Rostam Aziz anavyompiga tafu rafikiye Lowassa

Rostam Aziz anavyompiga tafu rafikiye Lowassa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,972
Reaction score
25,365
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia namna Channel Ten inavyotumika kumpamba Lowassa kwenye taarifa zake za habari, na kufanikiwa kuunganisha dots kama ifuatavyo:

Siku zote Channel Ten wamekuwa wakiripoti taarifa za Lowassa kwa ustadi wa hali ya juu sana na taarifa zake hupewa air time ya kutosha tofauti na wagombea wengine ndani ya CCM.

Huu ni mpango maalumu wa Rostam Aziz (mmiliki wa Channel Ten) kumpigia debe fisadi mwenzake ili pindi akifanikiwa kuingia ikulu ya magogoni washirikiane naye kuiba rasilimali za taifa.

Mtakumbuka kwamba Lowassa, Chenge na Rostam ni mapacha watatu (utatu wa KIFISADI) ndani ya CCM. Hawa watu hawakukutana barabarani. Wamekuwa wakishirikiana katika shughuli zao za kulihujumu Taifa kwa muda mrefu sasa.

Mtakumbuka hata Nape Nnauye alijaribu kuwavua magamba akawashindwa. Endapo EL atafanikiwa kuingia ikulu mwaka huu, basi elewa kwamba ikulu yetu itageuka kuwa pango la wanyang'anyi. Tuwe makini na mafisadi hawa na kamwe tusiwaruhusu kuisogelea ikulu yetu.

:israel:
 
Kanunue ndimu ukamue ujaribu kujinasua na hicho kichefu chefu...
 
Ni kweli kabisa Channel 10 wanampamba sana Lowassa na reporter siku zote ni mmoja ambae anaonekana kapewa jukumu la kuzunguka na Lowassa nchi nzima hata kule ambako Channel 10 ina waandishi(reporters) wengine!!

Ni mwanamke mmoja kwani sauti ni ile ile kila siku Lowassa awe Moshi,Mpanda n.k!
 
Amejitapa mda mrefu kwamba iwe isiwe yeye ndio Rais...ndio maana ya maajabu yote haya anayoyafanya sasahivi, ikiwa ni pamoja na kutafuta wadhamini tu yeye kageuza kipindi cha kampen. Tutaona mengi mwaka huu kisa tu mafisadi wanataka kutawala waiangamize nchi yetu
 
Hata wakimpatia airtime ya ziada itamsaidia nini Lowassa kuingia Ikulu?

1: maana CCM bado hawajamchagua mtu wa kusimama kama mgombea
2: kwa sasa hakuna mwananchi anayemchagua mgombea wa CCM, so hata akitangazwa sana haimsaidii kitu,
3: nadhani kwa sasa wanachofanya wakina Lowassa ni kujionyesha jinsi walivyojirikimbizia mali na jinsi walivyo na njaa ya kuingia ikulu kutufilisi
 
Simpendi EL na simkubali kabisa, ila mleta mada ni mnafiki wa kutupwa, kumbuka chanel 10 ni tv ya kibiashara na inafagilia anayeilipa regardgless faida kwa taifa.

Mbona kila siku tv ya umma tbc1 imesheheni taarifa za CCM na kupotosha kuhusu upinzani unakenua tu? Waambie hao tbc1 wamtangaze kwa mbwembwe mgombea wako ili akipata madaraka upate tender ya hata shughuli usizo na uwezo nazo.
 
Yule dada ni yule ripota wao wa Arusha ndo nimemsikia mara zote akimlipotia, hawa wamehongwa tu kama wachumia tumbo wengine ijapokuwa hawatafanikiwa
 
Ni kweli kabisa Channel 10 wanampamba sana Lowassa na reporter siku zote ni mmoja ambae anaonekana kapewa jukumu la kuzunguka na Lowassa nchi nzima hata kule ambako Channel 10 ina waandishi(reporters) wengine!!

Ni mwanamke mmoja kwani sauti ni ile ile kila siku Lowassa awe Moshi,Mpanda n.k!

mkuu kumbe hata wewe umenote hilo? huu ni mpango maalum unaotumiwa na mafisadi kumpiga tafu fisadi mwenzao ili akitinga ikulu washirikiane naye kuiba rasilimali za taifa. taarifa za lowassa hupewa muda wa kutosha na huripotiwa kwa mbwembwe za hali ya juu ili kuihadaa hadhira ya watanzania juu ya ufisadi wa lowassa.
 
huyu fisadi na kundi lake la majambazi

ikulu ni mahali patakatifu. ukiona fisadi anatimka mbio kuelekea ikulu, mwogope kama UKIMWI. kamwe hatuwezi kuwaruhusu mafisadi wainajisi ikulu yetu.
 
Jaman naona video ya matangazo ya mgombea mwingine na lowasa halaf tuangalie dakika mm siamin hili naona ni uzushi tuu na chuki Ndio ile ya Malima kusema mengi anajipendelea kwenye taarifa zake yale yalikuwa madai ya kijinga kabisa
 
Jaman naona video ya matangazo ya mgombea mwingine na lowasa halaf tuangalie dakika mm siamin hili naona ni uzushi tuu na chuki Ndio ile ya Malima kusema mengi anajipendelea kwenye taarifa zake yale yalikuwa madai ya kijinga kabisa

mkuu, sio kwenye matangazo...ni kwenye taarifa za habari za Channel Ten...Lowassa hupambwa zaidi ya wenzake na hupewa air time mara 3 zaidi ya watangaza nia wengine. umeona eeh?
 
Hivi Rostam anamiliki kila kitu humu nchini mwetu?
 
Watanzania wengi wanawachukia Matajiri.
Rostam ni mfanya biashara hajawahi muibia mtu chochote. Mwenye ushahidi aende mahakamani
 
Watanzania wengi wanawachukia Matajiri.
Rostam ni mfanya biashara hajawahi muibia mtu chochote. Mwenye ushahidi aende mahakamani

wewe ni ndoooooorobo! unajua kashfa ya UFISADI iliyopelekea rostam kuutema ubunge na kukimbilia nchini kwao India kabla Nape Nnauye hajamvua gamba au unakuja kuweweseka hapa kama kuku anayeta kiota cha kutagia?
 
Last edited by a moderator:
Watanzania wengi wanawachukia Matajiri.
Rostam ni mfanya biashara hajawahi muibia mtu chochote. Mwenye ushahidi aende mahakamani

hawachukii matajiri wanachukia mtanzania mwenzao akiwa tajiri mbona yule dangote kauziwa kipande cha mkoa ajenge bandari watu wamefurahi wanacheza ngoma ingekuwa Mengi, Dewji au Manji tatizo hovyooooooooo
 
Back
Top Bottom