Rostam Aziz: Dr. Slaa hatari kwa Taifa...............

Rostam Aziz: Dr. Slaa hatari kwa Taifa...............

Big up Rostam Aziz kwa maelezo mazuri sana,wewe huusiki kabisa na lolote wanakupaka matope tu hawa,Endelea kula bata tuu

Ooohhh!!! yamekuwa haya tena. mmhh!! hebu tusaidie kuelewa hawa bata anavyowakula.
 
Heshima yako mkuu,

Naomba uitundike document ya case proceedings uliyoquote kwenye message yako hii.

Natanguliza shukrani nyingi.

Ng'wana Diyu
 
Binafsi nimejifunza kitu. Watanzania weusi tunajenga nchi, watanzania wenye asili ya asia hasa wahindi na waarabu wanabomoa nchi. Ipo siku, kama hawatakuwa na adabu itabidi kuwafukuza. Si wote wafanyao hivyo bali wapo baadhi yao, wanamajivuno sana, wana kiburi, na wanataka kutufanya sisi kuwa wenda wazimu wao. Natoa rai kwao wajirekebishe kwani wanachochea moto wenyewe.

Ubongo wako unachemka Mlangaja, hapa suala sio rangi au asili, kuna mafisadi wengi sana ambao sio hao wahindi wala waarabu. Watu wabaya hawana rangi ila wana mioyo inayofanana.
 
Big up Rostam Aziz kwa maelezo mazuri sana,wewe huusiki kabisa na lolote wanakupaka matope tu hawa,Endelea kula bata tuu

"kweli kabisa,naona watu wameishiwa maneno kila saa rostam hivi rostam vile. Dr slaa ambae si doctor wa profession bali wa dini ni hatari ndio maana wamemshindilia store.nchi haiendeshwi na wendawazimu"
 
Wakati utaweka bayana kati ya hawa wawili yupi ni hatari zaidi na yupi anastahiri jera, nina imani kuwa katika uhai wangu huu (Inshallah Mungu jalia) nitashuhudia Rostam akiwajibishwa kwa madhambi yake na Dr Slaa akitukuzwa kwa uzalendo na ujasiri wake
 
Salvation time s around da corner! those who sarcasy us will be perished!
 
Time is a healer,si mbali sana ni karibu tu ukweli tutaujua............subira tu.Huyu Mungu alitujulisha mpaka hapo atatujulisha na hayo yaliyobaki,

Ni kweli Michelle, itafika hatua Mungu mwenyewe atachoka na yote yatajifunua waazi! Time will tell
 
Nani hatari kati ya mhujumu uchumi, mwizi, jambazi Aziz na mpigania haki Slaa mwenye uchungu na nchi yake????????????????????
Watz ifike pahala tutambue kuwa nchi hii inaliwa na watu wachache sana idadi yao hata kumi haifiki, ni watu wachache wanawapa wengine nafasi ya kuila nchi hii tajiri lakini tunaishi kwenye giza, nyumba za matembe, usafiri shida, elimu ya kisanii, hospitali zisizo na dawa.

Wazalendo wako wapi wenye uchungu na nchi yao.
 
RA huna siku nyingi sana utaumbuka tuu, mateso sisi watz tunayoyapata unayachnangia sana kwa wizi na ubaradhuli unaoufanya ktk nchi yetu.kilio chetu MUNGU anakisikia na siku si nyingi utaumbuka-MWIZI MKUBWA WEE.
 
Nani hatari kati ya mhujumu uchumi, mwizi, jambazi Aziz na mpigania haki Slaa mwenye uchungu na nchi yake????????????????????
Watz ifike pahala tutambue kuwa nchi hii inaliwa na watu wachache sana idadi yao hata kumi haifiki, ni watu wachache wanawapa wengine nafasi ya kuila nchi hii tajiri lakini tunaishi kwenye giza, nyumba za matembe, usafiri shida, elimu ya kisanii, hospitali zisizo na dawa.

Wazalendo wako wapi wenye uchungu na nchi yao.

Yaani bora mtu akunyime utajiri na si uwezo wa kufikiri, Ifike mahali wananchi wajue mbichi na mbivu. Mkuu nakuunga mkono 100%
 
"kweli kabisa,naona watu wameishiwa maneno kila saa rostam hivi rostam vile. Dr slaa ambae si doctor wa profession bali wa dini ni hatari ndio maana wamemshindilia store.nchi haiendeshwi na wendawazimu"

Ulitakiwa kufikiri kwa kina kwanza kabla hujaandika hii post yako!
 
Big up Rostam Aziz kwa maelezo mazuri sana,wewe huusiki kabisa na lolote wanakupaka matope tu hawa,Endelea kula bata tuu
Hysterical, zombie dont jump in to serious matters as this when you sick of hysteria.
 
"kweli kabisa,naona watu wameishiwa maneno kila saa rostam hivi rostam vile. Dr slaa ambae si doctor wa profession bali wa dini ni hatari ndio maana wamemshindilia store.nchi haiendeshwi na wendawazimu"

don't think like a chicken
 
Ooohhh!!! yamekuwa haya tena. mmhh!! hebu tusaidie kuelewa hawa bata anavyowakula.
Kaka kile ki Avtar chako cha Paka na Mtoto wa Kuku kiko wapi?
Ni PM basi Kama vp
 
Mmiliki wa gazeti la Rai; Rostam Aziz, ambaye ndiye wengi tunaamini ni mwakilishi wa JK kwenye kashfa ya DOWANS ambayo isipovaliwa njuga italigharimu taifa zaidi ya bilioni 100 ametumia nafasi yake tajwa visivyo alipotumia kumchafua Dr. Slaa na kumwita ni hatari kwa taifa wakati sisi tunaamini yeye Rostam Aziz ndiye hatari kwa usalama wa taifa hili.................................kwa kutuingiza mkenge ili tulipe ufisadi na hivyo kukwamisha jitihada za taifa hili kujitoa kwenye lindi la umasikini............

Aidha Rostam Aziz alidai ya kuwa Dr. Slaa alimzushia kushiriki kikao cha mwanza kilichopanga uchakachuaji wa kura wakati yeye alikuwa safarini Afrika ya Kusini safari ambayo hadi leo Rostam Aziz kashindwa kututhibitishia kuwa kwenye tarehe hizo kweli hakuwa nchini baada ya hata kushindwa kuonyesha kwenye pasi yake ya kusafiria mihuri na viza ya kuingia na kutoka kule Afrika ya Kusini.

Rostam Aziz pia anadai ya kuwa kwa mara nyingine Dr. Slaa amemzushia safari ya kwenda Marekani kwa ajili ya kupanga mipango ya kulipora Taifa hili mabilioni ya fedha kupitia DOWANS huku akishirikiana kwa karibu na swahiba wake JK safari ambayo Rostam Aziz anadai hakwenda..........kwani kwenye tarehe hizo alikuwa humu humu nchini..........Lakini kinyume na awali ambapo Rostam Aziz alionyesha baadhi ya ushahidi ambao uliongeza utata juu ya utetezi wake safari hii hakutoa ushahidi wowote ule kuthibitisha madai yake katika mazingira yanayothibitisha zaidi ya kuwa pengine hata safari hii anasema uongo tu...............Huenda safari hiyo ya marekani alikwenda na sasa anajishauashaua tu..............kujaribu kufunika ukweli.................Upo ushahidi ambao ulitolewa na Tanesco kwa msuluhishi ya kuwa Rostam Aziz ni mwasisi wa kashfa ya DOWANS.......................kama ushahidi huu uliotolewa na tanesco kwenye uamuzi wa DOWANS unavyojieleza..........

RostamAziz.jpg

Nakubaliana na Yeye Rostam kwamba Dr SILAA ni hatari kwa Taifa kwani ni kweli tupu maana ya Taifa kwa Rostam ni Mafisadi, maana wao ndo nchi ya Tanzania kwa kupitia Mlango wa CCM, sisi wananchi masikini ni wahamiaji wanasubiri tu waturudishe kwetu udongoni kwa shida zinazotukabili...
 
Kwa sasa hakuna mtu ambaye ni hatari katika nchi hii kama muajemi Rostam Aziz, yaani anatuibia mabilioni yetu mchana kweupe halafu tukionyesha kukataa kwa njia ya amani anaamuru polisi wake wauwe watanganyika. JAMANI KWA NINI HUYU MUAJEMI RA ASIUAWE?????????????
 
Rostam Aziz aikana Richmond
• Asisitiza kuendelea kuchochea uwekezaji nchni

na Mwandishi wetu

amka2.gif
KAULI aliyoitoa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa imemuibua Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Rostam alikanusha maelezo ya Dk. Slaa aliyemhusisha na tuhuma za kuhusika kwake kuileta nchini kampuni ya Richmond nchini kutoka nchini Marekani.
Dk. Slaa ambaye kauli yake ilichapwa katika gazeti hili juzi alisema Richmond ililetwa nchini baada ya Rais Jakaya Kikwete na Rostam kwenda Marekani kwa malengo hayo kwa safari mbili tofauti.
Akijibu shutuma hizo, Rostam alikanusha kwenda nchini Marekani wakati wa mchakato wa kuileta Richmond nchini na akasema kwa mara ya mwisho alikuwa nchini humo Desemba mwaka 2008.
Alisema safari yake hiyo ya mwisho ya nchini Marekani ambayo alikwenda kwa mapumziko akiwa na familia yake, ilikuwa ni ya kwanza na ya mwisho kwenda huko katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
“Siyo kweli hata kidogo kwamba nilikwenda Marekani kuishawishi Richmond ije nchini. Dk. Slaa anaendeleza porojo zile zile ambazo leo hii zimeligharimu taifa.
“Angalia pasi yangu hii hapa ya kusafiria uone mwenyewe ukweli kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita nimepata kwenda Marekani mara moja tu, Desemba mwaka juzi,” alisema Rostam huku akionyesha pasi yake ya kidiplomasia yenye namba za usajili AD000455.
Alipotakiwa kueleza ni kwa sababu gani hasa jina lake limekuwa likitajwa katika sakata zima la sakata la Richmond, Rostam alisema jambo pekee analokiri kupata kulifanya ni kuwashawishi wamiliki wa kampuni ya Dowans Holdings SA iliyorithi mkataba wa Richmond kuja kuwekeza nchini katika sekta ya umeme.
“Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke.
“Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga,” alisema Rostam.
Alipotakiwa kueleza iwapo yeye ni mmoja wa watu wanaotarajia kufaidika na malipo ya shilingi bilioni 185 ambazo TANESCO inatakiwa kuilipa fidia Dowans, mfanyabiashara huyo alikana kuimiliki kampuni hiyo.
Mbali ya kukanusha hilo, Rostam aliyabeza madai ya baadhi ya wanasiasa wanaohusisha fedha hizo na yeye akisema katika mkusanyiko wa biashara zake anazofanya ndani na nje ya nchi kiasi hicho cha fedha wanazotarajiwa kulipwa Dowans ni sawa na mapato yake ya miezi minne tu.
Alisema, ni jambo linalosikitisha kwamba pamoja na porojo na maneno ya uongo anayosema mara kwa mara Dk. Slaa dhidi yake, mwanasiasa huyo ameendelea kuaminiwa na wananchi kwa sababu tu ya historia yake ya nyuma ya uongozi wa kidini.
Akitoa mfano wa kile anachokiita porojo za Dk. Slaa, alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, mwanasiasa huyo alipata kumhusisha na kuwapo katika kikao kimoja cha siri kilichodaiwa kufanyika jijini Mwanza wakati yeye (Rostam) akiwa nje ya jiji hilo.
Katika gazeti la jana la Tanzania Daima Jumatano, Dk. Slaa alikaririwa akisema kwamba safari ya Rais Kikwete kwenda Marekani ambayo ilifuatiwa na ile ya Rostam katika kipindi cha mwaka 2006 ndizo zilizoileta Richmond nchini.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo wakati akijibu taarifa ya Ikulu iliyotolewa mwanzoni mwa wiki hii ambayo ilikuwa ikikanusha madai ya Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA aliyemhusisha Rais Kikwete na ujio wa kampuni ya Dowans nchini.
Ikulu katika taarifa yake iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, ilipinga maelezo hayo ya Dk. Slaa ikitumia lugha kali, kejeli na dharau.
 
Alipotakiwa kueleza ni kwa sababu gani hasa jina lake limekuwa likitajwa katika sakata zima la sakata la Richmond, Rostam alisema jambo pekee analokiri kupata kulifanya ni kuwashawishi wamiliki wa kampuni ya Dowans Holdings SA iliyorithi mkataba wa Richmond kuja kuwekeza nchini katika sekta ya umeme.
"Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke.
"Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga," alisema Rostam.

Hivi huku kama siyo kukiri basi nini?
 
Back
Top Bottom