Rostam amesahau nini kwenye siasa?

Rostam amesahau nini kwenye siasa?

huyu jamaa nimpigaji tu!hafai hata kidogo,majanga yote ya upigaji kuanzia epa (kagoda)richmond,symbion na sasa vodacom...
Kama ulikuwepo kwenye mawazo yangu huyu jamaa atakuwa mwizi tu.
 
haa haa naona mapacha watatu wanarudi kwa kasi ili watuwekee fisadi wao magogoni. na kwa vile hao watu wameshapenya misikitini na makanisani kama taifa tumekwama.
 
Rostam mwizi,anayemuunga mkono nae mwizi,hii haikubariki watanzania sio mazumbukuku...
 
Atakayeungwa mkono na rostam anajichafua kwa kinyesi
 
Na Mwandishi Wetu

Rostam Aziz aliyejiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011 kwa shinikizo kutokana na kashfa ya ufisadi, amerudi kwenye siasa kwa nguvu kubwa huku akiapa kuwa ni lazima ahakikishe anamuingiza Rais wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2015 kwa kutumia fedha alizonazo.

Katika kuitimiza azma yake hiyo ya kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma, tayari amekuwa akiratibu vikao mbalimbali vya kimikakati nyumbani kwake Oysterbay, ili kuhakikisha kuwa mgombea wake ambaye amejijengea sifa ya kuwa mgawaji fedha maarufu kwenye harambee na tafrija mbalimbali, anapitishwa na CCM na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania.

Pamoja na kuwa jina lake na la mgombea amtakaye tayari yameshachafuka sana mbele ya macho ya Watanzania, kutokana na kashfa zao za ufisadi zilizowahi kuwakumba huko nyuma; wawili hao wamepanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kununua vyombo vya habari ambavyo watavitumia kuendesha kampeni ya kujisafisha na hatimaye waonekane ni watu safi kabisa mbele ya wananchi.

Tayari mgombea huyo wa Rostam amesikika akiwaambia watu wake wa karibu kuwa kambi yake imeshavishika vyombo vya habari karibu vyote hapa nchini.

Karibu vyombo vya habari vyote vya Tanzania tumeviweka mkononi. Simuoni mtu wa kuzuia harakati zangu, mimi ni kama mafuriko sizuiliki, mgombea huyo alisikika akitamba.

Katika kufanikisha harakati zao, wawili hao, wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza ushawishi kwa makundi mbalimbali ya kijamii. Tayari mgombea huyo wa Rostam ameonekana akishiriki harambee mbalimbali na kutoa fedha nyingi na pia amekuwa akitoa kauli zenye kuashiria kujipigia debe ili apitishwe kugombea Urais na CCM.

Pia, mgombea huyo ameendesha harakati za chini kwa chini za kuwagawa wabunge na wanachama wa CCM katika makundi ili afanikishe azma yake ya kuupata Urais. Wawili hao ambao wamekuwa pamoja katika harakati za muda mrefu wanadaiwa kujivunia nguvu kubwa ya fedha waliyonayo kufanikisha mambo yao.

Mdau mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedokeza: Hawa jamaa wanaamini kuwa kwa fedha walizonazo wanastahili kabisa kuinunua nchi. Wanadhani kuwa sifa ya kuwa na fedha nyingi ndiyo sifa ya kipekee kabisa ya wao kupata Urais, masuala ya uadilifu na uaminifu kwao siyo muhimu kabisa.

Mtazamo wa wachambuzi wa mambo.

Hata hivyo, pamoja na nia yake hiyo, wachambuzi wa mambo, wameyatathmini maisha ya Rostam na kubaini kuwa ni mtu hatari sana ambaye amefanikiwa kupata utajiri mkubwa kutokana na kujihusisha na dili za kifisadi ambazo zimeliacha taifa katika umaskini mkubwa.

Huyu mtu ameshiriki katika ufisadi mkubwa ambao umechangia kudhoofisha uchumi wa nchi hii halafu anarudi kwa kutumia fedha alizozipata kifisadi kutaka kuwarubuni Watanzania na kuchukua uongozi tena, hii haikubaliki, mmoja wa wachambuzi ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini alisema.

Rostam ametajwa kwenye orodha za matajiri wakubwa Afrika na Jarida la Forbes. Pia inadaiwa kuwa miongoni mwa makampuni anayoyamiliki yeye na familia yake kuwa ni pamoja na: Africa Tanneries Ltd- Mwanza, Tanzania Leather Industry Ltd- MOROGOR, African Trade Development Group (Tz), Tanzania Packages Manufacturing, Caspian construction, New Habari corporation na Wembere Hunting Safari company.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa mara nyingi Rostam hutumia staili ya kuanzisha makampuni kwa kutumia mawakala kufanikisha dili zake. Inadaiwa kwa hufanya hivi ili yakitokea matatizo aweze kuruka kwamba hahusiki.
Tabia ya kukwepa kujibu tuhuma za ufisadi

Pia, wachambuzi wamesema kuwa Rostam Aziz amekuwa na tabia ya kukimbia kujibu hoja mbalimbali za ufisadi zinazoibuliwa dhidi yake kwa kutoa matusi kwa watoa hoja hizo.

Kuna kipindi Rostam alibanwa kila kona kuhusu ushiriki wake katika dili kadhaa za kifisadi. Baada ya kuzidiwa alitumia staili ya kuwaita majina mabaya wale wote ambao walikuwa wakiongelea kuhusu dili zake chafu za kudidimiza uchumi wa nchi huku akizunguka nyuma na kujifanya kuwa yeye ni mtu mwema, anaendelea kueleza mchambuzi huyo.

Imeelezwa kuwa bado taifa halijasahau namna ambavyo Mchungaji Mtikila alipoambiwa arudishe hela alizokopa pale alipoibuka na kuuzungumzia ufisadi wa Rostam.

Kilichomponza Mtikila ni kitendo chake cha kuandika kijarida kilichobeba kichwa cha "Hatima ya Mwajemi Sakarir" alichokitoa mwezi juni mwaka 2008, ambacho kilizungumzia namna ambavyo nchi inatafunwa na pia kikagusa kuhusu maisha na uraia wa Rostam Aziz, mchambuzi mwingine anaeleza.

Katika kijarida hicho Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni kiini cha uporaji mkubwa wa rasilimali za nchi unaoendelea kufanyika. Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliofanyika katika Benki Kuu na Hazina. Sehemu ya kijarida hiyo inaeleza:

Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja na utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya 'mataahira' kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la 'Rostam'. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ngombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu.

Mtikila alitahadharisha kuwa Watanzania wawe makini kwasababu Rostam anazo hati za kusafiria (passport) mbili ambazo anazitumia kusafiria maeneo mbalimbali na kwamba mambo yakiharibika nchini anahamia nchi nyingine.

Nilipoanza kuzungumzia uraia wa 'Rostam' Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo'Rostam' amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli. Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu, Mtikila alieleza katika kijarida hicho. Mtikila alimalizia kwa kuitaka Serikali imkamate na kumweka ndani Rostam.

Siku chache baada ya kutoa tuhuma hizi, Rostam aliibuka na kuitisha mkutano na vyombo vya habari ambako alisema kuwa Mtikila anamwita yeye fisadi wakati alikuwa amemkopesha shilingi milioni tatu na akasema kuwa anabaguliwa kwa kuzingatia misingi ya rangi yake.

Hoja hizi zilipingwa na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa kuwa ni nyepesi ambapo wadau mbalimbali walisema kuwa nchi hii ina maelfu ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia; Kizungu, Kiarabu ambao wana mafanikio makubwa sana kibiashara lakini hawakuwahi kuhusishwa na ufisadi wa kutisha kama alionao Rostam, sasa kwanini yeye aonewe?

Ugomvi na Mengi

Mbali na Mtikila, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, pia alikumbwa na mkono mkali wa Rostam pale alipomtaja kuwa ni miongoni mwa mafisadi papa wanaoididimiza Tanzania. Badala ya kuongelea kuhusu tuhuma zake, Rostam aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuanza kumshambulia Mengi kwa kusema kuwa Mengi ni fisadi nyangumi ambaye amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwachafua wenzake

Katika hali ya kushangaza, Rostam alienda mbali zaidi na kuyatumia magazeti na vyombo vya habari anavyovimiliki kuandika habari, makala na tahariri zilizoonyesha kuwa Mengi ni mtu asiyefaa katika Jamii na kwamba wananchi wamchukie. Rostam alisema kuwa Mengi aliifilisi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kukopa deni lililofikia 28 Bilioni.

Wakati akimtuhumu Mengi alisahau kuwa na yeye aliinunua kampuni ya ngozi iliyokuwa chini ya umiliki wa Serikali.
Hata pale Rostam aliposhauriwa na watu kuwa kama anaona anazushiwa aende mahakamani kushtaki, alisema kuwa hawezi kwenda mahakamani kwa kuwa tuhuma dhidi yake ni za kutungiwa. Uamuzi wake huu ulitafsiriwa na wengi kuwa ilikuwa ni kama amezikubali tuhuma alizotupiwa za wizi wa mabilioni ya kodi za Watanzania kupitia EPA, Richmond na Dowans.

Pia, baada ya kuona ufisadi wake umeanikwa aliamua kuwaandama Dk. Harrison Mwakyembe kama kulipiza kisasi kwa sababu Kamati Teule ya Bunge aliyoiongoza kuanika wizi katika mkataba wa Richmond, ambao Rostam alikuwa na maslahi nayo. Vyombo vyake vikawa vikiwaandama Spika wa Bunge, Samwel Sitta, na viongozi wengine kutokana na sababu hiyo hiyo.

Kutokana na hali hiyo wadau wengi wametahadharisha harakati hizo za wawili hawa kurudi tena kwenye nafasi za uongozi wa nchi kuwa sawa na nchi kuruhusu awamu mpya ya uchotwaji mkubwa wa fedha za wananchi.

Huyu Rostam alipokuwa akijiengua kwenye Ubunge alisema kuwa ameamua kuachana na siasa za Tanzania kwakuwa ni siasa uchwara, sasa anapoamua kumuandaa mgombea Urais maana yake ni kushiriki katika siasa hizo hizo ambazo yeye aliziita kuwa ni uchwara. Inaonekana kuwa wakifanikiwa sasa hivi wataifilisi nchi kabisa, mchambuzi mwingine wa kisiasa alisema.


Kwa taarifa yako Mengi na Rostam hawana ugomvi. Wewe peke yako masikini ndiyo unayelalamika.
 
nasikitika tunaelekea kuiuza nchi mikononi mwa mabepar.kma lowasa akishinda tutarajie migodi na vitalu vya gesi kushikiliwa na akina Rostam na Lowasa
 
Rostam anatuona Watanzania mazwazwa. Ndo maana karejea tena
 
nazidi kusikitika zaid jinsi wasomi wanavyonunuliwa eti sababu ya pesa.hawajui kwamba pesa hizo wanazopewa sasa watazilipia na watalikost taifa kwa ujumla.na tusipo angalia vizur baada ya kushinda team lowasa tunaweza kuingia katika anguko la kiuchum tz coz utakua ni muda wa kurudisha gharama zote walizotumia ktk kampeni.watz 2THINK BIG.
 
ukitaka kumjua rosti tamu soma bandiko hili hapa chini

Mipango ya Kuuwawa kwa Mwakyembe

http://www.mwanahalisi.co.tz/print/slaa_mwakyembe_watishiwa_kuuawaMembe, Mengi, Mwandosya nao wamo IJP: Tuna taarifa hizo, tunachunguza Sheikh Yahaya Hussein naye ahusishwa

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini, Dk. Willibrod Slaa ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotishiwa kuuawa.
Mwingine aliye kwenye orodha hiyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, MwanaHALISI linaweza kuripoti.

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IJP), Said Mwema amethibitisha kuwa ana taarifa kuhusiana na tishio hilo na kwamba ofisi yake inazifanyia kazi.

"Ni kweli, jeshi la polisi linazo taarifa hizo za kuwapo kwa tishio la mauaji. Lakini nafikiri hilo ni jambo la kiupelelezi zaidi," alisema IJP Mwema katika mahojiano yake na gazeti hili juzi Jumatatu.

Hata hivyo, Mwema alikataa kulizungumzia suala hilo kwa undani, badala yake alielekeza gazeti hili kumtafuta Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishina wa Polisi, Robert Manumba.

Naye Manumba alipoulizwa alikiri kuwapo kwa tishio hilo lakini aliishia kusema, "Bado tunafanya uchunguzi."

Alipoulizwa hatua walizofikia katika uchunguzi huo, Manumba alisema, "Unapofanya uchunguzi kuna mambo mengi ya kuzingatia. Kuna kukusanya ushahidi. Kwa jumla, bado tunafanya uchunguzi," alisisitiza na kusema muda ukifika taarifa kamili itatolewa.
Kufichuka kwa tishio la mauaji ya watu hao mashuhuri, kumeibuka kufuatia barua ya kurasa saba iliyoandikwa na Dk. Mwakyembe ambaye sasa ni naibu waziri wa ujenzi kwa IJP Mwema.
Katika barua hiyo ya 9 Februari 2011, iliyobebwa na kichwa kisemacho, "Taarifa ya njama za kuondoa maisha yangu na ombi kwa jeshi la polisi kulinda haki yangu ya kikatiba ya kuishi," Dk. Mwakyembe anataja watu wengine mashuhuri wanaotishiwa kuuawa.

Hao ni mfanyabiashara mashuhuri nchini, Reginald Mengi, waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Melecela.

Dk. Mwakyembe anasema katika barua yake, "Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takribani mwezi mmoja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake – kwa maana ya wahusika na maudhui – hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa."

Anasema pamoja na hayo, bado ana imani kubwa na jeshi la polisi kuwa litaifanyia kazi taarifa hiyo bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa.

Msingi mkuu wa yeye kuamua kuvitaarifu vyombo vya dola, anasema Dk. Mwakyembe, ni taarifa alizozipata kutoka Songea, 22 Januari 2011 zinazolihusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa 21 Januari 2011 wakitumia gari linalodaiwa kuwa la wizara yake.

Gari hilo aina ya Land Cruiser lilikuwa na namba za usajili STK 6868, lakini baadaye namba ilibadilishwa na kusomeka STK 6869.

Gari hilo liliwateremsha "abiria" hao saba sehemu iitwayo Madaba na kisha kuchukuliwa na gari jingine Land Cruiser hardtop, Na. T 768 BDU hadi baa ya Top Inn mjini Songea.

Anawataja baadhi ya abiria waliokuwamo katika gari hilo kuwa ni raia wawili wa Somalia, Hafidh na Faraj, "kijana mmoja wa Kichagga" kwa jina Mustafa a.k.a "Master" Mkusa ambaye imeelezwa kuwa ni ofisa wa idara ya usalama wa taifa na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Ramika kutoka Tanga, ambaye inadaiwa ndiye "mtaalamu" wa kukaba watu.

Dk. Mwakyembe anaeleza katika barua yake kwa IJP, kwamba aliyepokea genge hilo la wahalifu mjini Songea, ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini, Rajabu Mtiula akiongozana na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Manya.

"Usiku wa Jumamosi 22 Januari 2011, kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo kwa gari aina ya Defender STK 2654, likiendeshwa na Zuberi Komba kwa lengo la kukutana na ‘mganga' Majungu (kabila Mdendeule) ambaye anaishi ndani ya mbuga ya wanyama (Selous Game Reserve with impunity,)" anaeleza Dk. Mwakyembe katika barua yake.

Anasema, "Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha wageni hao kwa mganga ambako walikaa siku saba wakitengenezwa. Walirejea Songea 29 Januari 2011 na kesho yake, 30 Januari 2011 wakaanza safari kurejea Dar es Salaam."

Anasema kutoka Songea hadi Mafinga, watuhumiwa wa njama za kuua walitumia gari Na. T 768 BDU ambalo walilitumia awali kutoka Madaba hadi Songea. Anasema walifika Mafinga saa mbili usiku na kukuta magari mawibili yakiwasubiri. Moja, Hilux Mayai ya kampuni ya Vodacom na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro.

Akiandika kwa kujiamini, Dk. Mwakyembe anasema, "…walipofika Morogoro walipokelewa na askari mmoja anayemtaja kwa jina la Sabasita. Hapo kundi likagawanyika: Watu wanne wakiwemo wale wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol T 845 ADH mali ya kampuni ya Caspian, na wengine wakabaki Morogoro."

Kampuni ya Caspian ni mali ya Rostam Aziz, mfanyabiashara, mbunge wa Igunga (CCM) na wakala anayejitaja kuwakilisha kampuni ya kufua umeme ya Dowans ya Costa Rica. Gazeti lilipomtafuta, hakuweza kupatikana.

Anamwambia Mwema kuwa, Mganga Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wake wanaweza kuongea naye kama walivyofanya waliompa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Dk. Slaa na wengine.

Anasema mganga huyo "ametengeneza dawa ya kuwapumbaza waliohukumiwa kifo na kuwa mfano wa mbwa mbele ya chatu" ili kukimbia hasira za wananchi pale mpango wa mauaji utakapotekelezwa.
Dk. Mwakyembe anamueleza IJP Mwema, kwamba awali mkakati wa kumuua Dk. Slaa ulipangwa kutekelezwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, lakini ulisitishwa kwa hofu ya kuingiza nchi katika machafuko.
"…utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka jana kuwa mmoja wa presidential candidates (wagombea urais) atakufa, ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makinisa. Utabiri huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango wenyewe," anasema.
Wiki mbili zilizopita, Sheikh Yahaya alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kutatokea vifo vya watu kadhaa mashuhuri wakiwamo wanasiasa na mwandishi mmoja wa habari mashuhuri nchini. Wakati Shekh Yahaya anatoa utabiri wake, Mwakyembe alikuwa katika wiki ya tatu tangu awasilishe malalamiko yake polisi.
MwanaHALISI lilipowasiliana na Sheikh Yahya ili kufahamu iwapo utabiri wake unatokana na kutumiwa na watu maalum waliomlipa fedha ili kufanikisha mkakati huo wa mauaji, mnajimu huyo alisema, "Watu wasubiri matokeo."
Alisema anachokifanya yeye ni unajimu na tayari amefanya hivyo katika matukio kadhaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuwako kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

"Nilitabiri Raila Odinga kuunda serikali moja na Mwai Kibaki Kenya. Yametimia. Nilitabiri CCM itapata msukosuko baada ya uchaguzi mkuu, imekuwa hivyo. Sasa hapo unahoji nini?

"…Sijataja jina la mtu, hivyo watu wasijihisi kwa utabiri wangu, ila wao wasubiri matokeo. Halafu ninyi MwanaHALISI mnafanya kazi nzuri. Ipo siku nitawaita hapa kuzungumza nanyi. Ila nayi msihofu, msubiri matokeo."

Naye Dk. Slaa alipoulizwa kuhusu mpango huo, kwanza alicheka, kisha akauliza: "Nani kakuambia?" Alipoelezwa kuwa ni taarifa zilizothibitishwa na jeshi la polisi, Dk. Slaa alisema, "Basi nadhani wao ndiyo wanajua wanaohusika katika suala hilo."

Katika barua yake kwa IJP, Dk. Mwakyembe anasema kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hassani alitumwa kutoka Dar es Saalam kwenda Dodoma, 5 Februari mwaka huu kwa "maandalizi" ya kikosi cha mauaji. Amesema tayari kikosi hicho kimefanya utambuzi wa nyumba yake aliyopangiwa kuishi na serikali.

Anasema, "Tarehe 6 Februari 2011, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkonga (T 360 AKU). Waliokuwa kwenye kikosi hicho ni wasomali wale wawili, mgeni mmoja wa kiume kutoka Uganda, Mustafa a.k.a ‘Master' na kijana mmoja ambaye tarehe 19 Januari 2011 aliwabeba wasomali hao kutoka Morogoro kwa gari aina ya VX Lands Cruiser T 656 APF. Kijana huyo ana shepu ya Kitusi na anaongea Kifaransa."

Jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe anasema, "Wahitimu hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na Kiwanda cha Mohammed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa, chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa MALKAZ na juu ni sehemu ya kuishi."

Anaeleza kuwa tarehe 5 Februari, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda. Mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Anaripoti kuwa walipokelewa kwa magari mawili: moja la polisi, PT 0288 – polisi ujenzi na la pili lenye namba za kibalozi T 69 CD 82 aina ya RAV 4. Anasema, jioni wakawa na mazungumzo ya kina na raia wawili wa Somalia ambao inadaiwa ni kutoka kundi la Al-Shabaab.

Dk. Mwakyembe anasema katika maelezo yake kwamba amepata picha ya kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho wameingizwa nchini.

Anasema, "Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka wanaharakati wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewe hoja kuwa maadaui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu."

Katika barua yake kwa IJP, Dk. Mwakyembe anasema kila siku hupata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili; anazitoa taarifa hizo kwa jeshi la polisi ili ziwasaidie katika upelelezi.

Kwanza, taarifa zinaonyesha raia hao wa kisomali waliingia nchini kutokea Kenya na walikwenda Dodoma kupitia njia ya barabara kwa kutumia gari aina ya RAV 4 (new model- T 816 AQS) tarehe 08 Januari 2011.

Pili, Dk. Mwakyembe anasema walipofika Morogoro walipokewa na askari Sabasita wa jeshi la polisi mkoani humo, ambapo walikaa katika hoteli mbili tofauti – Hillux Hotel na Top Life. Anamtaja aliyewafanyia booking wageni hao ni mmiliki wa Morogoro Hotel aliyemtaja kwa jina moja la Kari.
Tatu, Dk. Mwakyembe anasema magari waliyotumia wakiwa Morogoro, ni RAV 4 T 816 AQS, VX Land Cruiser STK 1287, Mercedez Benz (Station Wagon) T 874 BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T 218 BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T 656 APF na Nissan patrol T 845 ADH.

Wakiwa Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe anataja watu waliokuwa na mawasiliano na waliotumwa kuchukua roho yake kuwa ni "Masuhe wa Central Police Station (polisi kati), Fred Lowassa ambaye inadaiwa aliwapelekea mbuzi watatu huko Kiwalani tarehe 04 Februari 2011 na hata kuwatafutia gari VX Land Cruiser T 656 APF.

Anasema walipokuwa Dar es Salaam, tarehe 13 na 14, Januari wabaya wake walifikia nyumba Na. 551, Mtaa wa Chakechake, Upanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Rajab Mtiula, hakupatikana juzi kuzungumzia kuhusishwa kwake katika mikakati hiyo.
Gazeti lilipowasiliana na Fred Lowassa kueleza juu ya kuhusishwa katika maandalizi ya kifo cha Dk. Mwakyembe na wenzake alijibu, "Kaka katika mazingira ya kawaida tu, hilo jambo ni very serious (hilo jambo zito). Kuua ni tuhuma nzito.

Alisema, "Siku hizi kuna teknolojia ambako ukifanywa uchunguzi, itaonekana tu. Mimi nimekutana na mambo magumu sana maishani, lakini siwezi kufikia hatua ya kuua au kuhusika kuua."
Fred ambaye ni mtoto wa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alisema, "Yakinipata magumu, mwokozi wangu ni Mungu. Naomba Mungu, halafu huwa nasamehe. Siku zote huwa sipendi kuingia kwenye malumbano," alieleza.

Lakini Dk. Mwakyembe katika barua yake kwa IJP Mwema anasema, "Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe."
Taarifa zinasema kila aliyetajwa kuuawa amejulisha taarifa hizo na Dk. Mwakyembe kama ambavyo ameeleza katika maelezo yake polisi.

Gazeti toleo lenye makala hii


Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 March 2011

 
Mkiacha kutumia Vodacom mtakua mmemmaliza Rostam,na sasa kapewa eneo la polisi oysterbay
 
Hizi ni baadhi ya hoja nzito ambazo UKAWA wamejitoa ufahamu na kuzipuuza
 
Back
Top Bottom