Rostam, Mkapa kuungana kampeni za CCM Igunga

kwa nini wanamuita gamba?
ina maana ccm wako tayari hata kutumia majambizi kushinda majimbo sio
na huyu Rostam alisema kahacha ccm hapa inakuwaje?.
/QUOTE]

Ninakubaliana mno na wewe! CCM kuliko wakose lile jimbo, wako tayari kuwatumia mafisadi wahonge wapiga kura! CCM ilikuwa na nafasi kubwa ya kujiondoa katika mitego na makwapa ya mafisadi (magamba) lakini kinara wao, Kiongozi Mkuu na Jemadari wa Taifa hili, ameshindwa na amekwenda kumpigia magoti Rostam amsaidie! Nafasi nzuri CCM inaipoteza kirahisi mno.

Hofu ya kupoteza jimbo mmoja, hofu ya kushindwa na upinzani umempa CCM kizungu zungu naam, na sasa tutaona mengine!

Habari niliyosoma Nipashe ya leo imenipa matumaini! Benjamin Mkapa na mgombea wa CCM wanatuhumiwa tayari kwa kuiangamiza nchi katika mikataba ya uchimbaji madini! Sinema nzuri iko mbioni kuonyesha! SAA YA UKOMBOZI NI SASA! Sikuwahi kuamini usemi huu, lakini naelekea huko sasa.

JF members mchana mwema na Idd Njema
 
Naomba jibu la swali hili, ni sababu zipi zinazoifanya CCM imtumie Mkapa kufungua kampeni Igunga?Je ni kwamba anapendwa Mkapa zaidi kuliko M/Kiti JK?Naomba nijibiwe tafadhali!!
 
Tuhuma zake wa2 wamezisahau ,kiwira,rada,ndege ya raisi, nyumba za serekali na tuhuma za m/kiti Jk bado mpya (waswahili wanasema Mavi yakale hayanuki)
 
Mkapa ni afadhali kuliko Jk. Mkapa aliendesha nchi kwa umakini mkubwa pamoja na baadhi ya kasoro zilizojitokeza. JK anaendesha nchi kisanii, hakubaliwi popote tz kwa hapa alipofikisha nchi. Kwanza ahadi za mwaka jana bado zinakumbukwa hata kugusa moja walau kuonesha kuwa zitatekelezwa hakuna. Atawaambia nini wana Igunga?
 
Tuhuma zake wa2 wamezisahau ,kiwira,rada,ndege ya raisi, nyumba za serekali na tuhuma za m/kiti Jk bado mpya (waswahili wanasema Mavi yakale hayanuki)

inawezekana ikawa kweli, lakini mi nahisi wameamua kumpa kazi ya kufanya, hajaosha jina na sura yake kwenye vyombo vya habari kitambo
 
Mkapa ni afadhali kuliko Jk. Mkapa aliendesha nchi kwa umakini mkubwa pamoja na baadhi ya kasoro zilizojitokeza. JK anaendesha nchi kisanii, hakubaliwi popote tz kwa hapa alipofikisha nchi. Kwanza ahadi za mwaka jana bado zinakumbukwa hata kugusa moja walau kuonesha kuwa zitatekelezwa hakuna. Atawaambia nini wana Igunga?

Nani afadhali? Mkapa nchi imeuzwa wakati wa uongozi wake. Nyumba za serikali ziliuzwa wakati wake, NBC iliuzwa wakati wake, EPA na madudu yake yalifanyika wakati wake, Viongozi kujilimbikizia mali, rasilimali za nchi, mikataba hatari kwa ustawi wa nchi yetu yote ilisainiwa na serikali yake.

Niungane na Mthuya kwamba, CCM inaamini wananchi wameshasahau UPUUZI wa Mkapa, lakini naamini ndo naye atalipuliwa vilivyo kuwa yeye ni mwizi na kalihasarisha taifa.
 
Hapa msema kweli ndiyo ninaposhindwa kuelewa.Ni gamba lilitakiwa kutoka, Limeotoka na sasa linatakiwa.Kwani kama mliona lina umuhimu kwa Chama kama kawaida yenu si mngeliacha?? Sasa sijui ni akili gani inatumika kumtumia Gamba Rostam kupiga debe kutafuta Gamba lingine.Huku ni kukosa sera na kutokuwa na Fikra endelevu. WADAU MWAONA JE JAMBO HILI??
 
Wanajua hawezi kukataa, naye pia anajua hana namna ya kukataa. Bila shaka watakuwa wamemwambia kuwa akikataa wanamshughulikia yale madhambi yake ambayo ni mengi tu. CCM wanajua namna ya kuwekana sawa na umiliki wake wa vyombo vya dola inavitumia vixuri.... kwa sasa anyway.
 
Natabiri Mkapa hatakanyaga igunga baada ya vitisho kuanza kutolewa leo kuwa watu wataanika maovu yake yote. Na kwa kuwa Mkapa hapendi malumbano huwa anachagua kukaa kimya hatakubali kwenda kuanikwa hadharani kwa wana Igunga. Halafu hizi siasa za akija fulani ndio kampeni zitakuwa nzuri tuziache, tushobokee sera kwani tumeishadanganywa sana. Hivi wana Igunga hata akija Rostam kukampeni mumchague mtu ambaye hamumpendi na mkazidi kuwa maskini atawasaidia nini? Kama anataka kuwasaidia angeendelea kuwa mbunge, na kwa kuwa amewatosa na nyie mtoseni?
 
Kwanza siamini iwapo RA huwa anafanya kampeni -- kwa maana ya mikutano ya majukwaani etc etc -- na kama anafanya basi ni michache mno. Yeye zaidi hutumia pesa -- yaani hongo -- kuwapa wananchi, au watu wanaosimamia uchaguzi, yaani ma-returning officers na wasimamizi wao vituoni -- na hapa CDM lazima wawe makini sana. Naamini RA bila ya hivyo asingeweza kushinda Igunga uchaguzi wowote ule.

Lakini hata hivyo hali ya kisiasa ya nchi imebadilika sana tangu uchaguzi uliopita kutokana na madudu ya CCM kuibuka kila kukicha. Tunaweza kusema pendulum ya kisiasa ime-swing sana upande wa CDM.
 
Anuwezo zaidi ya hawa walipo kwani pia anaaminika siyo hawa wamejaa uongo kila sehemu ya mwili wao. Wanajaribu lbda yeye anaweza okoa jahazi wao limeshawashinda ndio maana hawatatia mguu Igunga
 
hawa CCM wanajaribu kuficha arufu ya chupi chafu kwa kuvaa Suruali iliyotunzwa siku nyingi sandukuni wakidhani itaonekana mpya...wamesahau kukaa sandukuni tu inanuka uvundo. sasa wanachanganya harufu ya boxer vumbi na vazi zee wakihisi litaonekana jipya, maskin ndo wametuongezea harufu ya vyote Chupi +old trouser...jibu wanalo wana igunga nini wanahisi...Lets wait
 
Hata mi naamini Mkapa wont show up there! Pamoja na mafinyango yoyote bado Mkapa ni Presidaa aliyekuwa imara na ambaye ndani ya moyo wake siamini anaridhia mwenendo wa mambo sasa serikalini na ndani ya sisiemu. Sidhani kweli atakubaliana ofa hiyo kwanda Igunga
 
Hata mi naamini Mkapa wont show up there! Pamoja na mafinyango yoyote bado Mkapa ni Presidaa aliyekuwa imara na ambaye ndani ya moyo wake siamini anaridhia mwenendo wa mambo sasa serikalini na ndani ya sisiemu. Sidhani kweli atakubaliana ofa hiyo kwanda Igunga

Nami pia naona hatakwenda kule -- itakuwa balaa -- yaani badala ya kumkampenia mgombea wao time yao kubwa kubwa itakuwa kujibu tuhuma za ufisadi dhidi yake binafsi.
 
Pia wampeleke na Lowasa and Chenge.... so mkapa itabidi aseme Rost tamu siya fisadi duh magamba bana
Mkuu hiyo rangi kama ndivyo basi LA anaweza kugombea urai 2015 coz king maker anahusika lkn when you read btn the line ccm has finally reached an end!!!!! its obvious that, kama wana busara wakubaliane na Nape kwamba miaka minne aliyoacha RA Igunga isiwe ktk himaya ya ccm watumie nafasi hiyo ku-iron out their differences na kujenga chama kwa 2015 wakitegemea nguvu ya genge la mafisadi hilo ni timesetbom matokeo yake Dr Kafumu atafumuliwa kweli huko Igunga hiyo ndo rise and fall of Ccm kumbika kwamba hakuna kulala na kura hakuna kuiba kura vilevile Luhanjo/Jairo saga ndo cd inayouzika take note!!!
Mimimsimo ktk shimo!!!!!!
 
kwa kwel limeka vibaya kwa sababu wapinzani watapata cha kuongea zaidi juu ya huyu gamba ni bora asingekuwepo wapinzani wasinge zungumzia habari zake lakin yupo inamaana atakuwa anawashambulia wapinzani ss swali wapinzani watakubali?
 
Hata mi naamini Mkapa wont show up there! Pamoja na mafinyango yoyote bado Mkapa ni Presidaa aliyekuwa imara na ambaye ndani ya moyo wake siamini anaridhia mwenendo wa mambo sasa serikalini na ndani ya sisiemu. Sidhani kweli atakubaliana ofa hiyo kwanda Igunga
<br />
<br />
Hata mim pia naamin he wont show up there cause ata hotuba zake haungi mkono mambo yalivyo sasa
 
Back
Top Bottom