Roughly 90% ya wanaume hawana confidence mbele ya wanawake!

Jana Ulirudi Usiku

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
2,363
2,261
Huu ni utafiti wa kweli, unaohusisha nchi hii ya TZ tu. Wanaume wengi karibu wote wa TZ wana confidence kwa wanaume wenzao tu, kwa akina dada wana sunder.

Nilipokuwa o level, nakumbuka wale wanaume wote waliokuwa vinara wa kuongea ongea na kuchekesha, waliburuzwa vibaya sana na akina dada kwenye debate.

Midahalo yote iliyohusisha wanaume na wanawake, 98% zote wanawake walishinda tena kwa kishindo, aisee wanaume walikuwa wanachapika vibaya sana.

Ipo hivi: wanaume wengi ikiwemo wa humu jamvini hawana ujasiri wa kuchuana kwa hoja 'man to woman' mbele ya kadamnasi ya watu, hata wale wanaojifanya humu ni alpha males hawafui dafu kwenye hiyo show ya man to woman contest.

Hapa kuna ya kutafakari mno, imagine ofisini ulitokea mdahalo wa hoja uliohusisha wanaume na wanawake, huwezi kuamini wadada walikuwa wakiongea kwa kujiamini with an impressive flow of points.

Hata enzi zile nilipokuwa chuo, kwenye presentations wadada walikuwa wanajiamini mno na nakiri kwamba waliwaburuza sana wakaka. Yaani mdada anakwenda mbele ana flow materials na analitawala jukwaa.

Shida ni nini? Kwa nini tumefika huku kote?
Yaani wadada wanajiamini kuliko wakaka? Wanaume wengi ni keyboard warriors, ukiwaleta kwenye 'man to woman' battle [Blmbele za watu[/B], wanapoteana vibaya mno.

Mifano ni mingi sana. Hili siyo la kuliangalia juu juu tu, wanaume mnafeli wapi? Binafsi nashukuru Mungu ninajiamini na kujikubali, ninamudu majibizano ya hoja na wanawake mbele za kadamnasi iwe kwenye semina au event yoyote.

Daaah! Mambo siyo mambo! Au ulaji wa ugali kwa muda mrefu unadumaza kujiamini, akili na words' flow ya wanaume wa kitanzania?

Ugali upigwe vita?

Natafakari tu, ila kwa kweli wanaume tujitathmini(hasa hao 98% ambao hawana confidence mbele za akina dada, ni aibu kubwa).
 
Mimi nadhani labda unalo wewe hilo tatizo wengine kozi tulizosoma ni za kujenga hoja..kumzidi mwenzio kwaio wengine tunawabalasa vilivyo hao wanawake tena kwa ngeli iliosimama vizuri....
 
Mtoa mada umeniangusha,
Haiingii akilini Mada nzito Kama Hii
Tena inayohusu Wanaume Watu wazima wa JF

Afu mifano hai unatuletea ya vivulana vyanafunzi vya shule, sijui chuo, Sijui debate,Sijui nn...

Yaani totally Mifano inahusu mambo ya kitoto kitoto ambayo uliowatolea mifano hata Hawajui kuitafuta Pesa Wala majukumu ya kiume na kifamilia hawana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom