fangfangjt
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 571
- 139
RA amesema yeye ni mwanasiasa makini na kamwe hababaishwi na wanasiasa uchwara.
Amesema maisha magumu kwa watanzania hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa.
SOURCE: MWANANCHI PG2
Complete article.
MBUNGE wa Igunga,mkoani Tabora, Rostam Aziz amesema yeye ni mwanasiasa makini na kamwe hababaishwi na wanasiasa uchwara , ambao wamekua wakieneza maneno ya uongo na uzushi dhidi yake.
Akizungumza na wananchi wa mjini Igunga katika Viwanja vya CCM mjini Igunga jana, Rostam alisema kuna wanasiasa ambao kila kukicha, wamekuwa wakitoa maneno ya kuchafuana na kupakana matope.
Alisema hata hivyo , wanasiasa hao hawambabaishi.
Alisema mwanasiasa makini ni yule anayetoa hoja za ukweli na si anayetoa maneno ya kuhamashisha wananchi wafanye vurugu.
Aliwata wananchi wa jimbo hilo kuwaepuka watu hao kwa kuwa ni hatari kwa nchi.
"Hivi karibuni kumekuwa na chama cha siasa kinachoendesha propaganda na kupiga domo kwa kuwahadaa wananchi kwamba maisha magumu yanatokana na wao kuichagua CCM," alisema Rostam.
Aliongeza "watu hao ni waongo kwani maisha magumu hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa."
Alisema kupanda kwa bei ya sukari na mafuta nchini, hakutokani na CCM na kwamba chama hicho hakina kiwanda cha sukari wala hakiagizi mafuta kutoka nje ya nchi.
Alisema hata nchi jirani Kenya na Uganda, nazo zimekumbwa na mfumuko wa bei ya bidhaa hizo ambapo bei ya sukari katika nchi hizo ni Sh2,000 kwa kilo sawa na Tanzania.
Alisema propaganda za kisiasa zinazoendeshwa na chama hicho ambacho hakukitaja kwa jina, zinalenga katika kuwapotosha watu.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuyapuuzia maneno ya wanasiasa wa chama hicho kwa madai kuwa ni uongo.
Alisisitiza kuwa viongozi wa chama hicho ni waongo kuhusu madai wanayoyatoa.
"Nilikutana na Dk Wilibrod Slaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza nikamuuliza kuwa nilisikia wakati ukihutubia wananchi wa Musoma kwamba Chadema mkichukua nchi mfuko mmoja wa saruji utauzwa Sh5,000 tu, lakini hakujibu," alisema Rostam.
Alisema kwa mtazamo huo aligundua kwamba maneno wanayozungumza Chadema ni ya kudanganya wananchi ili wawape ridhaa ya kuongoza nchi na si kuwaletea maendeleo kama walivyokuwa wakijinadi.
Alisema katika kipindi hiki kigumu, amegundua kwamba wananchi wa Igunga wana hali mbaya ya chakula na kwamba atahakikisha kuwa hawafi kwa njaa. Mbunge huyo aliwaomba wananchi wa Igunga kumuunga mkono ili afanikishe malengo yake ya kuwaletea maendeleo.