Rostam! - Tafadhali Bwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam! - Tafadhali Bwana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 21, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  ROSTAM, TAFADHALI BWANA!
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Wananishangaza sana wale ambao wametoa kauli za kupongeza uamuzi wa Bw. Rostam Aziz kujiuzulu hasa wale wanaodai amefanya hivyo kwa maslahi ya taifa. Wananishangaza zaidi wanasiasa wa chama tawala na wa upinzani ambao wameweza kudai hadharani kuwa alichokifanya Rostam ni kitendo cha kuigwa. Lakini wanaonishangaza zaidi ni watu wote ambao wamefikia mahali pa kutukuza uamuzi wa Rostam kujiuzulu kana kwamba alifanya hivyo kuitikia wito wa baadhi yetu kumtaka ajiuzulu au alifanya hivyo kwa sababu ya kile kinachoitwa kujivua gamba.

  Ninashangaza na wote hao kwa sababu wanaopongeza uamuzi wa Rostam kujiuzulu wanafanya hivyo kama watu ambao hawajachukua muda kusoma hotuba yake. Ni kama watu walio wavivu kusoma, wagumu kuelewa, na wepesi kusahau. Rostam Aziz kujiuzulu kwani ni kwa kubeza; amefanya hivyo kwa sababu nyingine zote isipokuwa ile ya maslahi ya taifa. Simsingizii.

  Hotuba yake iliyokuwa na karibu kurasa nane ilikuwa na jumla ya maneno 3067. Kati ya maneno hayo:

  Neno “Wazee wangu” linatokea mara 34;Maneno “chama chetu” yanatokea mara 13; Neno “CCM” linatokea mara 16; Maneno “Halmashauri Kuu ya Taifa” linatokea mara 4
  Maneno “Kamati Kuu” yanatokea mara 6; Neno “biashara” linatokea mara 6; Neno “taifa” linatokea mara 8 - Mara 5 kati ya hizo likiwa linahusiana na Halmashauri Kuu ya Taifa au Kamati Kuu ya Taifa (vyombo vya uongozi wa CCM). Mara 1 likimtaja Baba wa Taifa na mara 1 likizungumzia “Waasisi wa Taifa letu” na sehemu nyingine likiwa kama sehemu ya neno jinginie yaaani “kitaifa, kimataifa”n.k; Neno “Tanzania” linatokea mara 6. Mara 3 kati ya hizo likitaja “watanzania”, mara 2 ikitaja nchi ya “Tanzania Bara” na mara 1 ikihusisha “Tanzania” na kufanyika kwa siasa chafu; Neno “nchi yetu” linatokea mara 7 - kati ya hizo mara 1 ni sababu ya yeye kuzungumza na wazee wa Igunga. Mara nyingine 6 ni katika kuendeleza wazo fulani; Neno “nchi yangu” linaonekana mara 1; Neno “Taifa langu” linaonekana mara 0; Neno “Watanzania wenzangu” linaonekana mara 1; Neno “wananchi” linatokea mara 4 na kati ya hizo hakuna kitu kama “wananchi wenzangu” na Neno “Wazee wetu” linatokea mara 1.

  Ndugu zangu, hapa ninawauliza wale wenye uwezo wa kufikiria, ni kitu gani kimewafanya waamini kuwa Rostam alijiuzulu au ameachia nafasi zake kwa sababu ya maslahi ya Taifa? Neno lenyewe “maslahi” linatokea mara moja na tena hapo ni katika kutaja “maslahi binafsi ya kikundi fulani cha watu.” Kimsingi hakuna sababu ya kiakili ambayo inaweza kutolewa na watu ya kwanini wanaamini kuwa Rostam alijiuzulu kwa sababu ya maslahi ya Taifa.

  Nyerere aliwahi kujiuzulu Ubunge kwa sababu ya msingi
  Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius K. Nyerere (mgongano na wale ambao wanajaribu kumvua Ubaba wa Taifa unaendelea) aliwahi kujiuzulu Ubunge wake wa kuteuliwa akikataa kuburuzwa na serikali ya Mkoloni wakati tunaelekea Uhuru. Inanishangaza kuwa leo hii watu wanaojiona ni wanasiasa hasa wameshindwa kufuata mfano wa kujiuzulu katika hali ya kupinga serikali inavyofanya mambo. Wengi bila ya shaka wanajua zaidi kuhusu kujiuzulu kwa Nyerere nafasi ya Uwaziri Mkuu na kumuachia Kawawa baada ya Uhuru, wachache wanakumbuka kuwa Nyerere alijiuzulu Bunge kupinga sera na jinsi wakoloni walivyokuwa wakijaribu kumburuza pamoja na jitihada zake zote za kujaribu kufikia muafaka wa aina fulani.

  Mwezi Julai 1957 Nyerere aliteuliwa kuwa Mbunge katika Baraza la Kutunga Sheria. Miezi michache kabla ya hapo alipigwa marufuku kuhutubia mikutano ya hadhara na mkoloni. Tarehe 14 Disemba 1957 aliandika barua ya kujiuzulu na siku mbili baadaye alielezea uamuzi wake wa kwanini alijiuzulu katika makala iliyotoka kwenye kijarida “Sauti ya TANU”. Katika maelezo yake marefu alielezea ni kwanini alikubali kuteuliwa kuingia Bungeni ya kuwa alifanya hivyo akiamini kuwa serikali ilikuwa na malengo ya kweli ya kushughulikia matatizo ya kisasa ya wakati huo. Miezi sita baadaye alijikuta kwamba amekubali kuachilia mambo mbalimbali ya msingi katika bona fide akiamini kwamba serikali nayo itakubali kuachilia madai au kubadilisha hatua zake mbalimbali.

  Mwisho wa siku aligundua kuwa serikali haikuwa tayari kubadili mwelekeo katika dhamira safi alijua kuwa asingeweza kuendelea kuwemo ndani ya Bunge ambalo haliko tayari kusikiliza hoja zake na hasa kwenye mambo ya msingi. Aliandika hivi (tafsiri toka Kiingereza yangu) “Kama ningeamini kuwa jukumu langu ndani ya baraza lilikuwa kutoa na siyo kuchukua, bado ningejiuzulu. Nimeweza kutoa kila kilichokuwa kwenye uwezo wangu kukitoa na vyote nilivyovitoa vimekataliwa. Niliingia Bungeni nikiwa na roho kidogo ya kutoa na kupokea. Hiyo roho haipo pale. Ningekuwa nawaibia wananchi, na kukiibia chama changu (angalia mfuatano wa wananchi na chama) kama ningeendelea kubakia humo, nikipokea posho na kuhudhuria tafrija kama Mbunge, watu wakiamini kuwa nilikuwa na manufaa fulani, wakati nilikuwa najua siku na manufaa yoyote. Hivyo sikuwa na uchaguzi bali kujiuzulu”.

  Uamuzi wa Nyerere kujiuzulu uliongozwa na kanuni; kanuni kwamba maslahi ya wananchi yako juu ya maslahi mengine yoyote yale. Leo hii Rostam amejiuzulu kwa sababu kubwa mbili - kama umesoma vizuri hotuba yake au kumsikiliza. Kwanza, ni kwa sababu ya Chama chake na pili ni kwa sababu ya biashara zake. Na kama alivyosema ni kweli basi suala la biashara zake lilikuwa juu zaidi. Rostam anasema “Athari kama hizo za kibiashara huingia ndani zaidi kuliko vichwa vya habari vya magazeti vinavyolenga kuchafuana, na athari hizo huwa kubwa zaidi kwa mtu kama mimi kwa sababu tofauti na wengine wengi hapa nchini, mimi ni mfanyabiashara wa kimataifa.”

  Na anamalizia hoja yake kwa kusema aliamua kujiuzulu kwa “dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu.” Kwa ufupi, Rostam hakujiuizulu kwa ajili ya maslahi ya Watanzania - wazo la kusababisha uchaguzi mdogo ambao utasababisha matumizi makubwa ya fedha, kulifanya jimbo la Igunga kutokuwa na mwakilishi wakati wa kipindi cha bajeti haviwezi kamwe kutafsriwa kuwa ni ‘maslahi ya taifa”

  Kama kweli Rostam aliona kuwa anahitaji kujishughulisha na biashara zake kwanini aliamua kurudisha fomu za kugombea Ubunge? Kwanini alikubali kusimama na Kikwete jukwaani na kuomba kura za wananchi ambao walimrudisha tena Bungeni kwa mara ya nne? Yote haya yanatufanya tubakie na jibu moja tu kwamba Rostam alijiuzulu kwa sababu ya maslahi ya Rostam. Maana kama angekuwa na maslahi mengine yoyote angeyasema au angekwepa kwa sababu maneno juu yake hayakuanza leo na hizo athari za kibiashara hazijaanza sasa.

  Lakini jambo la mwisho ambalo binafsi naamini linatudokeza zaidi ni kuwa Rostam hakumwomba radhi mtu yeyote. Alizungumza kama mhanga wa siasa mbaya na chafu. Sote tunajua kuelekea uchaguzi mkuu jinsi vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vyenye kuhusishwa naye vilivyoshiriki katika kuchafua watu mbalimbali. Wengi tunakumbuka kauli zake yeye mwenyewe alipojitokeza na kufanya siasa chafu alipowashambulia wale aliowaita “mafisadi nyangumi”. Lakini kote huko yeye alikuwa sahihi na hakuona kuwa ni siasa mbaya. Angekuwa na chembe ya uungwana angeliomba radhi taifa kwa sababu sehemu ya uchafu wa siasa zetu leo hii ni matokeo ya moja kwa moja ya yeye Rostam. Hakukiomba chama chake radhi, hakumwomba Rais radhi, hakuliomba Bunge radhi na zaidi sana hakuwaomba radhi wa Tanzania hasa kwa kuwa mshirika wa mambo ambayo yamekuwa misumari ya moto migongoni mwa Watanzania.

  Binafsi ninaamini, kuna hatua zaidi za kuchukuliwa:

  1. Kwanza ni kuvifunga vyombo vyake vyote vya habari ambavyo vimeshiriki katika kuwachafua watu wengine kama vile ambavyo amefanya yule mfanyabiashara maarufu Rupert Murdoch mmiliki wa vyombo kadhaa vya habari aliyelazimika kufunga gazeti maarufu duniani baada ya kukumbwa na kashfa.

  2. Kujipeleka yeye mwenyewe vyombo vya usalama na kuweka ushahidi wa kuhusika kwake na kashfa ya Kagoda na EPA kwa ujumla. Asipofanya hivyo DPP aanzishe uchunguzI mara moja na kama na yeye anajiuma meno basi aruhusu Mwendesha Mashtaka Huru chini ya Sheria ya Uendashaji Mashataka ya 2007 ili kuanzisha uchunguzI wa jumla wa kuhusika kwa Rostam na kashfa mbalimbali. Ni uchunguzI huru tu utakaoweza kumsafisha Rostam na tuhuma zote ili asibakie huko uraiani akiwa amezungukwa na wingu hili la kashfa. Kujiuzulu uongozi tu hakuondoi msururu wa tuhuma dhidi yake. Mtu akijitamba ana sabuni, haina maana kasema msafi.

  3. Chama cha Mapinduzi kimvue uanachama chini ya Kanuni za Maadili za CCM na Katiba ya CCM kwa “kukisababishia chama kashfa”. Kwa kadiri ya kwamba Rostam anaendelea kuwa mwana CCM, Chama cha Mapinduzi hakiwezi kudai kabisa kuwa kimejivua gamba. Watu hawakuwa na tatizo na Rostam kwa sababu alikuwa ni mbunge au mjumbe wa NEC, tatizo lao la msini linatokana na kuwa mwana CCM ambaye ameweza kutumia uwezo wake wa kila namna kushawishi siasa za CCM na hata za kitaifa. Yeye kawavulia gamba hadi mkiani, je NEC na CC wataweza kulimalizia?

  Kitu pekee ambacho naweza kumpongeza na kumshukuru Rostam kwa uamuzi wake wa kujiuzulu ni kuwa angalau sasa tumebakiwa na mtu mmoja Bungeni ambaye ana nguvu kuliko mwanasiasa mwingine yeyote nchini na ambaye natumaini naye atafuata mkumbo wa kuachia ngazi na huyo atafanya kweli kwa maslahi ya Taifa. Hapana, siyo Lowassa.

  Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
   
 2. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  JK nae amuige shoti ake Rost tamu
   
 3. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli hakujiuzulu kwa maslahi ya taifa bali kwa udhalimu na ufedhuli aliokuwa nao kujiuzulu ni bora kuliko kubakia madarakani! Tunashauri majuha wengi ktk serikali ya JK wafuate wamuzi huo kwani wanaletea taifa hasara kubwa mno! Hata mgonjwa wa Ukimwi akifa wanandugu hufura kwa hasara imepungua! Ni mtazamo
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu MMJ

  Mbele ya JK Rostam atakula raha zake ughaibuni
  Nguvu ya umma ndo inabidi itumike kumpeleka / kumfikisha kwnye vyombo vya usalama
   
 5. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Tanzania ni nchi pekee Duniani ambapo Usalama wa Taifa ni chombo cha Siasa na channel ya Ukwapuaji wa Mali za Taifa.Usishangae kuona TIS wakishiriki kumsafirishia Rostam fedha zake kwenda nje na kumficha mbele za macho ya Watz
   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  samweli sita ( mbunge )
   
 7. m

  mapambano JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubalia na Mwanakijiji 100%. Badala ya watu kushangilia kuanguka kwa huyu fisadi na kumlani kwa kuwabia, kuwatapeli watanzani, eti leo hii watu wanampongeza...R.A anatakiwa afikishwe kwenye mikono ya sheria sio kupongezwa hata kidogo.....he was never for the people, but for his dodge business deals...
   
 8. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndiyo,andrew chenge ( ubunge )
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  MMJ,

  Mapendekezo yako yote 3 hayatekelezeki aghalabu kwa Tz hii ya JK. Niko tayari kuweka dau lolote, na endapo yatatekelezwa niwe mhanga wa uamuzi wangu huo!

  DC
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Huyu fisadi anatakiwa arudishwe nchini ili tuelewane kwanza kuhusu tuhuma.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  sifaeli alikwambia wewe ni mbishi...ukasema hapana ...akakwambe basi twende bado ukagoma na kudai hadi akwambie wapi anakupeleka....akakwambia una kiburi bado uulikataa.....ndipo ukaamua kumfuata.... lile dubwana lilikuwa limeshika panga lenye makali kote kuwili na likatishia kukufata huku limenyanyua upanga wake....kwa woga na kujua yametimia uliamua kufunga macho na kukubali yote...lakini dubwal lile halikugusa hata unywele wako..na kwa woga ulianza kufumbua jicho la kulia taratiibu na kwa mara nyingine ukaiona nuru

  sifaeli alikuchukua hadi kule na alipofika ulifunguliwa mlango na kutahamaki hukumuona sifaeli .....sasa uko uso kwa uso na mtu mwingine....msikilize huyo nae atakwambia siri nzima lakini huyu hataweza kumfikia sifaeli aliyegusa personal life yako.....

  na hapo ndipo utajua kuwa una kazi kubwa ya kufanya juu ya nchi yako lakni pia huyo mtu atakwambia kila kitu juuya kina rostam hawa...lowasa nk..na gafla utajikuta hauko ufukweni mwa bahari ya hindi wa kando ya mto detroit
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  duh..!!! yamekuwa hayo tena?
   
 13. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [Kitu pekee ambacho naweza kumpongeza na kumshukuru Rostam kwa uamuzi wake wa kujiuzulu ni kuwa angalau sasa tumebakiwa na mtu mmoja Bungeni ambaye ana nguvu kuliko mwanasiasa mwingine yeyote nchini na ambaye natumaini naye atafuata mkumbo wa kuachia ngazi na huyo atafanya kweli kwa maslahi ya Taifa. Hapana, siyo Lowassa.

  Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com[/QUOTE]

  Ni huyohuyo!
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, Sheria haitachukuwa mkondo wake chini ya Kikwete, Kikwete mwenyewe ni mtuhumiwa No1
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Hii tusubirie kwenye jarida gani? Raia Mwema ama??
   
 16. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Nadhani wanaoshukuru kujiuzulu kwa Rostamu ubunge mantiki yao ni kuwa ilikuwa hatari sana kwa maslahi ya taifa kuendelea kuwa na mtu kama Rostam kwenye chombo muhimu kitaifa kama bunge. Katika hilo haijalishi amejiuzulu kwa nia njema au kwa maslahi binafsi lakini kuona jamaa aisye na huruma lakini mwenye uchu na fedha kama yule akiwa bado tu na mamlaka ya kuinfluence sheria za nchi, huku akiwa na access na viongozi wakuu wa kiserikali yaani tunakosa amani.
   
 17. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nimejaribu kuhusianisha haya yaliyoandikwa na Edson na hoja ywa Mwanakijiji nimeambulia patupu.
   
 18. A

  AbasMzeEgyptian JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 406
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  this is obsession now

  Jamaa kaondoka umeme bado hatuna

  sasa mshajua tatizo sio Rostam bali the entire system and political machine is rotten and rigged.


  how about cabinet nzima ikaondoka?

  haya mambo bila katiba mpya hayato tatulika trust me sasa hivi tunajaza maji kwenye gunia tuu
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  taifa hili linaloongozwa na ccm linatabia yua kuchukulia mambo kishabiki mno, yule mwizi alipaswa kuwa kule Keko akishugulikiwa na wababe wa jela nashangaa kuona yuko nje mpaka leo
   
 20. A

  AbasMzeEgyptian JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 406
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Tatizo sio Rostam, tatizo ni system nzima
   
Loading...