wanakupa router yenye powerbank ambayo unatumia hata umeme ukikatika. Na internet za waya Overall Zuku wapo vyema kama eneo lako wamepita.
 
Nilichukua Router ya Vodacom, 120k
1708354300832.png

Pamoja na bundle ikawa 120k nyingine. Hii ni 5G, though I don't enjoy iyo 5G kiivyo. Speed yake ni 30mps.
Tupo tunachanga na wana pamoja kulipia, na ni post paid; hata mwezi ukikata tunaweza kulipa wakati siku za mwezi husika zinaendelea.
Sema bado I am judging myself kama ilikuwa ni good option.
One among the bad things about it ni kutokuwa na powerbank ila pia kuwa Postpaid meaning siku nikiwa mwenyewe na sina wadau wa kucooperate nao, nitakuwa naenda against terms and conditions.
 
Nilichukua Router ya Vodacom, 120k
View attachment 2909199
Pamoja na bundle ikawa 120k nyingine. Hii ni 5G, though I don't enjoy iyo 5G kiivyo. Speed yake ni 30mps.
Tupo tunachanga na wana pamoja kulipia, na ni post paid; hata mwezi ukikata tunaweza kulipa wakati siku za mwezi husika zinaendelea.
Sema bado I am judging myself kama ilikuwa ni good option.
One among the bad things about it ni kutokuwa na powerbank ila pia kuwa Postpaid meaning siku nikiwa mwenyewe na sina wadau wa kucooperate nao, nitakuwa naenda against terms and conditions.
Kama umetumia voda 30mbps ukienda hizo za bei rahisi za 10/20mbps uta downgrade.

Angalia location yako kama kuna fiber, hizo pekee ndio uta upgrade toka hapo, kama raha 125K ni 80mbps.
 
Nilichkua Airtel 5G router 110,000 tarehe 25/12/2023. Ilikua inafanya kazi fresh na speed ni nzuri sana. Ila jana tarehe 20/01/2024 imegoma kabisa kushika. sasa sijajua ni shida ya mtandao kwa hali ya mawingu au ndio mwezi ukikaribia wanakata. Mwanzo speed ilikua nzuri ila mwisho. Nmeona ni Utapeli tu.
Dah haya masuala ndio huwa yananikatisha tamaa kuchukua kifaa cha mwendokasi
 
-Voda kuanzia 115,000 (bure kuunganishwa)
-Tigo kuanzia 70,000 (650,000 kuunganishwa)
-Airtel kuanzia 70,000 (200,000 kuunganishwa) na 120,000 (bure kuunganishwa)

Hio mitandao ya simu.

Kampuni za waya
-ttcl copper inaanzia 25,000 (unanunua router 55,000)
-ttcl fiber kuanzia 55,000 bure kuunganishwa
-Raha (liquid) kuanzia 50,000 ila wanaisuport majengo na sio mitaa.
-Zuku kuanzia 69,000
-Go fiber kuanzia 75,000
-Net solution fiber kuanzia 60,000 (wanataka uanze na miezi 3)

Overall Airtel wapo vizuri zaidi na hio laki 2 wanakupa router yenye powerbank ambayo unatumia hata umeme ukikatika. Na internet za waya Overall Zuku wapo vyema kama eneo lako wamepita.
Airtel wamekuwa mchemsho kwangu, yaani sina hamu nao.

Nina router yao ya 5G yenye power bank nilinunua kwao kwa 210,000 na wakaniunganishia data ya unlimited kwa 70,000 kwa siku 30 mtandao ulikuwa mzuri sana.

Nilipokuja kununua bundle lingine la unlimited kwa 70,000 speed ilikuwa ya kinyonga, nikaachana nayo nikahamia Vodacom na router yao ya 5G, power bank ya router ya airtel ndio naitumia kwenye router ya Vodacom
 
Airtel wamekuwa mchemsho kwangu, yaani sina hamu nao.

Nina router uao ya 5G yenye power bank nilinunua kwao kwa 210,000 na wakaniunganishia data ya unlimited kwa 70,000 kwa siku 30 mtangao ulikuwa mzuri sana.

Nilipokuja kununua bundle lingine la unlimited kwa 70,000 speed ilikuwa ya kinyonga, nikaachana nayo sasa nimehamia Vidacom na router yao ya 5G, power bank ya router ya airtel ndio naitumia kwenye router ya Vodacom
Charge inasukuma mda gani
 
Natumia tigo router postpaid 100k napewa 140GB sijawahi ijutia kuanzia 2021
 
Attachments

  • 20240408_162710.jpg
    20240408_162710.jpg
    2.2 MB · Views: 6
Back
Top Bottom