Rostam, Mkapa kuungana kampeni za CCM Igunga

Huku ni kumdhalilisha Mzee huyu, inamaana hadhi yake imeshuka mpaka kufikia kufanana na Jimbo moja badala ya nchi? Jamani aheshimike huyo mzeee.[/QUOTE]

Hello Dullo,

Hapo kwenye nyekundu nimecheka yaani sina mbavu! Kwamba jamaa(Mkapa) sasa analinganishwa na Kiwilaya kimoja cha Igunga wakti alikuwa Rais wa nchi??Teh.teh.tehe,uuuwwiiiiiiiii! Na siyo wilaya kuwa na hadhi ya wilaya tu,maana Kampeni si ataenda mpaka vijijini na vitongojini akipiga kelele za Kampeni?? Kwa hiyo hadhi yake itashuka mpaka Balozi wa nyumba 10! What a shame kwa mtu aliyekuwa Presida???
 
why, kikao kimefanyika ikulu, ambako tunafahamu kuwa ikulu si mali ya chama ni ya serikari, je ni fedha ipi imetumika kuendesha kikao, au serikari imeamua kukidhamini.

Unauliza majibu mwanawane?

Chama Cha Magamba c ndo chama Twawala? Ikulu ni yao maana Mwenyekiti wao Kiwete yuko pale. Kwa taarifa yako tu ni kwamba kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana 2010, Ikulu ndiyo ililipia GHARAMA ZOTE ZA MABANGO YA MATANGAZO YA KAMPENI ZA KIWETE!!!

Hao ndiyo Chama Cha Magamba bwana. Hawajali,hawaoni aibu,hawafauati sheria wala taratibu za nchi. Wao ndiyo kila kitu wakiamua leo wameamua.
Naamini kwa asilimia 100 IGUNGA CCM HAWASHINDI HATA IWEJE.Na kama ikitokea wakashinda basi watakuwa wamefanya kati ya haya yafuatayo:
  1. KUIBA KURA.
  2. KUCHAKACHUA MATOKEO.
  3. KUWATISHA WAFUASI WA VYAMA VINGINE WASIJITOKEZE SIKU YA KUPIGA KURA.
  4. KUTUMIA MABAVU YA POLISI WA KAWAIDA NA FFU KWA KUWAPIGA MABOMU WAPINZANI.
Ni bora CCM wakajitoa kwenye kinyang'anyiro hiki wakawaachia CDM na CUF wakagombea hilo jimbo.
 
Kweli kuwa mwanasiasa ni sawa na kubwia unga. Huyu kakaa kimya kwa muda sasa hamu ya kupiga saisa imemuingia tena. Nilikuwa nimesahau hivi suala la kumuondolea kinga ya kushitakiwa limeishia wapi?
 
Kweli kuwa mwanasiasa ni sawa na kubwia unga. Huyu kakaa kimya kwa muda sasa hamu ya kupiga saisa imemuingia tena. Nilikuwa nimesahau hivi suala la kumuondolea kinga ya kushitakiwa limeishia wapi? 
 
Nadhani atakuwa ni msaada mkubwa sana kwa CCM. Huyu mzee huwa haogopi mtu yeyote, nakumbuka alivyodiriki kuwaita Chadema KOKOTO pale Jangwani. Chadema walilalamika sana lakini jamaa hata hakuogopa.
<br />
<br />
gadafi aliwaita rebels crococh. Saiz mende wameangusha ka
 
Yes Good! Kukodi majeshi inaruhusiwa hasa kama aneyekodiwa anakubali kufanya hiyo kazi kwa moyo mkunjuf, safi CCM ila mnakosea kitu kimoja tu!

Kwanini Msimuombe akae pale Ikulu kwa hii miaka iliyobaki ya Kikwete? Kwanini msimtumie kwemye mambo ya maana ya kujenga nchni badala kumtumia kwenye upuuzi kama huo ambao mmeuleta wenyewe bila faida yoyote? Mi sioni faida yoyote ya RA kujiuzuru naona ni hasara tu imetuingiza katika gharama za uchaguzi wakati hata makosa aliyofanya hayashughulikiwi na wala hayaongelewi tena.
 
Ngoma inogile Mzee Mkapa kuongoza kampeni za CCM.

Namuonea huruma mzee wa uwazi na ukweli....mabomu yatakayo muangamiza ni haya hapa na CDM tutayatumia sana kwasasa,ni bora hasiende...
  1. Ununuzi wa ndege ya raisi,tena na kejeli juu..."Ni bora watanzania wale nyasi ndege ya raisi ipatikane..."
  2. Ununuzi wa mgodi wa Kiwira mbeya...yeye na rafiki zake tena kwa bei chee
  3. Umiliki wa ANBEN mbona kimya sana.....?
  4. Benki M ndio inaendelea kutesa yeye kakaa kimya........
Kwa haya machache tu,yaliyo wazi najua Dr wa ukweli atakuwanayo mengi zaidi sisi vijana wake ndio tunakujakuja katika mambo haya ya investigation...kwa kawaida sisi CDM motto wetu ni kuwa... no research no right to say...
 
Tuesday, 30 August 2011

ALIYEKUWA Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ni miongoni mwa makada watakaotumiwa na CCM katika kampeni za kumsaka mrithi wake katika jimbo hilo.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) kilichokutana juzi, Ikulu Dar es Salaam zinasema Rostam amepangwa kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za CCM zitakaofanywa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Septemba 10, mwaka huu.

"Labda ratiba ibadilike, lakini ni kweli Rostam amepangwa kwamba ataambatana na Mzee Mkapa kwenda Igunga na yeye atabaki huko kama wiki moja hivi kusaidia kampeni hizo," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu hiyo ya CCM.

Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema Rostam amepangiwa kwenda Igunga mara tatu: "Baada ya hapo atarudi tena katikati ya kampeni na pia atarudi tena wakati wa hitimisho."

Uamuzi wa CCM kumtumia Rostam katika kampeni zake za Igunga unatafsiriwa kuwa hatua ya kutafuta kuungwa mkono na wakazi wa jimbo hilo ambao "walikasirishwa" na kitendo cha mbunge wao huyo kujiuzulu kwa kile alichokiita "siasa chafu."

CCM kinakabiliwa na makovu huko Igunga yaliyotokana na kujiuzulu kwa Rostam ambaye wakati akitangaza kujiuzulu alitamka bayana kwamba uamuzi wake huo ulitokana pamoja na mambo mengine, wanasiasa uchwara wanaoendesha siasa za kupakana matope baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kutangaza mpango wa kujivua gamba.

"Nimepata msukumo wa kuamua kuachia nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama, nikianzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nikiuwakilisha Mkoa wa Tabora na hii ya ubunge wa Igunga ambazo kama si kwa baraka za chama changu, nisingelikuwa nazo," alisema Rostam siku alipotangaza kujiuzulu na kuongeza:

"Napenda kuliweka hili sawasawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM, haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu."

Rostam sasa anatarajiwa kushiriki kampeni hizo, akimpigia debe mgombea wa CCM, Dk Dalaly Peter Kafumu aliyepitishwa na CC ya chama hicho juzi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu ushiriki wa Rostamu katika kampeni za Igunga alisema: "Rostam ni mwanachama wa CCM na chama kimetoa mwaliko kwa wanachama wake kushiriki kampeni hizi, hivyo hilo labda ajibu mwenyewe lakini kama mwanachama ana haki ya kushiriki."

"Labda niseme hivi, ukiachilia mbali watu kama Mzee Mkapa ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi, hatukupeleka mwaliko kwa mtu mmoja mmoja, ila tuliwaalika wanachama wetu kusaidia kampeni hizi, kwa hiyo Rostam akiwa mwana CCM ana haki ya kukipigia kampeni chama chake."

Nape pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), John Chiligati walitajwa na Rostam wakati akijiuzulu kwamba ndiyo waliopotosha dhana ya kujivua gamba kinyume cha uamuzi wa NEC.

"Walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuzi wa kuwapa siku 90 wale walioitwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyo watafukuzwa na chama," alisema Rostam.

Hata hivyo, Rostam hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwani alipopigiwa simu yake ya kiganjani hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi alijibu kwa kifupi: "in a meeting, baadaye" akimaanisha kwamba alikuwa kwenye mkutano.

Juzi, Nape akitangaza uteuzi wa Dk Kafumua alisema: "Katika kufanikisha kampeni za CCM wanachama waliowania kuteuliwa katika nafasi hiyo wameahidi kuwa watashiriki kikamilifu katika kampeni hizo."

Alisema hata wagombea wengine wa chama hicho katika kura za maoni wameahidi kuwa watamuunga mkono Dk Kafumu ambaye aliibuka mshindi kwa kupata kura 588. Hao ni pamoja na aliyemfuatia kwa karibu, Jafari Omari aliyepata 193 na Shams Brahamu aliyepata kura 38. Katika uchauguzi huo wanachama 13 wa CCM waliomba nafasi hiyo.

Nape alisema CCM kitashinda kwa kuwa kina mizizi imara iliyojikita katika vitongoji vyote vya jimbo hilo, tofauti na vyama vya upinzani... "CCM ipo Igunga wakati wote (wa uchaguzi na usio wa uchaguzi). Vyama vya upinzani huonekana kule wakati wa uchaguzi."

CCM waunda timu nne
Katika kuhakikisha kinashinda uchaguzi huo mdogo, CCM Wilaya ya Igunga kimeunda timu nne maalumu, ikiwamo ya wafanyabiashara maarufu watakaohakikisha kwamba mgombea wa chama hicho, Dk Kafumu anashinda.

Hatua ya kuunda timu hizo inatokana na chama hicho ngazi ya taifa kutangaza kuwa majukumu yote ya kupanga na kuendesha kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu, zitasimamiwa na CCM Wilaya ya Igunga.

Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga, Neema Adam alisema jana kuwa tayari wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya vyama vitano vya upinzani vilivyosimamisha wagombea.

"Kimsingi uchaguzi unasimamiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya. Hivyo wajumbe wote wa kamati hiyo wataratibu shughuli zote za kampeni," alisema Neema lakini akidokeza kuwa kamati hiyo itasaidiana na timu nyingine tatu.

"Mbali na kamati hiyo, wafanyabiashara maarufu 20 hapa Igunga, wameunda timu itakayosaidiana na wanachama wa CCM kufanikisha kampeni hizo. Vilevile kila tarafa ina timu ya watu wanne na kila kata watu 10. Kwa hivyo ukiangalia utaona kuwa tumejipanga vizuri katika kuhakikisha tunapata ushindi."

Wagombe wengine ni Joseph Kashindye wa Chadema, Moses Edward (TLP) na John Maguma wa SAU na Leonard Mahona wa CUF. Uchukuaji fomu ulimeanza Agosti 24 na unatarajiwa kukamilika Septemba 6, mwaka huu.

CUF nayo yatamba
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema wamejipanga kikamilifu kukabiliana na CCM kwenye kampeni zijazo.Alisema wakati wa kampeni chama chake kitalipua siri zilizofichuka dhidi ya kiongozi yeyote wa CCM atakayefika Igunga, akiwamo Rais Mstaafu, Mkapa.

Katika kampeni hizo, Mtatiro alisema wataweka hadharani sababu ambazo wapiga kura wanapaswa kuzizingatia na kutoichagua CCM na badala yake kumchagua mgombea wa CUF.

Alisisitiza kuwa CCM wajiandae kukabiliana na maswali mengi ambayo watashindwa kuyajibu mbele ya wakazi wa Igunga.

Source: Mwanachi
 
Sikuwahi kuamini macho yangu wala masikio yangu kwamba eti CCM imempiga stop katibu mwenezi wake kushiriki katika kampeini za Igunga. wanajamii hivi hadithi hii ni kweli? siamini kabisa kwamba Chama hiki kimepoteza umakini kiasi hicho wandugu.

Kama hadithi hii ni kweli na kwamba kuonekana kwa Nnauye Igunga kutakigawa chama sasa najiuliza hoja ipi kwa ccm kama chama inauzito ni kuwaogopa mafisadi, nguvu na mvuto wao kwenye chama na kuruhusu ustawi wa kisiasa walioujenga katika njia ya kishetani ushamiri au ni kutekeleza dhana ya kujivua gamba kwa haraka sasa na kwa garama ya chama kupata makovu ambayo yanaweza kuponyeka kabla ya 2015.

Nani aliwahi kuwambia CCM kuwa maamuzi mazuri kwa niaba ya walio wengi yatakosa kuwagusa wachache ambao ni wanufaikaji wa mfumo huo haramu. Nani amewambia viongozi wa CCM kuwa tiba ya ugonjwa mwilini haiwezi kuleta madhara kidogo mwilini? unawezaje kulima shamba ukapata mavuno mazuri bila kutokwa na jasho na maumivu ya uchovu. Unawezaje kukijenga chama bora cha siasa ukawa rafiki wa kila mtu? unawezaje kusimamia serikali itoe huduma iliyobora na usiwadhuru wale wenye dhamana ya kutoa huduma iliyobora kwa kusimamia maadili katika njia iliyotukuka.

Nilidhani na pia nataka kusisitiza kuwa huko nyuma niliwahi kuuliza hivi agenda ya CCM igunga ni nini hasa? katika hili nilitaka mtu mmoja kwa ushupavu ndani ya CCM aseme ajenda yetu ni kwa wanachama waliochafuka kisiasa na ambao uchafu wao unakiadhiri chama lazima waachie ngazi na kazi hii iongozwe na yuleyule katibu mwenezi. Hii ndio agenda iliyofanya jimbo hilo liwe wazi vinginevyo hii double standard imetufanya tuliowengi sasa tuanze kuwaasi kwa spidi ya rocket. Wengi hatuoni nini hasa msimamo wa Chama katika ufisadi? kwamba CCM ya leo inaamini katika ushindi kuliko njia na hoja iliyowapatia ushindi? Chadema mnaliona hilo? huo upenyo ni fursa tosha ya kukiangamiza Chama Cha Mapinduzi.

Chama hiki kinahubiri kujivua gamba lakini kinasema agenda hii itahubiliwa tu pale ambapo haiwezi kuleta madhara katika chama. Hivi jimbo la Igunga au bariadi na kwengineko linathamani gani mbele ya haki ya watanzania na msimamo wa chama wa kuondoa virusi katika uendeshaji wa chama na serikali yake

Sitaki kuona wala kushuhudia chama hiki kikigeuka nyuma kwa kuogopa kivuli cha mafisadi na jamaa zao, kelele zao na vitisho vyao haviwezi kushinda njia ya haki. Ila kwa sasa naona njia nyeupe kuelekea kusiko mwanga na tofauti ya chama na wananchama wake inazidi kukua kila siku kwa sababu hakuna agenda ya watanzania kwa vitendo ndani ya CCM hilo tone kidogo tunaloliona sasa ni kwa sababu CDM inawapumlia mlangoni na kisogoni


Mungu Ibariki Tanzania

Mungu wabariki wanaigunga

Mungu wajalie wanaigunga nguvu za ziada kuua ufisadi

Mungu wabariki wanajamii waendelee kutoa mchango bila kujali nani atanufaika na mchango huo wa mawazo
 
Pengine tusi kubwa kwa wana-Igunga na wa-Tanzania wote wenye uchungu na nchi yao, siyo usongo wa kaulimbiu ya CCM "Tumethubutu, Tumeweza, Tunasonga Mbele", bali ni ukwasi wa kumchagua Ben W. Mkapa kufungua na kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga.

Ikumbukwe kuwa ugomvi mkubwa wa Rostam na akina JK, Msekwa, Nape, Mukama, Chiligati, etc ni kuhusu tuhuma za UFISADI na Kujivua gamba kwa Rostam na wenzie. Aghalabu, mojawapo ya tuhuma hizo ni wizi wa hela za EPA, kupitia Kagoda Agric kampuni ya Rostam, na kujumlisha na Richmond/Dowans, katika masuala ya utapeli wa umeme.

Sehemu zote hizo mbili Mkapa ana mikono na miguu pia. Nitafafanua.

Ni wakati wa awamu ya Mkapa, ndiyo wizi wa EPA ulifanyika na kupata baraka zote za Ikulu. Mkapa akiwa Raisi na Mwenyekiti wa CCM, aliafiki Mweka Hazina wake Rostam (Mweka Hazina msaidizi Salome Mbatia) kukwapua mabilioni ya hela za EPA, bila bughudha. Wizi huo ulifanyika huku mteule mwingine wa Mkapa, Gavana Balali wa BOT, akishiriki katika hatua zote. Takribani miaka 7 baadaye, Mkapa anaenda Igunga kutetea kiti cha ubunge kilichoachwa wazi na mwizi mwenzie.


Mkapa pia akiwa Rais aliamua, kwa mtutu wa bunduki, kuhamisha uendeshaji wote wa TANESCO kwenda Net Solutions Group ya South Africa. Mojawapo ya maamuzi ya Net Group ni kudumaza huduma za umeme, kufisha upanuzi wa vyanzo vya umeme, ili kujenga mazingira ya Kiwira kuingia katika uzalishaji umeme, hatua ambazo zilipelekea kuruhusiwa kampuni za briefcase kama Richmond na hatimaye Dowans, kuingia katika biashara ya umeme pia. Na kwa njia hiyo pia, Rostam akajikuta tena katika faida ya maamuzi ya Mkapa. Na tena takribani miaka 7 baadaye, Mkapa anaenda Igunga kutetea kiti cha ubunge kilichoachwa wazi na mwizi mwenzie.

Kamati Kuu (CC) ya CCM kama kweli ilikaa na kufikiri (nina mashaka na hilo, kwani kufikiri si jadi yao), basi watakua na jibu la tusi hili kwa wana-Igunga na wa-Tanzania wote wapinga ufisadi, na wapenda maendeleo ya dhati.

Na nadhani hapo ndiyo kaulimbiu ya CCM inapoonyesha maana yake: TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNASONGA MBELE.........na wanaweza kumalizia........ MWENYE NGUDU AJINYONGE.
 
Wako wapi wale walikuwa wanamkumbuka Mkapa, huyo sasa kaibukia Igunga!<br />
Mfuateni mkanywe nae Bia na Nyama choma
<br />
<br />
utawaweza wanafiki wa humu ooh bora mkapa angekuwepo now wanampiga madongo.phew...
 
kwa nini wanamuita gamba?
ina maana ccm wako tayari hata kutumia majambizi kushinda majimbo sio
na huyu Rostam alisema kahacha ccm hapa inakuwaje?
huu ni mtego mwingine ccm wanaingia kichwa kichwa, sasa wanatamaa na igunga hakuna kufikiria baadaye
hii cost yake ni 2015 maana wananchi watakua wameshajua kwamba hakuna cha magamba wa kuvua magamba ni mchezo wa kuigiza

anyway sidhani kama watu wanapiga kura kuchagua rostam this time ni kafumu, na hakuna wizi wa kura
 
hapo ndipo wanapojimaliza mwache aende Igunga ndio watajua joto ya jiwe hao. Magamba imebaki makaratasi tu na si chama.
 
Bila kuwa mnafiki kamwe hauwezi kuwa mwanachama wa CCM,hivi kweli rostam anaweza kwenda igunga kupiga kampeni!!?Tusubiri
 
Back
Top Bottom