Rostam Aziz: Dr. Slaa hatari kwa Taifa............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam Aziz: Dr. Slaa hatari kwa Taifa...............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Mmiliki wa gazeti la Rai; Rostam Aziz, ambaye ndiye wengi tunaamini ni mwakilishi wa JK kwenye kashfa ya DOWANS ambayo isipovaliwa njuga italigharimu taifa zaidi ya bilioni 100 ametumia nafasi yake tajwa visivyo alipotumia kumchafua Dr. Slaa na kumwita ni hatari kwa taifa wakati sisi tunaamini yeye Rostam Aziz ndiye hatari kwa usalama wa taifa hili.................................kwa kutuingiza mkenge ili tulipe ufisadi na hivyo kukwamisha jitihada za taifa hili kujitoa kwenye lindi la umasikini............

  Aidha Rostam Aziz alidai ya kuwa Dr. Slaa alimzushia kushiriki kikao cha mwanza kilichopanga uchakachuaji wa kura wakati yeye alikuwa safarini Afrika ya Kusini safari ambayo hadi leo Rostam Aziz kashindwa kututhibitishia kuwa kwenye tarehe hizo kweli hakuwa nchini baada ya hata kushindwa kuonyesha kwenye pasi yake ya kusafiria mihuri na viza ya kuingia na kutoka kule Afrika ya Kusini.


  Rostam Aziz pia anadai ya kuwa kwa mara nyingine Dr. Slaa amemzushia safari ya kwenda Marekani kwa ajili ya kupanga mipango ya kulipora Taifa hili mabilioni ya fedha kupitia DOWANS huku akishirikiana kwa karibu na swahiba wake JK safari ambayo Rostam Aziz anadai hakwenda..........kwani kwenye tarehe hizo alikuwa humu humu nchini..........Lakini kinyume na awali ambapo Rostam Aziz alionyesha baadhi ya ushahidi ambao uliongeza utata juu ya utetezi wake safari hii hakutoa ushahidi wowote ule kuthibitisha madai yake katika mazingira yanayothibitisha zaidi ya kuwa pengine hata safari hii anasema uongo tu...............Huenda safari hiyo ya marekani alikwenda na sasa anajishauashaua tu..............kujaribu kufunika ukweli.................Upo ushahidi ambao ulitolewa na Tanesco kwa msuluhishi ya kuwa Rostam Aziz ni mwasisi wa kashfa ya DOWANS.......................kama ushahidi huu uliotolewa na tanesco kwenye uamuzi wa DOWANS unavyojieleza..........


  [​IMG]


  Soma ukurasa wa 121 wa DOWANS_SIRI.pdf katika aya ya mwisho kabisa yenye nambari 17.11..................
  .https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=19555&d=1294041387  Rostam Aziz aikana Richmond
  • Asisitiza kuendelea kuchochea uwekezaji nchni

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] KAULI aliyoitoa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa imemuibua Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
  Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Rostam alikanusha maelezo ya Dk. Slaa aliyemhusisha na tuhuma za kuhusika kwake kuileta nchini kampuni ya Richmond nchini kutoka nchini Marekani.
  Dk. Slaa ambaye kauli yake ilichapwa katika gazeti hili juzi alisema Richmond ililetwa nchini baada ya Rais Jakaya Kikwete na Rostam kwenda Marekani kwa malengo hayo kwa safari mbili tofauti.
  Akijibu shutuma hizo, Rostam alikanusha kwenda nchini Marekani wakati wa mchakato wa kuileta Richmond nchini na akasema kwa mara ya mwisho alikuwa nchini humo Desemba mwaka 2008.
  Alisema safari yake hiyo ya mwisho ya nchini Marekani ambayo alikwenda kwa mapumziko akiwa na familia yake, ilikuwa ni ya kwanza na ya mwisho kwenda huko katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
  "Siyo kweli hata kidogo kwamba nilikwenda Marekani kuishawishi Richmond ije nchini. Dk. Slaa anaendeleza porojo zile zile ambazo leo hii zimeligharimu taifa.
  "Angalia pasi yangu hii hapa ya kusafiria uone mwenyewe ukweli kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita nimepata kwenda Marekani mara moja tu, Desemba mwaka juzi," alisema Rostam huku akionyesha pasi yake ya kidiplomasia yenye namba za usajili AD000455.
  Alipotakiwa kueleza ni kwa sababu gani hasa jina lake limekuwa likitajwa katika sakata zima la sakata la Richmond, Rostam alisema jambo pekee analokiri kupata kulifanya ni kuwashawishi wamiliki wa kampuni ya Dowans Holdings SA iliyorithi mkataba wa Richmond kuja kuwekeza nchini katika sekta ya umeme.
  "Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke.
  "Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga," alisema Rostam.
  Alipotakiwa kueleza iwapo yeye ni mmoja wa watu wanaotarajia kufaidika na malipo ya shilingi bilioni 185 ambazo TANESCO inatakiwa kuilipa fidia Dowans, mfanyabiashara huyo alikana kuimiliki kampuni hiyo.
  Mbali ya kukanusha hilo, Rostam aliyabeza madai ya baadhi ya wanasiasa wanaohusisha fedha hizo na yeye akisema katika mkusanyiko wa biashara zake anazofanya ndani na nje ya nchi kiasi hicho cha fedha wanazotarajiwa kulipwa Dowans ni sawa na mapato yake ya miezi minne tu.
  Alisema, ni jambo linalosikitisha kwamba pamoja na porojo na maneno ya uongo anayosema mara kwa mara Dk. Slaa dhidi yake, mwanasiasa huyo ameendelea kuaminiwa na wananchi kwa sababu tu ya historia yake ya nyuma ya uongozi wa kidini.
  Akitoa mfano wa kile anachokiita porojo za Dk. Slaa, alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mwanasiasa huyo alipata kumhusisha na kuwapo katika kikao kimoja cha siri kilichodaiwa kufanyika jijini Mwanza wakati yeye (Rostam) akiwa nje ya jiji hilo.
  Katika gazeti la jana la Tanzania Daima Jumatano, Dk. Slaa alikaririwa akisema kwamba safari ya Rais Kikwete kwenda Marekani ambayo ilifuatiwa na ile ya Rostam katika kipindi cha mwaka 2006 ndizo zilizoileta Richmond nchini.
  Dk. Slaa alitoa kauli hiyo wakati akijibu taarifa ya Ikulu iliyotolewa mwanzoni mwa wiki hii ambayo ilikuwa ikikanusha madai ya Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA aliyemhusisha Rais Kikwete na ujio wa kampuni ya Dowans nchini.
  Ikulu katika taarifa yake iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, ilipinga maelezo hayo ya Dk. Slaa ikitumia lugha kali, kejeli na dharau.
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ukimkamata mwizi aliyekubuhu akiiba, ukampeleka mahakamani na kumwuliza je, ulikuwa ukiiba kweli, atajibu HAPANA. Ila, ukimbana sana kwa maswali ya kisheria, atajikuta anasema, "Kama uliniona naiba, je, nilikuwa nimevaa nguo gani?". Ukimwambia ya kijani, atasema, "Hapana, nilikuwa nimevaa nyekundu". Ipo siku, majibu kama hayo yatatokea.
   
 3. N

  Nipohaitena Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umesema kweli, na kama hawakubali wawashitaki kwa kusema uongo.
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu RA tumeshindwa kumwondoa hapa nchini!! Tunashindwaje kufanya hivyo???
   
 5. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  I wanna kill right now... wanna kill right now ....I wanna kill right now...wanna kill right now......
   
 6. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  I wanna kill right now... wanna kill right now ....I wanna kill right now...wanna kill right now......:whoo:
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Time is a healer,si mbali sana ni karibu tu ukweli tutaujua............subira tu.Huyu Mungu alitujulisha mpaka hapo atatujulisha na hayo yaliyobaki,
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,257
  Trophy Points: 280
  Kweli nyumba inaungua wewe unachekelea moto unavyowaka badala ya kuzima??
   
 9. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Siku watanganyika tutakaposhika hatamu!! Wewe na huyo RA wako... you'll be dead meat!!! And I promise you.... That wont be long!!!!
   
 10. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huyu Rostam anawaona WATZ wote kama mabwege hivi hamna namna ya kum-assassinate?
   
 11. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inashangaza kuona mwizi akimgeuzia kibao aliyemwibia na kumwita mwizi!!!
   
 12. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,989
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  what do you need from me? ammunitions or the gun itself?
  also tell me if you need a sniper - there's one in me for free!!
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Another schizophrenic reply, Entymologist wewe?
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo ukweli ni kwamba Rostam Aziz ndiye mmiliki halisi wa Dowans????
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Binafsi nimejifunza kitu. Watanzania weusi tunajenga nchi, watanzania wenye asili ya asia hasa wahindi na waarabu wanabomoa nchi. Ipo siku, kama hawatakuwa na adabu itabidi kuwafukuza. Si wote wafanyao hivyo bali wapo baadhi yao, wanamajivuno sana, wana kiburi, na wanataka kutufanya sisi kuwa wenda wazimu wao. Natoa rai kwao wajirekebishe kwani wanachochea moto wenyewe.
   
 16. n

  ngoko JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana aendelee hata akitaka ulinzi tunamhakikishia kama taifa tutampa covert and overt security ili bata alike vizuri ila tunamtaka mifupa ya hao bata atuachie ifikapo 2015 ikibidi kimyakimya tumsikie iran akiendelea na mambo mengine.
   
 17. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kweli common sense is not common..
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  maybe he had a quicky before responding to the post... hao ni imbeciles and dont even bite your tongue for them
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ndivyo anavyotuona,kama viongozi 'wetu' anawageuzageuza anavyotaka anaamini hao wanaowapigia kura ndo hamna kitu..hicho ni kiburi za Professional Misheni-tauni..
   
 20. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Ndiyo dada Michele, lakini hizi kauli za RA zinanifanya niwe na hasira ya kumpiga kichwa! Kwa nini, kila dalili zinaonyesha yeye ndiye amemkamatisha JK kwa masikio akimwelekeza kufanya ufisadi zote hizi. Hana haki ya kuzungumzia viongozi wetu kwanza sio raia. Haya ya kudai hakuwepo au alikuwepo wakati matukio fulani hana utetezi wowote huyu. Linaweza kabisa kuwa na passport mbili nilionavyo hili lijitu. Na kwa nini taifa likubali kuendeshwa kama kondoo anayepelekwa machinjoni! Jamani! Cha!
   
Loading...