Elections 2010 Rostam amvaa Dr. Slaa lakini utetezi wake wamweka pabaya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
Rostam Aziz amejitetea huku akimnyanyapaa Dr. Slaa kuwa ni mzushi na anazeeka vibaya lakini utetezi wake Bwana Rostam ya kuwa alikuwa Afrika ya Kusini wakati tarehe za hicho kikao cha kupanga mikakati ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi ambacho Dr. Slaa alidai kilifanyika Mwanza chini ya uenyekiti wake JK............

Tatizo kwa Rostam Aziz ni utetezi wake ndiyo unamweka pabaya sana...........

Bw. Aziz ametoa nakala ya pasipoti yake ikionyesha muhuri wa uhamiaji kwa tarehe ileile ambayo ilidaiwa alikuwa Mwanza...lengo hapa ni kuonyesha ya kuwa alikuwa safarini siku hiyo akielekea Afrika ya Kusini.......sasa tatizo ni nini?

Mapungufu ya utetezi wa Mheshimiwa Mbunge wa Igunga ni kuwa ushahidi wake haujitoshelezi hata kidogo kwa sababu zifuatazo:-

a) Pasipoti yake haikuonyesha mihuri ya uhamiaji ya Afrika ya Kusini wakati akiingia huko na akitoka jambo ambalo linaashiria pengine muhuri wa Tanzania kwa siku ya kuondoka ulikuwa umewekwa baada ya hizo tarehe ambazo yadaiwa alikuwa Afrika ya Kusini............

b) Hana ushahidi wa hoteli alizofikia kule Afrika ya Kusini kwa maana ya nakala za risiti ili watakaotaka kwenda kukagua hizo hoteli waweze kufanya hivyo na kujihakikishia kuwa yumo kwenye orodha ya wageni wa hoteli hizi kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu..kwa tarehe husika....kama ameghushi vitu hapo atakamatwa............................................................

c) Rostam anadai alikwenda kukutana na wafanya biashara wenzie huko Afrika ya Kusini lakini hajaambatanisha hati za viapo za hao jamaa zake ili kuweka uzito kuwa kweli kuna watu aliokutana nao Afrika ya Kusini na kwa kutofanya hivyo ushahidi wake wa kusemea watu wengine ni ."hearsay".......ambao tunalazimika kupuuza kabisa kuwa ni majungu aliyoyapika yeye mwenyewe.......

d) Mbaya kulikoni yote kwa Mheshimiwa Rostam Aziz hakuonyesha kwenye nakala za pasipoti yake mihuri ya Afrika ya kusini na Tanzania kuonyesha tarehe alizotoka Afrika ya Kusini na kurejea nchini................Tatizo hapa ni nini?...............Kulingana na ushahidi wake mwenyewe Rostam Aziz alipaswa awe bado yuko Afrika ya Kusini lakini sasa yupo nchini hili linawezekanaje?

e) Rostam atuonyeshe nakala za tiketi za ndege ambazo aliondoka nayo hapa nchini kwenda Afrika ya Kusini na ile iliyomrudisha nchini...........hapo ndipo kizazaa kilipo Mheshimiwa............

Yaani anavyo vielelezo vya uhamiaji vya kutoka hapa nchini lakini hana vya kurudi nchini hii ni nini kama siyo uhamiaji imeshiriki kuchakachua kumbukumbu zake kwenye pasi yake ya kusafiria ili kutoa mwanya wa kutoa utetezi wa kumbeza Dr. Slaa ambao hata haonyeshi ya kuwa utetezi huo ulienda darasa lolote...............

Bado tunamwomba Mheshimiwa Mbunge wa Igunga kujibu hizi hoja za kimsingi na kadri atakavyokuwa akiendelea kuzijibu atajifunza ya kuwa....the devil of "pack of lies" is always on the details.................Make my day Mheshimiwa Rostam Aziz.......and be my guest......This rebuttal of yours is no smoking gun, at all!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,466
1,164
Hivi huo uhudhuriaji wa kikao hicho umetajwa kwamba ni physical pekee au? Ina maana telephone na video conferencing haziwezi kumuhesabu mtu kama alihudhuria?

Just curious!
 
We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
46
Hivi huo uhudhuriaji wa kikao hicho umetajwa kwamba ni physical pekee au? Ina maana telephone na video conferencing haziwezi kumuhesabu mtu kama alihudhuria?

Just curious!

Kila kitu kina mwisho wake. Hata hivyo, ni kile tu ambacho kina mwanzo
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
Haya maswali vilevile huyu Ridhiwani aliyedai alikuwa nje ya nchi wakati wa kikao hicho anapaswa kutoa vielelezo vya ushahidi vinavyojitosheleza haitoshi yeye kudai kuwa alikuwa nje ya nchi kwenye hizo tarehe halafu akaishia hapo............We need concrete evidence and alibi.......we are not fools as they deign us we are.................................
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
Hivi huo uhudhuriaji wa kikao hicho umetajwa kwamba ni physical pekee au? Ina maana telephone na video conferencing haziwezi kumuhesabu mtu kama alihudhuria?

Just curious!
Mr. Nyambala; my friend, video-conferencing ndiyo itamweka mahali pabaya zaidi ya kuwa kumbe alikuwa nchini na yeye Rostam Aziz anataka aonekane alikuwa Afrika ya Kusini na hivyo asingeweza kuhudhuria kile kikao cha kupanga mikakati ya kuchakachua matokeo cha jijini Mwanza........................
 
Kishaini

Member
Jun 23, 2008
45
4
Cha msingi ni kwamba kikao kilifanyika. Ila sasa watu wanataka kujitoa kwamba hawakuusika/hawakuhudhuria. Ukiweka ukuwaji wa tekinologia, inaniofanya niamini kwamba AZ alihudhuria kikao hiki (physical or via phone or video link or skype, etc) na he was awere of the said meeting. Hayo anayoyasema ni bla bla tu. :A S angry:
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,685
13,199
Huyu msukuma ambaye wasukuma wanaamini ni msukuma kutoka asia...........kweli wajinga ndiyo waliwao..............kwa nini wasukuma mnaruhusu watu wa namna hii wa kuliangamiza taifa na ambao hawawezi kuchukuliwa hatua zozote na rais mnawachagua?.......tutaanza kuilaumu mikoa inayotuchagulia wasia wakati wana vijana wao wamewasomesha kwa pesa nyingi na kwa kukamuliwa na ccm..........akina rostamu sisemi tuwafukuze ila tuwaruhusu waendelee na kilichowaleta yaani wafanye biashara zao halali walipe kodo na mambo ya nchi watuachie................wasukuma bado mnachagua rangi?....hamtaki vijana wenu wazawa waende bungeni kuwatetea?.......hata km mtu anauwezo kiasi ganiu lakini lazima muheshimu utu wenu kwa kujiheshimu wenyewe..........nawalaumu wasukuma kwa kuendelea kutuletea mafisadi......chenge,rostam na arusha wanatuleta lowasa................
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,521
4,963
Kwa mtu ambaye ana dead conscience mnadhani angesemaje? kama si kuendelea kukana tu wakati moyoni anajua alilolifanya!
 
ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,427
Huyu msukuma ambaye wasukuma wanaamini ni msukuma kutoka asia...........kweli wajinga ndiyo waliwao..............kwa nini wasukuma mnaruhusu watu wa namna hii wa kuliangamiza taifa na ambao hawawezi kuchukuliwa hatua zozote na rais mnawachagua?.......tutaanza kuilaumu mikoa inayotuchagulia wasia wakati wana vijana wao wamewasomesha kwa pesa nyingi na kwa kukamuliwa na ccm..........akina rostamu sisemi tuwafukuze ila tuwaruhusu waendelee na kilichowaleta yaani wafanye biashara zao halali walipe kodo na mambo ya nchi watuachie................wasukuma bado mnachagua rangi?....hamtaki vijana wenu wazawa waende bungeni kuwatetea?.......hata km mtu anauwezo kiasi ganiu lakini lazima muheshimu utu wenu kwa kujiheshimu wenyewe..........nawalaumu wasukuma kwa kuendelea kutuletea mafisadi......chenge,rostam na arusha wanatuleta lowasa................

Kaka usitulaumu sisi wasukuma, laumu mfumo mzima wa Chama cha Mapinduzi kutetea mafisadi. tutake radhi.
 
quimby_joey

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
385
129
Jana nilikuwa najaribu kupitia maandiko fulani kuona ni vp mwizi na jangili anvyoweza kutawala watu wasafi wamwaminio Mungu, nikakutana na mstari mmoja unasema MWENYE NACHO ATAONGEZEWA NA ASIYE NACHO HATA KILE KIDOGO ATANYANG'ANYWA(emphasis is mine). Kilichopo sasa tuangalie tu mbele kila mtu aokoe nafsi yake.
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,466
1,164
Mr. Nyambala; my friend, video-conferencing ndiyo itamweka mahali pabaya zaidi ya kuwa kumbe alikuwa nchini na yeye Rostam Aziz anataka aonekane alikuwa Afrika ya Kusini na hivyo asingeweza kuhudhuria kile kikao cha kupanga mikakati ya kuchakachua matokeo cha jijini Mwanza........................

Mkuu Ruta, my curiousity kuhusu aina ya uhudhuriaji inakuja kutokana na kwamba barua imeeleza wahudhriaji kwenye kikao hicho. Lakini from what I know hata ukichangia mkutano thru teleconf. au videoconf. unakuwa ni muhudhuriaji and remember this can be done from anywhere in the world. Hivyo basi hawa watu kuibuka na kusema hawakuwa Mwanza siku hiyo si hoja yenye mashiko in this respect.
 
realtz7

Senior Member
Oct 23, 2010
110
1
ujue hawa jamaa majinga sana, wanadhani kufoji ni kazi rahisi?koporay real situation is an at, am sure sasa wanatauta hai fasta fasta, na becaus ni vlaza hawawzi kujiuliza maswali muhimu kuhusu ulaghai wao, kwa taarifa yao, kulaghai is an art, huwezi kurupuka utadakwa tuu
 
david2010

JF-Expert Member
Sep 23, 2010
257
49
Mafisadi kama hao tumeshawajua na kuwazoea kwani anaweza kufoji kila kitu na kujitakasa kwa kutumia pesa ila kila kitakachofanyika sirini kitafichuliwa, kama kweli hawahusili wakae kimya kila kitu kitawekwa wazi
Haya maswali vilevile huyu Ridhiwani aliyedai alikuwa nje ya nchi wakati wa kikao hicho anapaswa kutoa vielelezo vya ushahidi vinavyojitosheleza haitoshi yeye kudai kuwa alikuwa nje ya nchi kwenye hizo tarehe halafu akaishia hapo............We need concrete evidence and alibi.......we are not fools as they deign us we are.................................
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Mtakafufa na vijiba vya roho!

1.Hiyo barua ya Mwaanza aidha iliandikwa na wajanja wachache wa CCM ili kuwatisha wapiga kura

2.Au imegushiwa

3.Niemkuwa Mfuatiliaji na mshiriki wa siasa muda mrefu,Rais hawezi kuwa mjinga kiasi hicho cha kukutana na watu kwenye hoteli ya Lakairo na kupanga mipango mkibuwa kiasi hiki.Hell No

Mwizi msemeni ili ukweli juu yake Mmsiupotoshe.Nina uhakika RA alikuwa afika kusini kipindi hicho na kuna watu wangu wa karibu walikuwa naye kwenye huo mkutano Jo 'berg!
 
Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
111

Alikwenda kumalizia course fee ya masters yako!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom