VS![]()
![]()
Rose Asha Migiro na Halima Mdee nani zaidi
Tanzania kama kubahatika na kupendelewa tumefanikiwa lakini tumekuwa watu tusioweza kutumia vema nafasi tunazopata, pengine kutokuwa na utambuzi na ufahamu wa kutosha kwa uwajibikaji wa kujituma katika nafasi tulizopewa na kuelewa uzito stahiki unaotakiwa na jinsi werevu na kujituma kwa hali ya juu katika utendaji unaotakiwa katika kutumika nafasi adimu ambayo kwa ulimwengu mzima ni chanda cha dhahabu kwenye kisahani. Wanaopata heshima na sifa ni kutokana na kujituma si mradi kukalia kiti na kutabasamu.
Kwa miaka karibu mitano nimekuwa nikikodolea macho list ya wanawake bora na maarufu duniani kwa kiwango cha kimataifa, pamoja na Rose Migiro kushika nafasi pekee akiwa kama mwanamke wa kwanza UNO kuparamia kiti hicho, lakini hakubahatika hata kushika nafasi ya 100 kati ya 100 bora. Nilijiuliza na kuishia kukaukiwa cha kuandika na kusubiria nafasi nyingine kwa mwaka unaofuata hadi ilipofikia kutompa nafasi kwa ingwe nyingine.
Halima Mdee, hajashika nafasi pekee serikalini zaidi ya ubunge kutoka kambi ya upinzani, lakini bungeni alivyoonyesha ushupavu usio wa kawaida hadi kuwashikisha adabu viongozi waandamizi serikalini imeleta matumaini mapya hadi kushuhudiwa na dunia ambayo imempa tuzo stahiki, na labda mwanamke kama huyu Mdee angepata nafasi ile adimu na ya pekee katika historia ya wanawake katika Umoja wa Mataifa huenda angeweza kuingia bora 100 kwa miaka aliyokaa Migiro United Nation.
Inawezekana tumezoea kuwavimbisha vichwa wengi wetu bila stahili, na wapatapo nafasi inakuwa basi bora muda ukamilike aende, ni kwa haidhuri tu tumekuwa naye ofisini.
![]()
![]()
Ibarahim Lipumba na Tundu Lisu
- Ibrahim Lipumba ameshatikisa dunia kwa kuitwa kuitumika UNO kitengo cha uchumi kwa mwaka mmoja, huku ni kutambuliwa kimataifa kwa utumishi uliotukuka.
- Tundu Lisu ameshapata tuzo ya Kimataifa
Matukio kadhaa ambayo yametokea kimataifa na kushuhudiwa kutambulika kimataifa kwa baadhi ya watanzania kutoka vyama vya upinzani ni dira inayoleta matumaini makubwa kwamba hawajapata nafasi, wakiipata hata kuongoza nchi hii mapinduzi makubwa kimaendeleo yatatokea. Kwani kufanya mambo kwa mazoea kuna athari zake.
![]()
Hapa Tundu Lisu
anajaribu kumpa tuition kidogo Lukuvi.
Watu kama Lukuvi ni lazima waishi kwa kujikomba kutokana uwezo wao. Hawa watu jamani wanaendelea kuonesha uwezo mdogo kila muda unavyodogea mbele.