Rostam Aziz kuvuliwa Uraia?


Nawewe jaribu kuwa mwelewa! Huwezi kulinganisha uraia wa EL na rostam, nadhani hujafikiria kidogo. Huyu rostam ana uraia wa nchi mbili kitu ambacho ni kosa kisheria. Sasa kwa sababu na yeye na fisadi na anaonekana kutudharau basi tutumie njia ya uraia kumfukuza nchini. EL tutamshughulikia taratibu kwa sababu ni morani wa hapa hapa.
 
Tuacheni ushabiki. RA amefanikiwa sana, Mi ninaona anafaa hata kuiongoza nchi hii. Kama umefanikwa binafsi hata nchi unaweza kuifanikisha.

Kwa kweli mimi ninampongeza RA
 
kumbukeni kuwa hata Mh. Mwakyembe mbunge wa kyela wakati akijibu tuhuma alizotungiwa na kina rostam, alisema kuna watu wana uraia wa nchi mbili, akiwa anamlenga rostam, msomin kama mwakyembe hawezi kuropoka hivi hivi

Mwakyeme alisema: Wana uraia wa nchi tatu. Kwa lugha rahisi ni kwamba; RA ni raia wa Tanzania, Iran na Canada
 
KWA MASLAHI YA WADANGANYIKA...Jenerali Ulimwengu rudia makala hii

Ni makala uliyoiandika mwaka 2005 kuelekea uchaguzi. Ilizungumzia Sheria na Taratibu mbovu katika kusimamia taratibu za kupatika wagombea na matumizi ya fedha zisizo na kikomo wala maelezo. Ulikuwa ukitoa onyo kwa Serikali (Msajiri wa Vyama na NEC).

Sikumbumbuki jina na toleo la makala ila ulisema kwa kuruhusu matumizi ya pesa yasiyo na mipaka, atakuja mgeni asiye na uchungu bali uchu na rasilimali za nchi hii. Akifahamu kuwa ili mambo yake yaende vizuri lazima awe na ushawishi kwenye serikali. Na mojawapo ya mhimili ya ushawishi ni Bunge. Atauliza hivi: "Ni pilau ngapi, kofia ngapi na kanga ngapi zinahitajika kumpitisha mgombea kuwa Mbunge Na thamani yake ni Shilingi ngapi" watamjibu jimbo moja ni kama 100M. Kisha atauliza tena nahitaji wabunge wangapi kupitisha jambo lolote bungeni, watamjibu. Atachagua majimbo muhimu kwake na kusimika Wagombea kwa kuwafadhili. Matokeo yake mtakuwa na Bunge linalowajibika kwa Mgeni. Hii ni nukuu isiyo rasmi.

Mtazamo na maoni yangu:
Jenerali alikuwa anafahamu mbinu za wageni kuvamia mihimili ya nchi yetu. Yawezekana pia alikuwa na clue jinsi RAis alivyokuwa anajiandalia Mhimili katika nchi ya WADANGANYIKA kupitia ufadhili wa wagombea wa CCM. Alipiga kelele kadri awezavyo pasipo mafanikio. Sasa ishakuwa aibu ya kizazi, tumeacha kuchukua hatua madhubuti mapema.

Quiz:
Kama Bwana Harusi alishauriwa wakati wa ujenzi; kuwa mapazia pekee bila milango ya mbao au chuma nyumba haiwezi kuwa salama. Akaambiwa aweke mlango hasa chumbani kwake. Akakawia kuchukua hatua wakati wa ujenzi akaoa na kuhamia bila milango ya mbao wala chuma. Jirani akaleta taarifa juu ya waporaji wanaovamia kutoka vijiji vya mbali kuja kuiba na kulawiti kina mama na dada zao, bado mwenye nyumba akaziba masikio.

Ikitokea waporaji wakatembelea nyumbani kwake kwa nia njema labda kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Wakati wanazungusha macho wakamwona mkewe (Bi Harusi) yuko uchi chumbani. Kutokana na tabia yao ya kuiba na kulawiti, wakawashawishika na kumlawiti Bi Harusi. Maana wameisha vuruga, wakabaini hakutakuwa na mahusiano mazuri anymore kufanya Biashara. Hivyo basi wakamua wapore na kuondoka. Hili tendo la kulawiti limefanyka siku na saa mkeo (Bi Harusi) yuko kwenye "PEAK" hivyo yawezekana akawa amepata mimba.

Wewe kama Bwana wa Mgore, utafanyaje au utachukua hatua gani?
 

Magezi,

Uraia wa nchi mbili na Ufisadi ni uvunjaji wa sheria?

El na Ra ni wavunja sheria?

Nawewe hapo hujaelewa?

Ahsante
 
kuna copy and paste journalism tu...
 

Just like Obama says below....May be WaTz hatujataabika vya kutosha. But one day we will have to fight, tukiwatayari kwa lolote.
 

Kama ni kweli na aliweza kupitishwa kuwa Mbuge bila umakini wowote, I wonder kama Nchi hii ina viongozi makini.

Na zaidi bado najiuliza Watanzania tunayo matatizo gani hasa mpaka tunashindwa kutyatambua haya kwa nguvu zetu zote?
 
Hili lililomkuta Mtikila hayupo pekeyake, wapo wengi mno, Mtikila kaamua kukaa kimya lakini kuna wengine (Manyerere Jacton) wapo majukwaani kabisa kumtetea huyo jamaa kwa sababu wameshakula cha watu


(Manyerere Jacton) - Hata yeye naye kala? mbona namwonaga kama mwaminifu kwa taifa. Astakafirullah!
 
OBSESSION inatisha sana

GT mkuu mbona siku nyingine una toa post zinazo kucontradict? Una sema ushabiki je wewe unavyo mtaja Mengi kwenye kila mjadala unao husu maovu ya wengine tuitejee? Si na wewe basi una obssesion hiyo hiyounayo singizia wengine? Na pia hakuna thread inayo msema vibaya Mengi ukasema ni obssesion. Wewe upo obsessed na kumsema Mengi wengine wako obsessed kumsema RA. Toa tu hoja kupingana au kukubaliana na mada mkuu.
 
I keep on watching
najua bado mengi yatakuja kutufumbua macho.
Ahsante Mwanakijiji kwa kutuwekea jamvini hii dossier.

Sijui nchi yetu ikoje walah
 
Kama ni kweli na aliweza kupitishwa kuwa Mbuge bila umakini wowote, I wonder kama Nchi hii ina viongozi makini.

Na zaidi bado najiuliza Watanzania tunayo matatizo gani hasa mpaka tunashindwa kutyatambua haya kwa nguvu zetu zote?

Pale Idara ya Vizazi na vifo yazamani ya mama kaisi, Ilikuwa na utaratibu mbovu sana uliojazwa Rushwa, Ilkuwa pale nyuma ya Bilicanas, Pale nje ya Billicanas kulikuwa na viofisi vya kitapeli vingi sana nazani vipo mpaka leo, Hivi viofisi vilikuwa vinaendesha shughuli nyingi za kizushi, Mtu alikuwa anatoka Congo leo anakaa mwezi baada ya mwezi unamwona na passport ya Tanzania ukimwuliza anasema Billicanas,Hizi hati za kuzaliwa nyuma ya Billicanas zilikuwa zinachukua masaa tu kupataikana, The same Idara ya passport ilkuwa imejaa rushwa sana, Kwa mtu mwenye pesa ilikuwa haichukui mda,Inasikitisha sana.

Lakini the big question sio swala la uraia wa Rostam, Hata tukifahamu haitatusaidia, Kitakachofanyika tutamfunga maisha Tanzania ili hata huko alikohamishia mali zake asiende kuzifaidi, Huyu si wa kuachia maana ana mamuluki wengi sana dawa ni kumfunga pamoja na mamuluki wake wote.

Lengo la posting ya Mwanakijiji sizani ilikuwa ni kuhoji uraia wa Rostam rather ni kumkumbusha kwamba tunamfahamu vizuri sana na akae chonjo maana tutamumaliza soon.
 
wakuu wa kaya nawezaje kupata nakala ya cheche no 40. nimejaribu kuitafuta bila mafanikio. niwezesheni wazee.

asante mwanakijiji kwa jitihada zako. we really need changes,
Toleo la 40 hilo hapo.
 
Kwanini Rostam hakufungua mashtaka dhidi ya Mtikila? Kwanini serikali haikumkemea Mtikila n..k )? [/QUOTE]

Maswali magumu ambayo shurti wana JF wapate majibu yake
 
Kama ni kweli na aliweza kupitishwa kuwa Mbuge bila umakini wowote, I wonder kama Nchi hii ina viongozi makini

Kwannini asifanyiwe kama Generali Ulimwengu ambaye tangu utoto wake kama sio kuzaliwa alikuwa Tanzania masikini? Au viongozi wetu wana mpango wa kukimbilia Iran baada ya 'ku-retire'?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…