ROSTAM, TAFADHALI BWANA!
Na. M. M. Mwanakijiji
Nyerere aliwahi kujiuzulu Ubunge kwa sababu ya msingi
Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius K. Nyerere (mgongano na wale ambao wanajaribu kumvua Ubaba wa Taifa unaendelea) aliwahi kujiuzulu Ubunge wake wa kuteuliwa akikataa kuburuzwa na serikali ya Mkoloni wakati tunaelekea Uhuru. Inanishangaza kuwa leo hii watu wanaojiona ni wanasiasa hasa wameshindwa kufuata mfano wa kujiuzulu katika hali ya kupinga serikali inavyofanya mambo. Wengi bila ya shaka wanajua zaidi kuhusu kujiuzulu kwa Nyerere nafasi ya Uwaziri Mkuu na kumuachia Kawawa baada ya Uhuru, wachache wanakumbuka kuwa Nyerere alijiuzulu Bunge kupinga sera na jinsi wakoloni walivyokuwa wakijaribu kumburuza pamoja na jitihada zake zote za kujaribu kufikia muafaka wa aina fulani.
Mwezi Julai 1957 Nyerere aliteuliwa kuwa Mbunge katika Baraza la Kutunga Sheria. Miezi michache kabla ya hapo alipigwa marufuku kuhutubia mikutano ya hadhara na mkoloni. Tarehe 14 Disemba 1957 aliandika barua ya kujiuzulu na siku mbili baadaye alielezea uamuzi wake wa kwanini alijiuzulu katika makala iliyotoka kwenye kijarida Sauti ya TANU. Katika maelezo yake marefu alielezea ni kwanini alikubali kuteuliwa kuingia Bungeni ya kuwa alifanya hivyo akiamini kuwa serikali ilikuwa na malengo ya kweli ya kushughulikia matatizo ya kisasa ya wakati huo. Miezi sita baadaye alijikuta kwamba amekubali kuachilia mambo mbalimbali ya msingi katika bona fide akiamini kwamba serikali nayo itakubali kuachilia madai au kubadilisha hatua zake mbalimbali.
Niandikie:
mwanakijiji@jamiiforums.com