Rose Kamili, Askofu Kilaini wamshukia Dk Slaa

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Kauli ya Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dk Willibrod Slaa' imeendelea kutikisa, baada ya mke wake wa zamani (Rose) kuibuka na kusema kuwa Dk Slaa aliwadanganya wananchi.

Na Askofu Kilaini amesema Maaskofu hawanunuliki na Kanisa halifungamani na upande wowote wa kisiasa.
====

...Rose Kamili, Askofu Kilaini wamshukia Dk Slaa
Kauli ya Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dk Willibrod Slaa kuhusu hatma yake kisiasa imeendelea



===
Dar es Salaam. Kauli ya Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod Slaa kuhusu hatma yake kisiasa imeendelea kutikisa baada ya mke wake wa zamani, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamili alisema wakati Dk Slaa anatangaza kung'atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli.

Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa wa CHADEMA, alisema Dk Slaa aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri.

"Lowassa alisema ‘mimi nakushauri ujiunge na chama chochote'" alisema Kamili na kuongeza kuwa marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

"Mimi namshangaa anavyosema haongei na Lowassa… hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi?," alisema Kamili.

Kuhusu Sumaye, Kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita alipigiwa simu na kiongozi huyo akimuulizia namba ya Dk Slaa, baada ya kumtafuta kwenye simu yake bila mafanikio.

"Aliniuliza mbona simu yake haipatikani, nikampa akampigia wakaongea," alisema.

Mjini Bukoba, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini amesema anamshangaa Dk Slaa kutoa tuhuma dhidi ya maaskofu kwa kuwa aliwahi kuwa Katibu wa Baraza la Maskofu na anajua wanavyofanya kazi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi mjini Bukoba, Askofu Kilaini alisema Maaskofu hawanunuliki na kanisa halifungamani na upande wowote wa kisiasa huku akidai huenda kauli hiyo ilimponyoka.

Kauli ya Askofu Kilaini imetolewa ikiwa ni baada ya siku chache zilizopita aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Slaa kutangaza kustaafu siasa huku akiwatuhumu baadhi ya maaskofu kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa wagombea.

''Wanasiasa ni wachangiaji wazuri katika hafla mbalimbali za kanisa lakini hata siku moja huwezi kusema maaskofu wamenunuliwa Kanisa linashikilia maadili na kuombea amani kwa Taifa,'' alisema Kilaini

Pia Askofu Kilaini aliongeza kuwa matamko kama yaliyotolewa na Dk Slaa yanaweza kusababisha mkanganyiko kwenye jamii, huku akionya hatari ya dini kutumika kwenye mijadala kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Aidha alirejea mwaka 2000 kuwa baada ya vurugu kuanza kutokea Zanzibar na wananchi kukimbia, waliitana viongozi wa madhehebu yote ya dini na kutoa tamko la pamoja wakionya dini zisihusishwe kwenye harakati za kisiasa.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • IMG_20150904_041139.jpg
    IMG_20150904_041139.jpg
    757.3 KB · Views: 989
Rose Kamili bado anamachungu ya kutoswa kwa sababu ya tabiazake taka...
Huyu Kilaini kwann anakurupuks kuwaongelea/kusafisha wenzake bila kufanya utafiti? Kuna kitu wanafunika hapa...
 
fungukeni zaidi tuko mbali na magazeti



...ni Mke wa Slaa aibua mapya.

Adai katibu huyo wa zamani wa Chadema sasa anaifanyia kazi CCM baada ya kuahidiwa ubunge na uwaziri.

Mke wa zamani wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Rose Kamili.
Mke wa zamani wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Rose Kamili jana aliibuka na kumtuhumu mzazi mwenzake huyo kwamba anatumiwa kuvuruga upinzani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamili alitamka bila kuthibitisha moja moja kwamba mumewe huyo wa zamani anatumiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akihoji uadilifu wake katika jamii.

Lakini jana alipotafutwa kwa njia ya simu kujibu madai hayo ya chama chake kumtumia Dk. Slaa kuusambaratisha upinzani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema hana taarifa na hivyo apewe muda kabla ya kutoa taarifa kamili.

“Sina taarifa kama Rose Kamili kazungumza na vyombo vya habari leo. Ndiyo kwanza nasikia kwako, naomba unipe muda niweze kusoma yote aliyoyaeleza ndipo nikujibu,” alisema Nape.

Katika mkutano wake jijini Dar es Salaam juzi, Slaa aliyekuwa kimya kwa siku kadhaa alitangaza kuachana na shughuli za siasa kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa chama chake, hasa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais uliompa nafasi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea wa Chama hicho.

Dk. Slaa alimuelezea Lowassa kama mtu asiye na maadili wala sifa ya kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu anahusika katika tuhuma kadhaa za ufisadi ikiwemo ile kashfa ya zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyohusisha kampuni ya Richmond LLC na baadaye Dowans.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamili anayedai kuzaa watoto wawili na Dk. Slaa, alisema anachofanya sasa kiongozi huyo wa zamani wa Chadema, ni kukamilisha sehemu ya kazi aliyotumwa na baadhi ya makada wa chama tawala kwa nia ya kuisaidia katika kampeni za uchaguzi mkuu kwani ni kwa muda mrefu alikuwa akifuatwa na kuahidiwa ubunge na uwaziri pindi akikubali kuachana na Chadema.

Hata hivyo, Kamili naye hakuweza kufafanua kama naye kwa hatua yake hiyo ya kujitokeza hadharani kumshambulia mumewe huyo wa zamani, naye alikuwa katumwa, au ulikuwa ni utashi wake binafsi.

Aidha hakuweza kuweka bayana ni kwa nini hakujitokeza siku zote kuhoji uadilifu wa mume wake huyo wa zamani tangu alipojitokeza kugombea urais mwaka 2010 kupitia chama cha Chadema.

Alisema baadhi ya vigogo wa CCM ndiyo waliokuwa wakiongoza mpango huo, wakimuahidi Dk. Slaa vyeo hivyo huku yeye akiahidiwa kiasi kikubwa cha fedha kama akikubali pia kuachana na Chadema.

Hata hivyo, Kamili aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema katika Bunge lililovunjwa Julai 9 mwaka huu, alisema kuwa yeye alikataa ‘ofa’ hiyo na kubakia katika chama chake, lakini kwa anachokifanya Dk. Slaa sasa, ni dhahiri kuwa mzazi mwenzake amekubali kutumika na hivyo hatashangaa akimuona kwenye majukwaa ya kampeni za CCM ili kumchafua mgombea wa Ukawa na kukinadi chama tawala katika kampeni zinazoendelea.

Lakini katika mkutano wake na waandishi wa habari Dk. Slaa alitamka bayana kwamba anaachana na siasa na hana mpango wa kurudi CCM. Kamili alidai kwamba Dk. Slaa vilevile aliitwa na kigogo mmoja ndani ya Kanisa Katoliki na kushawishiwa akubali mpango huo wa kujiweka pembeni Chadema na kuitumikia CCM.

Alisema baada ya kumalizana na Dk. Slaa ndipo wakamgeukia yeye na kumtaka ahamie kwao (CCM) ili washirikiane katika kampeni za CCM.

“Mimi nimekataa... ila yeye amekubali na wakati wowote anaweza kutekeleza kazi aliyoianza kwa kupanda majukwaani kushiriki kampeni za CCM,” alisema.

Lowassa na ufisadi
Aidha alihoji Dk. Slaa kumuita mgombea urais wa Chadema kuwa ni fisadi, akimtaka ajihoji yeye mwenyewe kuhusu matendo anayoyafanya katika familia, kabla ya kuwahubiria wengine kuhusu maadili na misingi bora.

Kamili alisema kabla ya Dk. Slaa kuhoji mambo ya Lowassa ajihoji yeye mwenyewe kuhusu sababu zilizomfanya aondoke Baraza la Maaskofu Katoliki (Tec) akiwa kama Katibu mkuu na pia Kasisi wa kanisa hilo.

Aidha alikanusha taarifa zilizotolewa na Dk. Slaa kwamba yeye (Slaa) na familia yake wamekuwa wakila mihogo kama sehemu ya kutunza uaminifu wake, na kusisitiza kwamba kuwa siyo za kweli.

Kwa nini kajitokeza
Kamili alisema aliamua kujitokeza kuzungumza hadharani ni baada ya mzazi mwenziwe huyo kugusia masuala ya familia wakati alishaitelekeza kwa muda mrefu, pale alipoamua kuishi na mchumba wake mpya Josephine Mushumbusi.

Kwa mujibu wa Kamili, mbali na mzazi mwenziwe kuitelekeza familia yake, hakuwa, pia hajawahi kuwa na maisha magumu kiasi cha kula mihogo kama alivyodai, na kuongeza kwamba labda kama alikuwa anazungumzia watoto wake (Slaa) ambao amewatelekeza.

“Alisema yeye na familia yake wamekuwa wakila mihogo…hata kama mihogo ni chakula, watoto wangu hawajawahi kula mihogo hata kama aliwatelekeza labda watoto wake anaoishi nao. Huo ni uongo, ni upotoshaji. Atoe ufafanuzi kw Watanzania hao watoto anaowazungumzia ni watoto gani. Kama wewe ni muongo, huwezi siasa.” Kamili alisema

Kuhusu ndoa
Kamili alisema katika mkutano wa juzi, Slaa hakueleza kwa usahihi juu ya suala la ndoa kwa kudai kuwa serikali ya CCM ndiyo iliyoweka pingamizi dhidi ya maamuzi ya kufunga ndoa na mchumba anayeishi naye, Josephine Mushumbuzi.

Badala yake, Kamili alisema maneno hayo si ya kweli kwani yeye (Kamili) ndiye aliyeweka pingamizi hilo kwavile ndiye mke wa halali na kwamba, haiingii akilini kwa taasisi kama CCM kuweka pingamizi la ndoa ya mtu.
Alisema maneno hayo ni ya uongo kwani yeye ndiye aliyeweka pingamizi hilo kwa sababu ndiye aliyefunga naye ndoa na kwamba ingewezekana kuwekwa pingamizi na CCM iwapoa alifunga ndoa na chama hicho.

Alisema yeye na familia yake ya watoto wawili, Emiliana na Linus Slaa, wamekuwa wakimfichia siri nyingi lakini kwa taarifa hizo zimemfanya kuibuka huku akimtaka kuomba msamaha kwa kuwasema viongozi wa dini kwamba walipokea rushwa ya mamilioni kutoka kwa Lowassa.

Kugombea urais
Kamili alipinga madai ya Dk. Slaa kwamba hakuwa tayari kugombea nafasi ya urais kupitia Chadema, akisema ukweli wa suala hilo unadhihirishwa na ziara yake (Slaa) ya Ujerumani alikojifunza namna ya kuvaa na kujieleza mbele ya hadhara wakati wa kampeni za uchaguzi.

Aidha, Kamili alihoji ujasiri wa Dk. Slaa kumuita mgombea urais wa Ukawa, Lowassa kuwa ni fisadi anautoa wapi wakati yeye (Slaa) amejawa na matendo yanayotilia shaka uadilifu wake, baadhi yakiwa ni kumuacha mke wa ndoa (yeye Kamili) na kuishi na mwanamke mwingine.

Kadhalika, alidai sababu mojawapo ya Slaa kuondoka katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tec) ni kukosa uaminifu na hivyo, kamwe hastahili kumnyooshea kidole Lowassa kwa tuhuma za kuzushiwa kuhusu kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.


CHANZO: NIPASHE
 
Tatizo si la Maaskofu walipokea wala Slaa Aliyesema hadharani. Tatizo ni mentality ya mtoaji Mr.Low, yeye akichangia shughuli anahesabu kuwa kamununua mwenye shughuli. He's too Low to become a president.
 
Baba kilaini kila deal upo, escrow upon Kwa Mr Low upo pia? Hivi pesa wapeleka wapi?
 
Maaskofu tumewaona kwenye madili ya escew...hatushangai kuwaona kwenye foleni ya mgao wa Lowassa.
 
Slaa angeteuliwa kugombambia uraisi angeuza ukawa. The guy is too fake.Makomandoo wa ukawa wanaendeleza mapambano. Akumbuke tu inteligensia ya ukawa iko makini sana.
 
Back
Top Bottom