TANZIA Rose Nyerere, Mtoto wa Mwisho wa J.K Nyerere afariki dunia

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,678
68,653
Umuofia Kwenu wana JF,

Kheri ya Mwaka Mpya!

Mtoto wa mwisho wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Rose Nyerere amefariki leo mjini Dar es Salaam.

Taarifa za duru za uhakika zinaarifu kuwa Rose amefariki katika hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam ambako alilazwa kwa muda mrefu. Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.

RJKN.jpg


KK,
MINJINGU.

Dar es Salaam. Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imepata msiba wa mtoto wao Rosemary Nyerere aliyefariki jana jioni jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wanafamilia aliyejitambulisha kwa jina la Sophia Nyerere ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa shangazi yake amefariki.
Mwananchi limewatafuta baadhi ya wanafamilia akiwemo Manyerere Jacton aliyethibisha kuwa ndugu yao amefariki.

"Ni kweli dada amefariki jioni hii, lakini taarifa rasmi itatolewa," amesema Manyerere.

Rosemary alikuwa miongoni mwa watoto saba wa Mwalimu Nyerere
 
Back
Top Bottom