Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,901
- 20,410
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwa sasa kuna mgogoro mkubwa ambao umeibuka ndani ya Team Lowasa baina ya wale wanaomuunga mkono Apson Mwang'onda na kambi ya Rostam Aziz. Chanzo changu ndani ya Team Lowasa kimebainisha kuwa mara baada ya ujio wa Rostam, hali ndani ya kambi hiyo imeanza kwenda kombo kutokana na kutofautiana kifalsafa na mbinu za kumpeleka Lowasa Magogoni.
Taarifa zinasema kuwa kambi ya Apson inaundwa na watu weledi na wenye uzoefu kwenye mikakati mbalimbali hasa kutokana na wengi wao kuwa wamewahi kulitumikia taifa hili katika maeneo tofauti. Hata hivyo, weledi wao unaonekana kuwa si lolote wala chochote kutokana na kushindwa kufanikisha kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri kuu ambao wamekuwa wakimkemea waziwazi Lowasa pale anaposhindwa kwenda sambamba na kanuni na maadili ya chama. Pia kambi hii ni masikini na walala hoi kwa vile wamekuwa wakinyonya kambi ya Rostam kifedha kupitia kwa Lowasa mwenyewe. Kwa maana nyingine, kambi hii ni ya wanyonyaji na kwamba wapo kwa Lowasa kimaslahi zaidi na si kufanikisha lengo la Lowasa kwenda Ikulu. Hii ni kambi ya 'KUPE'.
Kambi Rostam, nguli wa kashfa mbalimbali za ufisadi nchini inaundwa na watu wenye jeuri ya pesa ambao wamekuwa wakiitwa au kujiita kwa majina yenye kuonesha jeuri ya pesa kama Mzee wa Vijisenti, Nyoka Mwenye Makengeza nk. Kambi hii inaamini kuwa fedha inaweza kufanya kila kitu ikiwa ni pamoja na kununua haki za wana CCM.
Kwamba wapende wasipende ni lazima Lowasa aende Ikulu kwa vile pesa zipo. Kwa maana nyingine Kambi Rostam ndio wafadhili wakuu wa Team Lowasa kifedha.
Kutokana na jeuri ya pesa waliyonayo, wamefanikisha kumshawishi Lowasa kuwatema baadhi ya washauri wake walio chini ya Apson na kwa sasa Rostam ndiye anayeratibu harakati zote za Lowasa huku akiwatumia vijana wake kama Peter Serukamba na Hussein Bashe.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona kuwa mwelekeo wa Team Lowasa kwa sasa ni mbaya na kwamba lengo lao la kumpeleka Magogoni halitafanikiwa. Kwamba, watu ambao wameteka kambi hiyo hawana taswira nzuri ndani ya chama na kwenye jamii kutokana na kuhusika kwao na kashfa mbalimbali zinazoibuka nchini ikiwa ni pamoja na EPA, RICHMOND, ESCROW, VODACOM nk.
Kwamba, ujio wa Rostam si kwamba amekuja kuimarisha kambi hilo bali amekuja kuliangamiza na kwamba amekuja kuzidisha uchafu kwenye uchafu. Ni sawa na kutupa kinyesi kwenye jalala.
Rostam hana pesa bali anatumia pesa alizokwapua kwa njia ya kifisadi kumweka fisadi mwenzake madarakani huku akiamini kuwa pindi Lowasa akiwa Rais, fedha zote zitarudi kwa njia ile ile ya kifisadi.